Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Kosa lake kubwa kabisa ni kutuachia katiba mbovu sana tena kwa maksudi kabisa!!
Kwa hilo ninauhakika anajilaumu sana huko aliko.
Siyo kosa lake. Ni mabadiliko ya muda (time change and relevance of the constitution for the specific time). Hakuna nchi ambayo itamlaumu baba wa taifa kwa kuwaachia katiba mbovu. Katiba huwa inabadilishwa/ inatungwa mpya ama kuziba viraka. Katiba ya Tanzania ya 1977 haikutungwa iwe ya milele. Mwalimu asilaumiwe, aenziwe kwa kazi kubwa na ya mfano aliyofanya.
 
Hakika Mwl alikuwa anaona mbali sana. Mungu ampe pumziko la milele, Mzee wetu.
 
Mwalimu uliyasema haya mwaka 1967 yametimia maono yako haya hadi imekuwa aibu.Sijui ulikuwa unafunuliwa.
 
Siyo kosa lake. Ni mabadiliko ya muda (time change and relevance of the constitution for the specific time). Hakuna nchi ambayo itamlaumu baba wa taifa kwa kuwaachia katiba mbovu. Katiba huwa inabadilishwa/ inatungwa mpya ama kuziba viraka. Katiba ya Tanzania ya 1977 haikutungwa iwe ya milele. Mwalimu asilaumiwe, aenziwe kwa kazi kubwa na ya mfano aliyofanya.
Tumia akili vizuri, Nyerere alikiri hadharani kuwa katiba hii ni mbaya! Yaani alijua fika kuwa ni mbaya!

Muda usiwe kigezo cha kiegezo!
 
Umalaya malaya tu, masenari ni malaya malaya tu
 
Yaaaaaani hii speech kama imetoka jana kumbe ni ya kitambo,
 
actually ni malaya maana hakuna jina lingine la kuwaita
 
Nyerere bwana.

Alikuwa anauwezo mkubwa sana wakuishawishi hadhira na kumuelewa vyema.
Kutoa Jumbe zenye maono na tafakuri pana.

Pia wakati wa ujana wake hakupendwa kutishwa tishwa ulingoni mnaingia kisha mnawekeana Heshima.

Speech hii imenifurahisha hasa sauti yake pale anaposema "Tutawasaka mmoja Mmoja"
 
Back
Top Bottom