ROMUARD KYARUZI
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 683
- 465
Mwalimu Nyerere asilaumiwe kutuachia katiba hii ya mlengo wa chama kimoja uelewa wa wananchi wetu ndio unachukuliwa kama advantage yakuendelea kukumbatia katiba hii yaku maintain status quo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Exactly. Leo mtu unaambiwa ni fisadi lisilofaa kwa lolote, kesho unaambiwa hilo ndilo the best presidential candidate. Mercenaries wanachoangalia ni pesa.Hiki ni kweli kabisa na ndicho kinachotokea.
P.
Mkuu naomba picha ikiwa attachment (graphic)
Mkuu, unaweza kutuma picha hii kama attachment? Natanguliza shukrani.
Achana na hiyoo sasa, kuna kitabu alikiandika kabla ya kufa unaambiwa lilikuwa ni bomu moja baya sana.Duh! Kumbe hata mwalimu alishawahi kuwaita malaya?
Huwa nawaita malaya all the time, nilidhani ni kosa kumbe ni kweli na wanastahili kabisa kuitwa hivyo.
Duh! Mkuu I wish ningepata hicho kitabu na hizo hotuba! Daah! Hicho kitabu ni Mkapa alipiga kiberiti?Achana na hiyoo sasa, kuna kitabu alikiandika kabla ya kufa unaambiwa lilikuwa ni bomu moja baya sana.
Yule Mmakonde aliagiza kipigwe moto chote na wala kisitoke nje. Kuna baadhi ya hotuba zake za ndani niliwahi kuzisoma kwa mtu niliogopa na kusema kama watanzania watayasikia haya basi wataumia sana!
Nani tena mwenye roho ngumu ya kufanya hivyo kama siyo yeye ?Duh! Mkuu I wish ningepata hicho kitabu na hizo hotuba! Daah! Hicho kitabu ni Mkapa alipiga kiberiti?
Asante sana. Ubarikiwe.Mkuu naomba picha ikiwa attachment (graphic)
Mkuu, unaweza kutuma picha hii kama attachment? Natanguliza shukrani.
Wakuu,
Nlikuwa nasikiliza hotuba ya baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa Julai 22 mwaka 1967 Baada ya kuwapokea Vijana waliotembea kwa Miguu kutoka Moshi.
Alikuwa anaongelea kuhusu wanasiasa kununulika, Yaani hawa wananunulia na kusaliti vyama vyao au jamii iliyowachagua kwa vipande vya pesa akawaita ni Mwanasiasa Malaya ambao wao wanajali hela tu kama mercenary.
Nikaona inaendana na Wakati huu tulionao wa wanasiasa kuhama vyama ambapo inadaiwa baadhi yao wananunuliwa na wengine wanahama kwa utashi wao.
Hapa chini namnukuu alichokionge kuhusu wanasiasa wanaoambatana na mtu kisa tu wamepewa hela.
Anaanza kwa kusema, "Unakuta mtu anafuatana nalo hadi unajiuliza, huyu anafuatana nalo kwanini? Manake si heshima huyu kuandamana na yule, lakini unagundua anaandamahela. Hii ni tabia ya Kimalaya malaya. Na tunao wanasiasa wenye tabia ya Kimalaya malaya namna hii, wananunulika, heshima yao inauzwa, ina bei. Anakuuliza anaona... unasema fanya kitendo kadhaa ambacho ni kitendo cha aibu, lakini anakuuliza ngapi bwana?, Ukitoa bei ukimlipa basi, anakubali. Mwanasiasa ana tabia ya kimalaya malaya.
Mtu mwenye tabia ya kimalaya malaya ananunulika anafikiri kila mtu ananunulika. Kwahiyo anatoka anaenda kwa watu wengine, anadhani watu wengine wanaweza kufanya mambo ya aibu aibu ambayo hayana heshima..halafu anajuta, anajuta.
Kuna majeshi duniani humu yanaitwa Majeshi ya mercenary, yalikuwa hapo Congo, wengine ni vijana wadogo mnajua mercenary. mercenary ni mtu anafanya kazi kwa malipo, kwa pesa tu. Sababu yake kufanya kitendo kile ni pesa tu. Ukimuuliza kwanini unafanya hivi? anakujibu nalipwa.
Na hajali nani anayemlipa. INawezekana nchi mbili adui zinapigana hii na hii, anaweza kwenda kwa hii akasema mtanialipa? Kama hamuwezi kumlipa atawapigania hawa wengine kuua hawa. Yeye hana upande, anajua pesa tu. Maaskari hawa wanaitwa mercenary... anajua pesa tu, ni Malaya Malaya tu. Yupo tayari kuua au kuchukua hatari ya kuuawa sababu ya pesa tu. Askari wa kawaida yupo tayari kuua au kufa kwa sababu ya heshima ya nchi yake.
Lakini huyu yupo tayari kufa au kuuawa kwa sababu ya pesa tu. mercenary ana tabia ya Kimalaya Malaya tu.
Na tunao Wanasiasa mercenary, ni mercenary. Mtu yoyote anaweza kuwalipa tu, mtu yoyote, anakwambia mapesa haya hapa, utanifanyia kazi
Na tunayo mijitu humu, inafanya kazi si za wananchi hapa ni za watu wengine..hawa ni mercenary.. malaya Malaya tu. Halafu wapumbavu hawa, wanafikiri tunaunda jeshi la mercenary, wendawazimu hawa.
Sasa wamekiona cha mtema kuni. Na tumewatangazia, tumesema waende wapumbavu hawa kama hatujawatia ndani wote hawa. Tumepata aibu mara moja wanafikiri tunaweza kupata aibu mara mbili tena.
Jeshi letu ni jeshi la Wananchi wa Tanzania..sijui hawaelewi!!? Ni jeshi la Wananchi wa Tanzania Sio jeshi la Vibaraka Malaya Malaya eeh?.
Kwahiyo Vijana msijali, Msiwe na wasiwasi hata kidogo. Tunawajua, tutawasaka mmoja mmoja, mmoja mmoja.. Malaya watupu hawa, tutawasaka mmoja mmoja, na kila tutakapo wasaka tutawatangazieni kwamba Malaya mmoja tumeshamshika." Mwisho wa kumnukuu.
Je, unamtizamo gani juu ya haya aliyoyasema kutokana na hizi zama tulizo nazo. Je, wanaohama Wanaunga juhudi za rais au ni mercenary?
Nilivyosikia audio nikadhani imebuniwa badae nikagundua kweli bhana..! Huyu mzee ni nabii aisei pia wakatolic wafanye tumpate mtakatifu wa kisiasa.Hiki ni kweli kabisa na ndicho kinachotokea.
P.
Kwa mara ya kwanza mwaka huu nime admire kizazi cha kwanza cha Uhuru kuwa kama ingempendeza muumba ningeishi kipindi kileHahahaha babuuuuu.
Apumzike kwa amani huko uliko.
Natamani ningekuwa na uwezo wa kumrudisha lakini sina!
Kuna mtu alisema ukiwa Kijana na usiwe revolutionary hiyo ni biological contradiction.Hahahahaha, daaah!
Unaambiwa kipindi hiki Mzee Nyerere alikuwa na the highest desire for belligerency.
He often made bellicose statements hadi unaweza kubaki mdomo wazi tu na kusema huyu ndiyo Raisi ?
Sasa na ukichangia na ujana ndiyo kabisaa, Too much Testosterone Burning ndiyo kabisaa alikuwa mkaksi.
Naomba title mkuu kama hutojali hata PMAchana na hiyoo sasa, kuna kitabu alikiandika kabla ya kufa unaambiwa lilikuwa ni bomu moja baya sana.
Yule Mmakonde aliagiza kipigwe moto chote na wala kisitoke nje. Tena kuna baadhi ya maneno yake aliyoyasema miaka ya 1990's nilyasoma kwa mtu niliogopa na kusema kama watanzania watayasikia haya kuhusu Serikali basi wataumia sana na mtu kama Raisi Mkapa hawawezi kumpenda kamwe.
Kuna dhana kuwa familia nzima haimkubali mmmakondeAchana na hiyoo sasa, kuna kitabu alikiandika kabla ya kufa unaambiwa lilikuwa ni bomu moja baya sana.
Yule Mmakonde aliagiza kipigwe moto chote na wala kisitoke nje. Tena kuna baadhi ya maneno yake aliyoyasema miaka ya 1990's nilyasoma kwa mtu niliogopa na kusema kama watanzania watayasikia haya kuhusu Serikali basi wataumia sana na mtu kama Raisi Mkapa hawawezi kumpenda kamwe.