Necromancer
JF-Expert Member
- Sep 20, 2018
- 3,187
- 3,138
Nan...
Umesema kweli "legacy" ya Mwalimu ni kubwa.
Kitabu cha Abdul Sykes kimepata umaarufu sababu yake ni Nyerere.
Kitabu kimeeleza yale ambayo Nyerere mwenyewe hakupata kuyasema wala mwanahistoria yeyote kuyaandika.
Hiki ndicho kilichowavutia watu wengi.
Lakini wako waliofadhaishwa na kitabu hiki kwa kuona kuwa Nyerere anagawana historia yake na watu ambao wao hawakupata kuwasikia hata siku moja.
Wako waliojiuliza mbona historia hii tunayosoma leo haikusomeshwa?
Iweje kadi za TANU tatu za mwanzo mbili ni za ndugu wawili khalis Abdulwahid na Ally Sykes?
Nini maana ya jambo hili?
Hili si suala la uadilifu au uzalendo wa Nyerere.
Maswali ninayoulizwa kote vyuoni ninapozungumza ni imekuwaje taifa likapoteza historia yake yote ya wazalendo wake waliopigania uhuru?
Prof. Haroub Othman hili lilimtatiza.
Angalia video hiyo namzungumza Prof. Haroub alivyotafuta maelezo kutoka kwa Mwalimu Nyerere:
View: https://youtu.be/lCyNc0C46Zo?si=X11DvnNUTCtbaOak
Lazima ukubali kuwa kila movie ina starring wake.Nyerere hawezi kugawana historia na wanaharakati mzee!