Inside,
Tuanze na hili la udini.
Bila shaka unakusudia Uislam.
Hili wala usiwe na shaka.
Nimeandika kitabu sasa maarufu kitabu hiki kimechapwa mara nne.
Kitabu kinaitwa: ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes The Untold Story of the
Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press London, 1998.
Sababu ya kuandika kitabu hiki ni pale historia iliyoandikwa ya harakati za uhuru ilifuta mchango wa
Waislam.
Nimeweka bold kwa makusudi na kukudhihirishia kuwa hilo ambalo wewe unaliita udini hakika ni Uislam na ndiyo nililokusudia.
Ingekuwa kauli na maandishi yangu ni chuki dhidi ya Nyerere TBC, AZAM, ITV na vyombo vingine vya habari visingekuwa vinakuja kwangu kwa ajili ya kufanya vipindi vinavyomuhusu Nyerere.
Angalia picha hiyo hapo chini nafanya kipindi cha Nyerere Day nimesimama Mtaa wa Stanley na Sikukuu mbele ya nyumba ya Abdul Sykes ambayo Nyerere alifikishwa na Kasella Bantu kuja kutambulishwa kwa Secretary na Act. President wa TAA Abdulwahid Sykes mwaka wa 1952.
Hapo nimezungukwa na watu wengi sana wamevutiwa kuona camera za TV na mimi nazungumza historia ya Nyerere na Abdul Sykes.
Watu wamenizunguka mimi na Jaffar Mponda Mtangazaji wa AZAM wanatusikiliza.
Wamepigwa na butwaa kusikia kuwa Nyerere na Mama Maria waliishi hapo.
Nyumba hiyo ninayoizungumza haipo hivi sasa badala yake kuna ghorofa.
Huwezi kuonyesha chuki dhidi ya Baba wa Taifa TV ikakurekodi na kurusha kipindi Watanzania na dunia wakione.
Kinachokuumiza wewe na mko wengi ni kwa nini historia ya Mwalimu Nyerere kote kazungukwa na Waislam?
Nataka nikufahamishe kitu.
Huko ulikotaja Ujiji, Buguruni na baadhi ya misikiti ya Dar es Salaam huko siko ninakoheshimika.
Mimi naheshimika kwenye Vyuo Vikuu vinavyosomesha African History, Marekani na Ulaya.
View attachment 3001350