Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Tumia akili vizuri, Nyerere alikiri hadharani kuwa katiba hii ni mbaya! Yaani alijua fika kuwa ni mbaya!

Muda usiwe kigezo cha kiegezo!
Aliposema ni mbaya hakumaanisha kuwa yote ni mbaya. Ni baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo ilipaswa kufanyiwa amendments. Mfano kweye suala la katiba ya 1977 inaweza kumfanya raisi kuwa dictator, kwa sababu ana mamlaka makubwa sana kwa mujibu wa katiba.
 
Exactly. Leo mtu unaambiwa ni fisadi lisilofaa kwa lolote, kesho unaambiwa hilo ndilo the best presidential candidate. Mercenaries wanachoangalia ni pesa.
huwezi kuhama kwako ukahamia kwingine pasipo kuwa na chochote
 
Aliposema ni mbaya hakumaanisha kuwa yote ni mbaya. Ni baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo ilipaswa kufanyiwa amendments. Mfano kweye suala la katiba ya 1977 inaweza kumfanya raisi kuwa dictator, kwa sababu ana mamlaka makubwa sana kwa mujibu wa katiba.
Huo ndio ubaya wenyewe mkuu!
Alipaswa kurekebisha hapo kabla hajaondoka madarakani
 
Malcom Lumumba,
Nikipitia hotuba na maandishi kutoka kwa Nyerere, za mwanzo miaka ya 60-70, au hata kwenda nyuma zaidi, na za badaaye miaka ya 80 na baada ya kustaafu, naona zileza mwanzo zina discipline zaidi kuliko za mwisho.

Kwa sababu kadhaa nafikiri.

1. Mwanzo alikuwa hana uzoefu sana, na anataka kufanya mambo sawa sana.
2. Mwanzo alikuwa na matumaini zaidi ya kufanikiwa, alikuwa hajawa disappointed.
3. Mwanzo alikuwa kijana, ana wazee wengi anaowaheshimu na waliomsaidia sana kupigania uhuru walikuwa wanamtazama na anawatazama. Mwisho yeye ndiye alikuwa mzee wa kutazamwa na wenzake wengi walishatangulia mbele ya haki au aliweza kuwatuliza.
4. Mwanzo alikuwa na jukumu la kutengeneza mambo yeye, yakiharib ikailibidi aeleze kujitetea, si kwa ukali wa kukemea sana, mwisho mambo yaliendeshwa na wengine, alikuwa na uhuru sana wa kukemea serikaliambayo si yake.
5. Mwanzo alikuwa idealistic sana, alikuwa ana formulate njia ya nchi kuchukua, mwisho ingawa bado alikuwa idealistic, realism ilikuwa haikwepeki.

Ukimsikiliza Nyerere hotuba nyingi za miaka ya 1960's kwa mfano, alikuwa anaongea very formally, scripted, respectfully, with authority but justifying decisions etc. Baadaye huko miaka ya 80 na 90 akawa anafundisha, anakemea, anaonya,anadhihaki, anakebehi etc, mambo mengine hakufanya miaka ya mwanzo. Hapo kashakubalika "Baba wa taifa", neno lake kama la kijini-mtu!

Ukisema Nyerere alitoa bellicose statement mpaka ubaki mdomo wazi na kusema huyu rais, inabidi ujieleze statement kama ipi?

Maana unaweza kusema statement ya Nyererekuwaambia Wajerumani wang'oe nyaya za simu Tanga, kwa sababu za misimamo ya kisiasa ni bellicose, wakati unaweza kuambiwa statement hiyo ni stance ya sovereignty, na bellicose statements wametoa kina Kenyatta waliotukana matusi ya nguoni wakitoa hotuba nchi nzima inawasikiliza, au Magufuli anatoa statement inayoweza kuitwa bellicose anapotetea rushwa, anapohimiza watu wasijali uzazi wa mpango, anapo undermine international relations kwa kebehi za kijinga etc.

Sasa, inawezekana una ushahidi kuhusu habari ulizoandika.

Ila, ingekuwa vizuri zaidi uuweke hapa, tuone "bellicose statement" unayoisema ni ipi?

Maana isije kuw amtu anapinga unyanyaswaji wa raia wake,wewe ukasema bellicose statement.

Katika marais wa Tanzania, hakuna rais aliyekuwa anatoa hotuba zilizopangiliwa vizuri kimantiki na ki presentation kama Nyerere wa miaka ya 1960s na 1970s.

Nashangaa ninavyoona unasema alitoa bellicose statement, labda amesema kitu offhand kwenye parties za Ikulu mnajua sie hatujui, lakini kwenye record - as far as we restrict bellicose to bellicose, and not use the word in a hypernolic sense- I am struggling to find a case where Nyerere stated something bellicose.

If you want to be hyperbolic, even the declaration of war against Idi Amin can be said to be bellicose.
 
Mbali na umalaya wa wanasiasa anasisitiza ni jeshi la wananchi wa Tanzania, sasa hivi tuna kikundi cha jeshi limegeuka mercenary kama anavyosema Nyerere, nalo ni the so called jeshi la polisi.

Hili jeshi sasa hivi si la wananchi au kulinda raia na mali zao limegeuka kikundi cha kulinda maovu ya CCM, wako tayari kusindikiza masanduku ya wizi wa kura zilizoshapigwa tayari. They are non other than mercenary.
Ni Malaya [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yunawaomba ITV warushe hii kama hawatafungiwa leseni ya kurusha matangazo. Hata TBC wakirusha kesho yake Ryoba hana kazi na UD harudishwi.
 
Back
Top Bottom