Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

Nlikuwa nasikiliza hotuba ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa Julai 22 mwaka 1967 Baada ya kuwapokea Vijana waliotembea kwa Miguu kutoka Moshi.

Alikuwa anaongelea kuhusu wanasiasa kununulika, Yaani hawa wananunulia na kusaliti vyama vyao au jamii iliyowachagua kwa vipande vya pesa akawaita ni Mwanasiasa Malaya ambao wao wanajali hela tu kama mercenary.

Nikaona inaendana na Wakati huu tulionao wa wanasiasa kuhama vyama ambapo inadaiwa baadhi yao wananunuliwa na wengine wanahama kwa utashi wao.

Hapa chini namnukuu alichokionge kuhusu wanasiasa wanaoambatana na mtu kisa tu wamepewa hela.

Anaanza kwa kusema, "Unakuta mtu anafuatana nalo hadi unajiuliza, huyu anafuatana nalo kwanini? Manake si heshima huyu kuandamana na yule, lakini unagundua anaandamahela. Hii ni tabia ya Kimalaya malaya. Na tunao wanasiasa wenye tabia ya Kimalaya malaya namna hii, wananunulika, heshima yao inauzwa, ina bei. Anakuuliza anaona... unasema fanya kitendo kadhaa ambacho ni kitendo cha aibu, lakini anakuuliza ngapi bwana?, Ukitoa bei ukimlipa basi, anakubali. Mwanasiasa ana tabia ya kimalaya malaya.

Mtu mwenye tabia ya kimalaya malaya ananunulika anafikiri kila mtu ananunulika. Kwahiyo anatoka anaenda kwa watu wengine, anadhani watu wengine wanaweza kufanya mambo ya aibu aibu ambayo hayana heshima..halafu anajuta, anajuta.

Kuna majeshi duniani humu yanaitwa Majeshi ya mercenary, yalikuwa hapo Congo, wengine ni vijana wadogo mnajua mercenary. mercenary ni mtu anafanya kazi kwa malipo, kwa pesa tu. Sababu yake kufanya kitendo kile ni pesa tu. Ukimuuliza kwanini unafanya hivi? anakujibu nalipwa.

Na hajali nani anayemlipa. INawezekana nchi mbili adui zinapigana hii na hii, anaweza kwenda kwa hii akasema mtanialipa? Kama hamuwezi kumlipa atawapigania hawa wengine kuua hawa. Yeye hana upande, anajua pesa tu. Maaskari hawa wanaitwa mercenary... anajua pesa tu, ni Malaya Malaya tu. Yupo tayari kuua au kuchukua hatari ya kuuawa sababu ya pesa tu. Askari wa kawaida yupo tayari kuua au kufa kwa sababu ya heshima ya nchi yake.

Lakini huyu yupo tayari kufa au kuuawa kwa sababu ya pesa tu. mercenary ana tabia ya Kimalaya Malaya tu.

Na tunao Wanasiasa mercenary, ni mercenary. Mtu yoyote anaweza kuwalipa tu, mtu yoyote, anakwambia mapesa haya hapa, utanifanyia kazi

Na tunayo mijitu humu, inafanya kazi si za wananchi hapa ni za watu wengine..hawa ni mercenary.. malaya Malaya tu. Halafu wapumbavu hawa, wanafikiri tunaunda jeshi la mercenary, wendawazimu hawa.

Sasa wamekiona cha mtema kuni. Na tumewatangazia, tumesema waende wapumbavu hawa kama hatujawatia ndani wote hawa. Tumepata aibu mara moja wanafikiri tunaweza kupata aibu mara mbili tena.

Jeshi letu ni jeshi la Wananchi wa Tanzania..sijui hawaelewi!!? Ni jeshi la Wananchi wa Tanzania Sio jeshi la Vibaraka Malaya Malaya eeh?.

Kwahiyo Vijana msijali, Msiwe na wasiwasi hata kidogo. Tunawajua, tutawasaka mmoja mmoja, mmoja mmoja.. Malaya watupu hawa, tutawasaka mmoja mmoja, na kila tutakapo wasaka tutawatangazieni kwamba Malaya mmoja tumeshamshika." Mwisho wa kumnukuu.

Je, unamtizamo gani juu ya haya aliyoyasema kutokana na hizi zama tulizo nazo. Je, wanaohama Wanaunga juhudi za rais au ni mercenary?


 
Nilisikilza ile hotuba juzi. Nikasema Shida Masamba ana dukuduku nini? Yaani inalenga wakati huu ambapo kuna dhana inayo sambaa kuwa baadhi ya wanasiasa wananunulika.

Nyerere anawaita Malaya si mara moja, neno malaya limetumika kama mara 20 kama sikosei tena kwa msisitizo mkubwa sana.

Kwa tafsiri yake mtu yeyote anayetanguliza pesa na si utaifa ni MALAYA, MALAYA, MALAYA.
 
IMG-20180927-WA0001.jpg
 
Nilisikilza ile hotuba juzi. Nikasema Shida Masamba ana dukuduku nini? Yaani inalenga wakati huu ambapo kuna dhana inayo sambaa kuwa baadhi ya wanasiasa wananunulika.

Nyerere anawaita Malaya si mara moja, neno malaya limetumika kama mara 20 kama sikosei tena kwa msisitizo mkubwa sana.

Kwa tafsiri yake mtu yeyote anayetanguliza pesa na si utaifa ni MALAYA, MALAYA, MALAYA.
Hahahahaha, daaah!
Unaambiwa kipindi hiki Mzee Nyerere alikuwa na the highest desire for belligerency.
He often made bellicose statements hadi unaweza kubaki mdomo wazi tu na kusema huyu ndiyo Raisi ?
Sasa na ukichangia na ujana ndiyo kabisaa, Too much Testosterone Burning ndiyo uwiii alikuwa mkaksi.
 
Mbali na umalaya wa wanasiasa anasisitiza ni jeshi la wananchi wa Tanzania, sasa hivi tuna kikundi cha jeshi limegeuka mercenary kama anavyosema Nyerere, nalo ni the so called jeshi la polisi.

Hili jeshi sasa hivi si la wananchi au kulinda raia na mali zao limegeuka kikundi cha kulinda maovu ya CCM, wako tayari kusindikiza masanduku ya wizi wa kura zilizoshapigwa tayari. They are non other than mercenary.
 
Kosa lake kubwa kabisa ni kutuachia katiba mbovu sana tena kwa maksudi kabisa!!
Kwa hilo ninauhakika anajilaumu sana huko aliko.
Katika hili alikosea sana, na hili lilitokana na kuwa na hofu ya mabadiliko ambayo wajamaa wengi wanayo.
Lakini mimi binafsi naamini kabisa huyu mzee alikuwa na nia njema sana na Tanzania yetu. Maana katika watu ambao wangeamua kutuuza wangefanikiwa basi huyu mzee angefanikiwa sana.
 
Nilisikilza ile hotuba juzi. Nikasema Shida Masamba ana dukuduku nini? Yaani inalenga wakati huu ambapo Luna dhana inayo sambaa kuwa baadhi ya wanasiasa wananunulika. Nyerere anawaita Malaya si mara moja, neno malaya limetumika kama mara 20 kama sikosei tena kwa msisitizo mkubwa sana. Kwa tafsiri yake mtu yeyote anayetanguliza pesa na si utaifa ni MALAYA, MALAYA, MALAYA.
Huyu BABA WA TAIFA MUNGU amrehemu huko aliko! Maana alikuwa anajua mengi YAFUATAYO! Japo viongozi wetu Wa sasa ukiongea kitu tofauti nao bc wewe wanasema UMETUMWA! MCHOCHEZI au C MZALENDO! MUNGU ibariki TANZANIA!
 
Mwalimu iliiona kesho jana.

Aliiona Tanzania chini ya udikteta kutokana na Katiba mbaya. Aliwaona wanasiasa malaya wakati wa kipindi cha udikteta.

Wakati wa udikteta, Mwalimu aliwaona vijana waoga badala ya vijana jeuri, vijana wanaohoji.

Wakati wa udikteta, alikiona chama legelege, chama ambacho kiongozi wake anakuwa na nguvu kuliko chama. Chama kinachoshindwa kutoa mwongozo kwa watawala.

Mwalimu tunajua wewe ni mwanadamu, na yawezekana kuna sehemu wakati wa kuishi kwako ulimkosea Mungu au wanafamu wenzako, lakini tunakuamini sana katika dhamira yako kwa watanzania, dhamira ambayo haikuwa na hila, dhamira ambayo haikuwa na unafiki.

Baba yetu wa Mbinguni, kwa kuangalia dhanira yake njema, umjalie taji katika ufalme wako, nao waishio leo kwa tamaa ya madaraka hata kufikia kuiba kura, wenye kuwadhalilisha wenzi wao kwa nia ya kujikweza, wenye kujitangaza sana kufanya mema kwaajili ya kuutaka utukufu, wenye kutaka kuua au wale wauao kwa sababu hawataki maovu yao kutajwa, basi uwapatilize wao na vizazi vyao hadi watakapokurudia na kutambua kuwa wewe ni Bwana wa Haki na una mamlaka juu ya wale wakutiiao na wale wenye kulitaja jina lako kwa hadaa.
 
Back
Top Bottom