Kumbe hii kasumba ya mwenye pesa kuonekana mwizi imeanza kututafuna miaka mingi sana, kama unaamini mtu ameiba, na ushahidi unao, mpeleke mahakamani, shida iko wapi?!
Lakini kumnyima haki zake kwa madai ya kihisia, kwasababu tu anaonekana ana pesa ni kumuonea. Lowassa amevumilia mengi toka kwenye jamii ya kishamba iliyokuwa nyuma ya fikra zake za mitikasi ya kujitafuta maishani.
- Jamii inayoona umaskini ni sifa, ndio maana utaskia fulani akijiita mimi mtoto wa maskini. Usipokuwa jasiri mtanzania unaweza kuacha kupambania maisha yako kwa kuogopa kuitwa mwizi!.
Ajabu kuanzia miaka hiyo mpaka miaka ya karibuni bado akawa anaitwa fisadi, kumbe tumerithi tabia ya kuhukumu kwa hisia bila udhahidi toka enzi za Nyerere, tukawa bado tunaishi nayo mpaka sasa, hili ni tatizo la jamii ya kitanzania - awe mpinzani au chama tawala.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app