Mkuu Mkuu
Nguruvi3, kuna msemo usemao numbers don't lie!. Wazanzibari wanapiga kura 5, kuchagua Sheha, mjumbe wa BLW, Mbunge wa Bunge la JMT, Rais wa Zanzibar na Rais wa JMT. Matokeo ya Rais wa JMT na mbunge wa Bunge la JMT yanatangazwa na NEC, matokeo ya sheha, Mwakilishi na rais wa Zanzibar ni ZEC, there are always discrepancies between idadi ya wapiga kura kati ya matoleo ya NEC na ya ZEC, matokeo ya NEC yanapaswa kuwa juu zaidi ya ZEC kwasababu kila Mtanzania lazima amchague rais wa JMT, hivyo Watanzania Bara walioko Zanzibar wanapiga kura moja tuu ya NEC wanamchagua rais tuu wa JMT.
Matokeo ya kweli ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, ni mimi niliyatangaza nikiwa Channel Ten, ZEC wakatoa matokeo yao 4 days later!.
Uchaguzi wa 2015 ZEC walifuta matokeo NEC hawakufuta the numbers didn't lie!, nikasema humu
Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
Hivyo sasa 2025 haki Zanzibar itatendeka!.
P
Mkuu nimekupata kama unaongelea suala hili. I'll be blunt on this! Wazanzibar wana matatizo ya ku focus kwa Tanganyika kama tatizo lao kubwa. Watatumia muda mwingi sana kutukana na kuwasumanga Watanganyika bila kujua tatizo lipo ndani yao.
Wazanzibar wana structure kama Baraza la Wawakilishi, Serikali na vyombo vingine. Regardless of their political affiliation wana uwezo wa kuondoa udhia tofauti na Tanganyika ambako hakuna serikali wala uwakilishi.
Kwanini wana focus kwa Tanganyika? Jibu ni rahisi, wanakwepa ukweli wa tofauti zao.
Ndiyo maana kuna Mapinduzi Daima na Mapinduzi Haramu
Mfano, suala la Katiba mpya ambalo kwao limekuwa la siku nyingi, kama CCM Kisiwandui na ACT Wazalendo wangeungana na kusema hawatashiriki mchakato wa viraka, Katiba ingepatikana
Kama Wabunge wao wangesema hawaji Dodoma hadi mchkato wa katiba uanze , Katiba ingepatikana
Nilisikia Wazanzibar wakisema kwenye space na club house kwamba Tanganyika ni watu milioni 60 kwahiyo wana nguvu zaidi. Nilijua ni ukosefu wa elimu tu unawasumbua.
Tanganyika haipo wazi na hivyo haina structure. JMT ni Tanganyika, haiwezi kujipinga kutokana na mkoroganyo
Zanzibar wapo 1.5M lakini wana nguvu sana katika Muungano. Kwa mfano, kwa uchache wao bado wana 2/3 ya maamuzi kwa baadhi ya Mambo Bungeni.
Wanaweza kutoshiriki Bunge la Dodoma kwa shinikizo na Bunge lisiendelee kwasababu bila wao halitimii kwa mantiki na akidi achilia mbali kikatiba
Wana SMZ inayoweza kusimamia mambo, wana Baraza la Wawakilishi.
Vyombo vyote vinaweza kufanya mambo kama tukio la Katiba ya 1984 toleo la 2010 ambalo limeifanya katiba hiyo kuwa KUU kuliko ya JMT na hakuna anayefanya jambo.
Kwanini wanashindwa kufanya mambo, ni kwasababu wamekuwa obsessed na Tanganyika, na viongozi wao hawasemi ukweli kwamba kuna 'nyufa' miongoni mwao.
Njia rahisi ni kuhamishia matatizo yao Tanganyika na kusahau kwamba wao wenyewe si wamoja, nitty gritty