Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Tena wakati ule wanataama hakukuwa na social media nk
Watu wametamba kivyaovyao

Ova
 
Ila kama media zingekuwa na hiyo domination hadi Leo, diamond angebaki ni yesterday story kama waliopita
Nadhani Kuna wasanii wawili tu naweza kusema walipitia mkono wa chuma wa clouds na bado wakatoboa 1. Jay Dee 2. Sugu. Ni hawa tu wawili japo kwa sasa wakati umeshawatupa mkono ila Diamond hapana mitandao ya kijamii imemsaidia.
 
Mitandao mkuu social media ilimuokoa
Yule ni special case Kwasababu mpaka anagombana na clouds tayari alikuwa na kundi kubwa la mashabiki wa kumsapoti, Tena alikuwa namba 1 kwa Tz.

ila mitandao ya kijamii kibongobongo Bado Haina power ya kumuweka msanii kwenye ramani kama mnavyodhani. Bado sapoti ya Redio inahitajika kwenye career ya msanii.

Kwa ulaya na marekani inawezekana, ila kibongobongo unaweza kunitajia msanii aliyechipukizia kwenye social medias na akamaintain usupastaa bila sapoti ya Redio?

Kuna watu kama Nacha ukiingia YouTube Wana views nyingi kuliko hata kina Young lunya,Rapcha,Nk.

Lakini kimtaan wanaoonekana ni wadogo kuliko hao Kwasababu hawana sapoti kubwa ya media.
 
Nadhani Kuna wasanii wawili tu naweza kusema walipitia mkono wa chuma wa clouds na bado wakatoboa 1. Jay Dee 2. Sugu. Ni hawa tu wawili japo kwa sasa wakati umeshawatupa mkono ila Diamond hapana mitandao ya kijamii imemsaidia.
Mondi kafungua Wasafi, ndo inayombeba yeye na genge lake lakina Zuchu na Mboso.
Bila Wasafi media WCB isingeweza kumaintain ukubwa huo hadi leo.
 
Katangaza kama hiyo 500k sio level yake ikimaanisha yoyote atakaemfuata, ajue kaisa hapigi show kwa hela hiyo. Kiufupi kaonesha thamani yake
Hili suala lina utata sana nimemsikia Chegge chigunda anasema nyuma ya nature kuna watu wapo kwa maslahi binafsi na wengine wanasema ile account ilicomment madai ya kudai kulipwa laki 5 inaongozwa na manager wake Rich one sijajua kipi ni sahihi hapo
 
Kama hayupo kwenye Trend walimfuata wa nini?

Hao wakongwe wana mashabiki wao watiifu wanaoenda kwenye show kukumbushia enzi zao ndiyo hao wanagundua kukosekana kwa Nature Mtwara.

Ruby alipokacha show ya fiesta kwa hoja hiihii ya maslahi basi Bwana Ruge alisimangwa kwa unyonyaji na roho mbaya!
 
Eyce
 
Kwahiyo aende mpaka Mtwara kwa laki 5?
Sasa kupata laki tano kwa dakika 20 na kukaa kurasini unavuta bangi bora nini?

Mnawapotosha sana hawa vijana, kila zama na kitabu chake, Bigirimana amecheza ligi kuu England lakini amekuja Yanga kuzidiwa mshahara na Aziz Ki na bado akaachwa.

Sasa Nature wa Wachuja Nafaka siyo huyu wa leo asijidanganye. Kwanza nyimbo zenyewe akiimba anasahau.

Hivi hii laki tano mnayoidharau wangapi IPO mfukoni mwenu SAA hizi?

By the way naamini hizi ni siasa chafu tu za kumchafuwa Dogo Diamond.

Nature si Mara ya kwanza kufanya huu upumbavu, alishafanya Uingereza hakutoka hotelini ilibidi inspector Haroun akaenda kukamuwa show peke yake.
 
Nadhani Kuna wasanii wawili tu naweza kusema walipitia mkono wa chuma wa clouds na bado wakatoboa 1. Jay Dee 2. Sugu. Ni hawa tu wawili japo kwa sasa wakati umeshawatupa mkono ila Diamond hapana mitandao ya kijamii imemsaidia.
Hao uliwataja walikuwa wanasapotiwa na media nyingine kubwa kama efm na IPP media ya mengi lakini diamond nyimbo zake zilikuwa hazipigwi kwenye media zote kubwa efm, IPP media na Clouds yenyewe. Nitajie msanii yoyote aliyetoboa kwa social media pekee?
 
Sioni nafasi ya kupeleka lawama kwa social media kwenye tatizo lililotengenezwa kupitia ujinga wa watu.

Zamani hakukuwa na sources za burudani

Katika tafsiri yako ya hizo sources za burudani una maanisha ni lazima hizo burudani ziwe za kijinga jinga?

Ukisema ili u trend ni lazima ufanye kitu cha hovyo basi ni kweli upo kwenye jamii ambayo imeshiba sana ujinga.
 
Kama wewe ulivyoyajua ya Daimond na Nature..
Hakuna sehemu yoyote Kati ya sugu au msanii amedeclare analipwa kiasi gani we umejuaje siku analipa vizuri hayo ya Diamond na nature ni baada ya nature kusema napo pia kuna utata wenzake kwenye kundi wamepingana na madai ya nature kuhusu hayo malipo
 
C'mon man kipindi ambacho Jaydee na Sugu wanapitia mkono wa chuma wa clouds kwa asilimia mia Majizo alikuwa bado DJ na pia EFM ilikuwa bado haijaanzishwa.

Halafu inaonaeka ulikuwa huijui nguvu ya mkono wa Ruge na Kusaga katika Bongo fleva enh!. Basi kaa na wadau wa Sanaa watakwambia.
 
Hakuna sehemu yoyote Kati ya sugu au msanii amedeclare analipwa kiasi gani we umejuaje siku analipa vizuri hayo ya Diamond na nature ni baada ya nature kusema napo pia kuna utata wenzake kwenye kundi wamepingana na madai ya nature kuhusu hayo malipo
Shida yako wewe unaleta u'team wa Dai na Nature....

Mambo ya nimejuaje hayo najua mimi....Na ndiyo maana nikaandika...ili mtu kama wewe usiyeelewa, uelewe,usipotaka unaacha

Narudi Bongo Flavour Honours ya Sugu wanalipwa vizuri....

Kumlipa mtu laki 5 kwa Show anazofanya Nature ni upuuzi kama upuuzi mwingine..Awalipe hao waimba Amapiano wenzake hiyo hela...
 
Bro Huo ujinga wa watu unadhani umezalishwaje au umetokeaje au umekujaje? Maana hakuna unga tuliolishwa au malaika aliyeshushwa kuleta ujinga Tanzania.

I'm sorry to disappoint you kwamba jamii ya kitanzania always imekuwa ya wajinga wengi kuliko werevu. Tena Bora sikuhizi idadi ya werevu kidogo imeongezeka kuliko zamani.

Tofauti tu ni kuwa, baada ya kuwa na hizi social medias, Power ya kutengeneza trend imeondolewa kwa wenye media au watu maarufu na imepelekwa kwa watu wote mtandaoni (ndo tunapata watubaki wanatrend kama mzee wa 900 itapendeza,Pierre liquid,Nabii Tito,Harmorapa,RC wa Tabora,Mwijaku, babalevo Nk.)

Hivo imekuwa Rahisi kwa wajinga kusapoti ujinga wao kuliko zamani. Na Kwasababu wajinga Tanzania ni wengi ndio maana ujinga unatrend.

Na wasanii Kwasababu wanataka kutrend wanafanya vitu ambavyo jamii inataka.

Social media zimetengeneza mazingira ya echo chambers kwa watumiaji kuflock kama nyumbu kwa vitu wanavyovipenda.
Sasa Kwasababu watumiaji tayari waanaenda kama nyumbu, ni ngumu kwa msanii kuwapa kitu tofauti na walichokizoea wakakifuata.
Tofauti na zamani ambapo msanii ndo alikuwa ana power ya kufanya chochote na kutengeneza trend na yeye ndo anaweza kudirect upepo uelekee wapi maana jamii ilikuwa Haina alternative.

Ndomaana sikuhizi hata diversity ya mziki inapungua kwa Kasi, wasanii wote wanakuwa na ladha ileile kama ikitrend amapiano Kila mtu anaimba amapiano, sio kama zamani Kila msanii alikuwa na style yake unique.
 
Pengine hiyo laki 5 kutokana na uchumi wako unaiona kubwa na inafaa kuwa bajeti ya siku nyingi.

Lakini jaribu kufikiria kwa namna nyingine.

Wasafi ni brand kubwa na iliyo take over industry ya mziki hapa Tanzania.

Ni brand ambayo ndio ina msanii maarufu na mwenye hela Tanzania na yeye mwenyewe amekuwa akijisifia.

Ni Festival ambayo host anamiliki vitega uchumi vikubwa vinavyomuingizia hela nyingi.

Na hata hii Festival haifanyi kama Foundation, haifanyi kama msaada kusema anatoa hela yake mfukoni kuwalipa wasanii waperfom bila mategemeo ya kupata chochote in return.

Hapana ni show ambayo ina wadhamini wakubwa kama Pepsi ambao hawa wanaweka mpunga mrefu.

Una amini Diamondi kumuita Nature kwenye show ilikuwa ni msaada au Diamondi mwenyewe aliona kitu special ambacho Nature angeweza ku offer kuifanya show yake iwe impressive?

Haikuwa ni msaada ilikuwa ni biashara na ndio maana wapo wasanii walioitamani hiyo nafasi hata kwa bila malipo.

So usimuone mjinga kuikataa hela hiyo, yes inaweza ikawa kubwa kwangu mimi na wewe ila yeye ikawa ni tofauti.
 
Kwani Bongo Fleva Honours ,Promo si wanafanya Wasafi tena free ndani ya ya mwezi mzima, kuanzia kwenye radio mpaka video.

Na unaweza ukakuta hilo wazo la Sugu ,radio nyingine walilikataa,ila Wasafi wakalibeba na kumbuka mtu airtime ni hela ambayo halipii na hata hiyo Gate collection Wasafi hawachukui.

Kuna wasanii hawa wa Zamani wanapiga show huko mahenge, hawapati hata hiyo laki tano na baada ya show wanakabiziwa viroba vya mchele.

Sometimes nae Mondi ache shobo ,adeal na watu wa kwenye circle yake kama kubeba na kusaidia kisha wasaidia wengi,awaache wapambane wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…