Mwalimu Kambarage Nyerere, kama mtu, alikuwa ni mchakato...
Historia haitengenezi watu, watu wanatengeneza historia.
Historia ni uso wa juujuu wa tafsiri za muktadha wa sura za watu/jamii, matendo na matukio/sura ya utukufu wake.
Watu wanaitengeneza 'historia' kwa mujibu wa ule muktadha wa 'maadili na miiko' ujayo na/kwa 'mila na desturi' -- mila na destiri zinazoshindanishwa kimapana ya nyakati na matukio na utashi--'Wakati-Jamii-Machaguo ya Kitaasisi-Matukio'....
'Mila na desturi' ni mambo yajayo na
kadiri ya kiasi cha mwangaza/Elimu ama mapokeo ya jamii--lakini mwangaza ni jambo kuu kuliko 'mila na desturi' yeyote.
Kambarage Nyerere alikuwa ni 'Mtu wa Mwangaza'--watu wa mwangaza wananamna ya kutizamwa na kubayanishwa asili ya matendo yao, na basi nguzo za imani zinazokadirisha mapana ya 'dhamira, uono na vina vya tafsiri' kwa ajili ya kujichagulia kwao..
Hili linafanya sura sahihi ya kubayanisha muktadha wa wito, matendo na urithi/legasi ya mtu wa mwangaza kuwa na ufundi wake mahususi--si jambo la hoja, mijadala na midahalo.
Ufundi huu unaitwa Elimu 2.0: Uono na ufikirifu mifumo.
Mambo ya elimu 2.0 na Elimu 3.0 ndiyo yanaweza kubangulia undani wa wito, matendo na legasi ya Mwalimu Nyerere. In Shaa Allah, hili tunakuja kulifahamu ilivyobora wakati muafaka; na linatengeneza kitovu cha 'kuifumua historia mbovu' na 'vina visivyo sahihi vya tafsiri ya wito, matendo na legasi'--Hata ya Mwalimu Nyerere; kwa kuwa kuna upande wa ndani wa mambo ambavyo watu wa namna hii ama ile, silika hiii ama ile, imani hii ama ile hongozwa kukadirisha 'Jaala' ya 'Waja Wema'...
Kwa hivyo hata mambo ya kukadirisha muktadha na kadiri ya 'Utume' wa mtu fulani ni jambo la 'Usanii' tu; lina makusudi yake--yanaweza kuwa ni 'mema' ama 'si mema hasa'. Inategemeana na upeo wa mtu kiakili, kihisia na kiroho.
Watu wa mapana hasa--mapana hasa ya kiakili, hisia na kiroho--watu wa Elimu 3.0 ndiyo wenye 'Utashi wa kweli' na 'Hekima'.
Hawa wakidhihiri hekima hiyo kwa umma ndipo ndipo umma utazinduka na kuzifahamu mbichi na mbivu za ustaarabu na ustawi wao...
Watu wa hekima hawafanyi vikundi vya mipango na hadaa, bali hawa hasa ni walinzi na waongozeaji wa hatma za jamii, mataifa na tawala. Kuwa mmoja wao si suala la 'maombi na kukubaliwa' ili kuifanya 'Taasisi fulani'; watu hawa 'hujichagua/kujichagulia wenyewe' na 'kufanya yao'--husaidiana kwa sura ya wazi na sura isiyo ya wazi kuitengeneza njia ya 'dhamira zao njema'.
Historia ndiyo inaweza kupotosha isipoweza kubaini ama kuotea 'matendo ya ndani' ya 'washirika' katika kuongozea umma -- kuongozea umma katika utu bora na maendeleo...
Siku si nyingi karibia kila kitu kitafahamika kuhusu 'Uhuru wa Ndani' wa wanajamii na 'Ushirika katika Imani ya UTU wema'--jambo linalokwenda kuwa chachu kuu ya mageuzi na mapinduzi ya kijamii Tanzania, Afrika na Duniani...
'Utume wa Nyerere' ni fumbo la Imani kwa watu 'wasio na macho'--kusubiri wengine wawape tafsiri ya mambo...
'Utume wa Nyerere' ni fumbo la kuitika wito wa kudhamiria UTU bora, Amani na Mapenzi mema Duniani.
'Utume wa Nyerere' ni fumbo la kubidi kufumbuliwa kitendawili cha 'Mapinduzi'-- Mapinduzi ni 'Muda wa Ufunuo', na hali 'mapinduzi endelevu' ni 'ukuwakujia wa UTU bora', 'Amani' na 'Mapenzi mema duniani'...
Hmmm