Julius Nyerere Mtume wa Afrika 1950s - Julius Nyerere Mtakatifu Mwenye Kheri 2000s

Mwalimu Nyerere angeamua angeuza nchi, angeuza bandari, angeuza mbuga za wanyama, angeuza kila kitu.

Mpeni Mwalimu Nyerere maua yake.
Mwingine kapewa nchi miezi 24 tayari kauza Bandari,kauza NGORONGORO,Kauza KIA,Kauza Misitu........Nyerere bado ataendelea kuwa number moja mpaka kesho.
 
Nan...
Sifa zote ulizompa Mwalimu anastahili na mimi nimezieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

Lakini ukweli utabakia ukweli hauwezi kufutika.

African Association iliasisiwa na Kleist Sykes mwaka wa 1929.

Mwaka wa 1933 akaasisi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na vyama hivi viwili vilishirikiana katika kupambana na ukoloni wa Muingereza.

Ukiikataa historia hii tayari unaingia katika matatizo makubwa.

Walioikwepa historia hii leo ndiyo hawa wanahangaika na Mohamed Said.

Mohamed Said anawajibu na kuwaeleza historia ya kweli.

Sasa ikiwa huzikubali Nyaraka za Sykes utakubali nyaraka za nani?

Mwalimu Nyerere kama atakuwa na nyaraka za historia ya TANU basi zitakuwa kuanzia 1953.

Mimi sijaziona popote hata Maktaba ya CCM Dodoma hazipo.

Mimi nimeziona Nyaraka za Sykes zenye historia ya harakati kuanzia 1924.
 
Nakushauri uangalie movie ya Black Hawk dawn.kuna Phrase inasema "history remembers only Kings and not warriors"na hii ndo Kanuni ya dunia.Umar alipigania sana uislam lakini anayeongelewa ni mtume
 
Nakushauri uangalie movie ya Black Hawk dawn.kuna Phrase inasema "history remembers only Kings and not warriors"na hii ndo Kanuni ya dunia.Umar alipigania sana uislam lakini anayeongelewa ni mtume
Nyerere was King Sykes etal were warriors.History remembers Kings only.
 
Historia hukumbuka wafalme na si wanajeshi.Aliyeshinda vita ya Uganda ni Nyerere na si Msuguri wala Sarakikya
 
Pamoja na kwamba hayati Nyerere alikuwa na mapungufu yake ni mazuri mengi aliyofanya!
 
Nakushauri uangalie movie ya Black Hawk dawn.kuna Phrase inasema "history remembers only Kings and not warriors"na hii ndo Kanuni ya dunia.Umar alipigania sana uislam lakini anayeongelewa ni mtume
Nan...
Mimi sina tatizo fikra za wengine wala sitaingia katika hayo mengine.

Nimeandika kitabu na kimepokelewa vyema.

Kleist Sykes na wanawe wamo katika Cambridge Journal of African History na halikadhalika katika Dictionary of African Biography.

Taifa limetoa Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Abdul na Ally Sykes kwa mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Afisa wa Ikulu aliyekwenda kuonana na Ally Sykes kumtaarifu kuhusu hili alimuuluza Ally Sykes, "Kwani Bwana Ally nini mmefanya?"

Ally Sykes alimpa kitabu cha Abdul Sykes akamwambia yote waliyofanya katika historia ya Tanganyika yamo ndani ya kitabu hicho.

Kitabu hiki toka kichwape 1998 kishachapwa mara nne.
 
Historia hukumbuka wafalme na si wanajeshi.Aliyeshinda vita ya Uganda ni Nyerere na si Msuguri wala Sarakikya
Nan...
Hayo hayahusiani na niliyoandika mimi.

Mimi nimesahihisha historia iliyokuwapo kuhusu uhuru wa Tanganyika.

Historia hii ndiyo tunayojadili leo si historia ile iliyokuwa na upungufu mkubwa.
 
Nyerere aliiacha nchi ina kila kiwanda cha wakati huo.

lakini viongozi waliofata ni chenga
 
Nyinyi ndio misukule yenyewe
Gamm...
Hapana haja ya kutumia lugha kali.
Tujitahidi kuisomesha historia ya TANU kwa utulivu na lugha ya kuwavutia wasomaji.

Jambo lolote ukilitia upole litapendeza.

Wao hadi sasa wameshaujua ukweli kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika ilifanyiwa khiyana.

Hawa wanajua kwa yakini kabisa ya nafsi zao kuwa Mohamed Said ameisahihisha historia ya Tanganyika.

Niliombwa nifanye kipindi cha Nyerere Day.

Kipindi kilikuwa cha Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere ambacho kilirushwa na AZAM TV.

Mtangazaji Jaffar Mponda alitaka twende Mtaa wa Stanley na Sikukuu aone nyumba ya Abdul Sykes ambayo Mwalimu Nyerere alipelekwa kujulishwa kwake na Joseph Kasella Bantu mwaka 1952.

Nyerere akaja kuishi nyumba hii baada ya kuacha kazi ya ualimu mwaka wa 1955.

Iko picha nipo hapo lakini Dar-es-Salaam ile ya miaka ya 1950 si hii ya leo.

Nyumba ndogo hazipo tena.

Ni ghorofa ndefu kila upande wa mtaa pamoja na nyumba ya Abdul Sykes ni ghorofa.

Jaffar Mponda alitaka tuanze kipindi chetu hapo.

Tulipofika nilimuonyesha Jaffar Mponda kuwa ile nyumba ya Abdul Sykes ambayo Nyerere aliishi hapo baada ya kuacha kazi mwaka wa 1955 ni hilo jumba mbele yetu maofisi na juu ni nyumba za kupanga.

Mtaa wa Stanley ulibadilishwa jina na kuwa Aggrey Street kwa heshima ya Dr. Kwegyir Aggrey kutoka Ghana.

Dr. Aggrey alikuja Tanganyika mwaka wa 1924 na alikutana na Kleist Sykes, baba yake Abdul.

Alikuwa Dr. Aggrey ndiye aliyempa Kleist wazo la kuunda African Association.

African Association ndiyo iliyounda TANU 1954.

Mtaa huu umebadilishwa jina unaitwa Max Mbwana lakini kibao cha jina jipya hakijawekwa.

Kuna mtu anaeweza kuipinga historia hii?
Waangalie video hii ya TBC.


View: https://youtu.be/qgo7OpTu8eI?si=u3cSI9x9G1-o5lgH
 
Nimeishia kwenye heading na nimegundua harufu ya udini, dhihaka na chuki zako dhidi ya nyerere..
Katika chuki unataka kujiheshimisha na wafuasi ktk viambaza vya mtoro, idrisa, ujiji na buguruni kama sio mwembechai.
Cc Nguruvi3
 
Umeandika kwa tafsida, sijaambulia kitu
 
Kama kawaida yako ukikaa kidogo lazima utengeneze thread ya kumdogosha Mwl Nyerere. Unapata nini kwa kufanya yote haya?
 
Nimeishia kwenye heading na nimegundua harufu ya udini, dhihaka na chuki zako dhidi ya nyerere..
Katika chuki unataka kujiheshimisha na wafuasi ktk viambaza vya mtoro, idrisa, ujiji na buguruni kama sio mwembechai.
Cc Nguruvi3
Inside,
Tuanze na hili la udini.
Bila shaka unakusudia Uislam.

Hili wala usiwe na shaka.
Nimeandika kitabu sasa maarufu kitabu hiki kimechapwa mara nne.

Kitabu kinaitwa: ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press London, 1998.

Sababu ya kuandika kitabu hiki ni pale historia iliyoandikwa ya harakati za uhuru ilifuta mchango wa Waislam.

Nimeweka bold kwa makusudi na kukudhihirishia kuwa hilo ambalo wewe unaliita udini hakika ni Uislam na ndiyo nililokusudia.

Ingekuwa kauli na maandishi yangu ni chuki dhidi ya Nyerere TBC, AZAM, ITV na vyombo vingine vya habari visingekuwa vinakuja kwangu kwa ajili ya kufanya vipindi vinavyomuhusu Nyerere.

Angalia picha hiyo hapo chini nafanya kipindi cha Nyerere Day nimesimama Mtaa wa Stanley na Sikukuu mbele ya nyumba ya Abdul Sykes ambayo Nyerere alifikishwa na Kasella Bantu kuja kutambulishwa kwa Secretary na Act. President wa TAA Abdulwahid Sykes mwaka wa 1952.

Hapo nimezungukwa na watu wengi sana wamevutiwa kuona camera za TV na mimi nazungumza historia ya Nyerere na Abdul Sykes.

Watu wamenizunguka mimi na Jaffar Mponda Mtangazaji wa AZAM wanatusikiliza.

Wamepigwa na butwaa kusikia kuwa Nyerere na Mama Maria waliishi hapo.

Nyumba hiyo ninayoizungumza haipo hivi sasa badala yake kuna ghorofa.

Huwezi kuonyesha chuki dhidi ya Baba wa Taifa TV ikakurekodi na kurusha kipindi Watanzania na dunia wakione.

Kinachokuumiza wewe na mko wengi ni kwa nini historia ya Mwalimu Nyerere kote kazungukwa na Waislam?

Nataka nikufahamishe kitu.

Huko ulikotaja Ujiji, Buguruni na baadhi ya misikiti ya Dar es Salaam huko siko ninakoheshimika.

Mimi naheshimika kwenye Vyuo Vikuu vinavyosomesha African History, Marekani na Ulaya.



Northwestern University, Evanston Chicago


 
Kama kawaida yako ukikaa kidogo lazima utengeneze thread ya kumdogosha Mwl Nyerere. Unapata nini kwa kufStuxanya yote haya?
Stux...
Unasema nikikaa kidogo.
Hapana mimi maisha yangu yote ni kusoma na kuandika.

Sijapata kumdogosha Mwalimu Nyerere.

Ikiwa umesoma mahali nimemdogosha Mwalimu weka hayo niliyoandika hapa kama ushahidi.

Unaniuliza nini nilichopata?
Kwa kuandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika nimepokea nishani tano.

Hapa JF angalia mwenyewe hapo chini:


 
Sihutaji kuyajua hayo Mkuu wangu.Nachojua historia huwakumbuka wafalme tuu.Bahati mbaya sana mashujaa kama babu zako hawawezi kuongelewa kwa gravity kama ya nyerere hilo lazima ukubali.Nyerere ana mchango mkubwa sana kwa ustawi wa taifa hili kuliko wazee wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…