Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Wakati mwingine, tukubali kung'atuka. Hii Viseo Mzee mwenzangu ina ujumbe gani kwetu wasikilizaji. HaielewekiMwalimu Julius Nyerere historia yake ni kubwa sana.
Walioandika maisha yake wameandika vitabu vinne zaidi ya kurasa 1000.
Bahati mbaya sana kitabu hiki hakikuweka mengi ambayo yalihusu historia ya Mwalimu na Waislam wa Tanganyika.
Sijui kwa nini.
Kukosekana kwa hili kumeondoa utamu na ladha katika maisha na historia ya Baba wa Taifa kama alivyoishi na watu wa Dar-es-Salaam.
Historia ina kawaida ya kujirudia.
Wakati mwingine mapenzi ya watu kwa viongozi wao yanafika mbali sana.
Sikiliza kisa cha Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU 1954 - 1958:
View: https://youtu.be/cDXRaONNaCY?si=cT3yTTxutMuBv5Gb
Miaka zaidi ya 20 amakufa,na miaka zidi ya 30 tangu alipoacha na na uraidi,mbona huo utajiri siuoni,ach kulia lia pambana mtoto wa kiume utaolewa bure.Nyerere alikuwa ni mnyama hana utume wowote, alitesa sana waliokuwa wakimpinga na alitutia umasikini wa kutupwa na kufanya wabongo kuwa wavivu wa kutupwa kutegemea kila kitu wafanyiwe na serikali bila kuchangia.
Mbuzi weweMiaka zaidi ya 20 amakufa,na miaka zidi ya 30 tangu alipoacha na na uraidi,mbona huo utajiri siuoni,ach kulia lia pambana mtoto wa kiume utaolewa bure.
Wakati mwingine, tukubali kung'atuka. Hii Viseo Mzee mwenzangu ina ujumbe gani kwetu wasikilizaji. Haieleweki
Narumuk,Wakati mwingine, tukubali kung'atuka. Hii Viseo Mzee mwenzangu ina ujumbe gani kwetu wasikilizaji. Haieleweki
Mpaji...Pamoja na madhaifu yake mengi, ila mwalimu Nyerere alikua genius sana kuweza kudhibiti ukanda na udini haikua kazi ndogo
Ili nijue tatizo la udini ni mpaka nisome kwenye kitabu chako?Ukitaka kujua tatizo la dini ni lazima usome hii sehemu ya tatu ya kitabu
Mpaji...Ili nijue tatizo la udini ni mpaka nisome kwenye kitabu chako?
Katika hali ya kawaida siwezi fanya observation?
Mtakatifu Nyerere ndiye binadamu wa kwanza duniani kuyaunganisha zaidi ya makabila 120 kuwa kitu kimoja.Mwalimu Julius Nyerere historia yake ni kubwa sana.
Walioandika maisha yake wameandika vitabu vitatu zaidi ya kurasa 1000.
Bahati mbaya sana kitabu hiki hakikuweka mengi ambayo yalihusu historia ya Mwalimu na Waislam wa Tanganyika.
Sijui kwa nini.
Kukosekana kwa hili kumeondoa utamu na ladha katika maisha na historia ya Baba wa Taifa kama alivyoishi na watu wa Dar-es-Salaam.
Historia ina kawaida ya kujirudia.
Wakati mwingine mapenzi ya watu kwa viongozi wao yanafika mbali sana.
Sikiliza kisa cha Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU 1954 - 1958:
View: https://youtu.be/cDXRaONNaCY?si=cT3yTTxutMuBv5Gb
Kudhibiti ukanda na udini haikuwa kazi ndogo.Ungekuwa wewe usingeweza Mkuu wangu.Mwalimu apewe maua yake.Bila Mwalimu kusingekuwa na wakristu mijini.Mwalimu alifanikiwa kufanya intergration ya hali ya juu kabisa.Hufurahii haya mkuu wangu?Narumuk,
Hiyo video imetanguliwa na maelezo naeleza ukubwa wa historia ya Nyerere na vipi waandishi wa historia yake walivyoipunguza kwa kukosa kueleza jinsi alivyoingiliana na watu wa Dar-es-Salaam.
Laiti wangefanya hivyo wangeijua historia kama hii ya Sheikh Suleiman Takadir alipomnyanyua Nyerere na kumtia kwenye daraja la Utume kwa Bara la Afrika.
Utume anatoa Mwenyezi Mungu.
Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kwa hili amelipiku Kanisa kwa mbali sana kwa kutoa cheo cha "Mwenye Kheri" cheo wanachotoa binadamu.
Kwenye video naeleza nguvu ya chama cha TANU kupitia Tawi la Mtaa wa Mvita.
Kwenye video naeleza jinsi TANU ilivyokuwa na mbinu ya kumzingira Mwingereza.
Serikali imempiga marufuku Nyerere asifanye mkutano.
TANU inapiga taarab na kuwaalika watu waende kusikiliza na katika mkusanyiko ule Nyerere anasalimiana na wananchi.
Kwa kitendo hiki Nyerere bado anaonekana na wananchi wakiwa nyuma yake.
Njama za Gavana Edward Twining zinaambulia patupu.
Ikiwa bado hujaelewa nifahamishe.
Nan...Mtakatifu Nyerere ndiye binadamu wa kwanza duniani kuyaunganisha zaidi ya makabila 120 kuwa kitu kimoja.
Mtakatifu Nyerere kila alilolifanya hata kama lilikuwa kosa lilikuwa na nia njema kwa maslahi ya taifa la Tanzania.
Hakuna mbaguzi wa kidini atampenda mtakatifu Nyerere kwa sababu mtakatifu Nyerere angependa kuibadili hii nchi iwe ya dini yake kusingekuwa na wa kumzuia.
Mtakatifu Nyerere alikuwa mzalendo kwelikweli na aliipenda nchi hii upeo.
Mtakatifu Nyerere ndiye nembo ya uadilifu ya bara la Afrika,hakujilimbikizia mali wala kuuza raslimali za taifa letu.
Alichukia wezi,mafisadi, wadini na wajinga wore wenye nia ya kuligawa taifa.
Fikra na mawazo ya mtakatifu Nyerere ziendelee kudumu
Nan...Kudhibiti ukanda na udini haikuwa kazi ndogo.Ungekuwa wewe usingeweza Mkuu wangu.Mwalimu apewe maua yake.Bila Mwalimu kusingekuwa na wakristu mijini.Mwalimu alifanikiwa kufanya intergration ya hali ya juu kabisa.Hufurahii haya mkuu wangu?
Legacy ya Mwalimu haiwezi kufutwa kizembe maalim.Ni kiongozi ambaye Africa haijawahi pata mfano wake.Kwa uelewa wako ukipewa nafasi ya kumlinganisha na marais wote wa Tanzania,yupi anamzidi Mwalimu intergrity na uzalendo?Nan...
Huwa kuna mambo mengine napata shida kuyaeleza kwani najisikia vibaya.
Haya ni yale ambayo wengi mmeyaamini kutokana na mliyojifunza katika historia iliyokuwa si ya kweli.
Hapajakuwa na tatizo baina ya makabila.
Hayo mengine uliyoeleza inahitaji usome hizo rejea nilizoweka: Bergen, Sivalon na Njozi.
Utakutana na mambo ambayo hukuwa unayajua.
Legacy ya Mwalimu haiwezi kufutwa kizembe maalim.Ni kiongozi ambaye Africa haijawahi pata mfano wake.Kwa uelewa wako ukipewa nafasi ya kumlinganisha na marais wote wa Tanzania,yupi anamzidi Mwalimu intergrity naNan...
Huwa kuna mambo mengine napata shida kuyaeleza kwani najisikia vibaya.
Haya ni yale ambayo wengi mmeyaamini kutokana na mliyojifunza katika historia iliyokuwa si ya kweli.
Hapajakuwa na tatizo baina ya makabila.
Hayo mengine uliyoeleza inahitaji usome hizo rejea nilizoweka: Bergen, Sivalon na Njozi.
Utakutana na mambo ambayo hukuwa unayajua.
Nyerere hakuingizwa kwenye harakati kwa kuonewa huruma,he earned it kwa merits mzee!Nan...
Hapajakuwa na tatizo la dini baina ya Waafrika wenyewe.
Laiti lingekuwapo isingewezekana Nyerere kutiwa katika uongozi wa TAA 1953 na TANU ikaundwa 1954 Nyerere akiwa kiongozi mkuu.
Historia hii ya kikao cha Nansio nyumbani kwa Hamza Mwapachu kuweka mipango ya kumuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA nimeieleza mara nyingi sana.
Kitabu cha Abdul Sykes kimeeleza hili kwa kirefu.
Kwa bahati mbaya historia hii haikuwa inafahamika.
Unaeleza fikra zako kutokana na historia uliyosomeshwa ambayo haikuwa sawa.
Angalia video hiyo kipindi cha TBC1 naeleza vipi Nyerere alivyochaguliwa kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Unaweza kusoma historia yote ya Mwalimu Nyerere hapa:
mohamedsaidsalum.blogspot.com.
Mohamed Said
MWANAHISTORIA NA MWANDISHI . HISTORIA YA TANZANIA KWA UKAMILIFU WAKE . . SUBSCRIBEyoutube.com
View: https://youtu.be/oLkefadOoJ0?si=EoMPlmY2QdWclftV
Legacy ya Mwalimu haiwezi kufutwa kizembe maalim.Ni kiongozi ambaye Africa haijawahi pata mfano wake.Kwa uelewa wako ukipewa nafasi ya kumlinganisha na marais wote wa Tanzania,yupi anamzidi Mwalimu intergrity na uzalendo?
Nan...Legacy ya Mwalimu haiwezi kufutwa kizembe maalim.Ni kiongozi ambaye Africa haijawahi pata mfano wake.Kwa uelewa wako ukipewa nafasi ya kumlinganisha na marais wote wa Tanzania,yupi anamzidi Mwalimu intergrity na uzalendo?