Julius K. Nyerere: Ikulu ni pahali patakatifu, sio pango la wanyang'anyi

Julius K. Nyerere: Ikulu ni pahali patakatifu, sio pango la wanyang'anyi

Kama hayo yanatoka moyoni kwake n kwanini aliacha ubnge na kujarbu kukimbilia Ikulu? "Watu wanao kimbilia ikulu tuwangope kama UKIMWI"

Tehe tehee! Nyani haoni kundule, ndio alijaribu kukimbilia, je aliyejaribu kukimbilia na kufanikiwa kuingia vipi? Tena kwa kuchafua wenzake na kutumia vijisenti vya EPA!!!

Tofautisha kati kuombwa kwenda Ikulu na kujaribu kukimbilia Ikulu tena kwa ushawishi wa Vijisenti.

POLICCM oyeee
TBCCM oyee
 
Ukiondoa ushabiki dr slaa upo sawa mipango yetu yotw ipo bungeni ila TZ
 
"Mimi sikuchaguliwa na watanzania ili niifanye Ikulu kuwa Pango la wanyanganyi"

Mwenye kuweza kuweka clip ya hotuba yake tunaomba afanye hivyo.

Pili naomba tujadili hali ya ikulu yetu, je ni pango la wanyanganyi au ni mahali patakatifu?

Utakatifu wa Ikulu na heshima ya mahali hapo ilikuwa wakati wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa hai. Sasa hivi ikulu imegeuka kuwa jumba la kufanyia dili za kibiashara, kusainisha mikataba tata na kushindanisha uvaaji wa suti na mavazi mengine. Kwa ujumla maana halisi ya ikulu kwa sasa haipo limebaki jina tu.
 
Baba yetu,ulitujengea taifa lisilo na ukabila japo ni taifa lenye makabila zaidi ya 120, hukuacha udini katikati yetu,ulisimamia uchumi wa nchi na ufisadi haukuonekana katika kipindi chako ikulu haikuwa inatorosha wanyama wetu wa polini kwenda nje ya nchi, hukufanya propaganda za kisiasa kama vile ikulu inavomwita Lipumba kwenda ikulu na kumpa nobel ya amani, wakati huo huo ikulu haitaki kuunda tume ya kijaji kuchunguza mauaji ya Arusha kwa njia mlipuko wa bomu,tulikuwa hatubambikizwi kesi za ugaidi....


Ikulu sasa ni mahali panapofanyika mikataba ya kuhujum madini,ges,ardhi, wanyama wa polini nk..ccm inabaka demmokrasia, polisi imeruhusiwa kutupiga tu....Baba yetu, watanzania hatupo kama vile ulivotuacha, ila tutajikomboa hivi karibuni...chama chako kitapumzika, likitimia hili, usitulaum watanzania, utupongeze kwa kurejesha heshima ya ikulu yetu.....
 
Poleeeee! maana umevuta hisia kama uko mbele ya kaburi la Baba wa Taifa!
 
naona unataka kupigwa na kitu chenye ncha kali. na kutolewa hizo kucha na meno bila kiganzi.
 
Sijui ni lini Wadanganyika mtafufuka akili zenu na kuacha kuishi chini ya uvuli wa huyu marehemu
 
Neno "mahari" ulikua unamaanisha "mahali"?

"Mahari" maana yake ni mali,au kitu cha thamani kitolewacho na mwanaume km ada ya kumuoa mwanamke!!!!!! MFANO mtu anaweza kutoa mahari ya ng'ombe,pesa,nk ili amuoe bint na kuwa mke wake!!

Kwahiyo neno "mahari" haliendani kabisa na muktadha uliokua unauzungumzia kwenye uzi huu!nadhan ulikusudia kuandika "mahali/mahala"
 
umesema vyema kaka, ikulu ya jk inanuka dhambi na dam za watu, ila mungu atatulipia hapahapa duniani
 
Baba yetu,ulitujengea taifa lisilo na ukabila japo ni taifa lenye makabila zaidi ya 120, hukuacha udini katikati yetu,ulisimamia uchumi wa nchi na ufisadi haukuonekana katika kipindi chako,ikulu yetu,wanyama wetu hawakutoroshwa kwenda nje ya nchi, hukufanya propaganda za kisiasa kama vile ikulu inavomwita Lipumba ikulu na kumpa nobel ya amani wakati huo huo ikulu haitaki kuunda tume ya kijaji kuchunguza mauaji ya Arusha kwa njia mlipuko wa bomu


Ikulu sasa ni mahara panapofanyika mikataba ya ya kuhujum madini,ges,ardhi, wanyama wa polini nk..ccm inabaka demmokrasia, polisi imeruhusiwa kutupiga tu....Baba yetu, watanzania hatupo kama vile ulivotuacha, ila tutajikomboa hivi karibuni...chama chako kitapumzika, likitimia hili, usitulaum watanzania, tupongeze kwa kurejesha heshima ya ikulu yetu.....

Una hoja lakini mh.... R na L ni tatizo
 
Neno "mahari" ulikua unamaanisha "mahali"?

"Mahari" maana yake ni mali,au kitu cha thamani kitolewacho na mwanaume km ada ya kumuoa mwanamke!!!!!! MFANO mtu anaweza kutoa mahari ya ng'ombe,pesa,nk ili amuoe bint na kuwa mke wake!!

Kwahiyo neno "mahari" haliendani kabisa na muktadha uliokua unauzungumzia kwenye uzi huu!nadhan ulikusudia kuandika "mahali/mahala"

Asante kwa masahihisho, imerekebishwa tayari...
 
Back
Top Bottom