Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,605
- 3,176
Tatizo sio sheria mkuu, mfumo wetu wa kudai haju una tatizo. Kwa polisi wa Tanzania huwezi kumuuliza kwanini amekukamata, au kwanini anakusachi, ukijaribu kumbishia hata kwa maelezo kama mleta mada alivyoelezea utaingia kwenye matatizo tu.
Kuna watu wanapigwa hadu wanapoteza maisha na wengine kusababishiwa ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kubishana na polisi au ujinga wa polisi wa kutotambua mtuhumiwa halisi wakati wa jaribio la kumkamata mtuhumiwa.
Hivi kama polisi amekupiga au amekudharirisha bila sababu ya msingi utamfanya nini? Maana huwezi kwenda kumshtaki polisi bila kupitia kwa polisi tena ambapo kimsingi naona ni kupoteza muda tu.
Sio lazima kupitia polisi ili kufikisha suala lako mahakamani. Tunapitia polisi ili kukamata mtuhumiwa tu lakini kesi inaweza kufunguliwa bila kupita polisi na hasa kama polisi wenyewe wanahusika.
I stand to be corrected.
Tiba