Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Kizazi cha watoto wa mwaka 2000 wengi hawamtambui na ndo wahudhuriaji wa matamasha hayo!!

Muda umemuacha soko pia halimuhitaji asijilinganishe na hawa vijana wa sasa wanaoimba "bia tamu"😂
Mbona Lady jay dee anafanya matamasha yake very classic na anapata pesa kama kawaida!!!...

Kitu msichofahamu, audience ya nature na legends wengine ni kuanzia miaka 25 kwenda juu, hawa walianza kusikiliza muziki wakati hivyo vichwa vilikuwa katika peak. Uzuri zaidi hiyo age group ndo ina nguvu ya kimaokoto kuliko hao wa 2000.

Kwa hiyo mkuu usifikiri nature ni wa hadhi ya chini kiasi cha kukubali hiyo pesa, hata kama wakongwe hawaezi lipwa sawa na, wa sasa ila wasidharaulike.
 
Tuwe wakweli hivi Juma nature sasa hivi atangaze show kiingilio 2000 kwa kichwa wangapi humu wataenda?
Ukweli ni kwamba binafsi hata Diamond, Ali Kiba, mjomba nchumali, sijui kina Marioo wapige show bure hapo kibarazani kwangu siwezi kwenda.. kila mtu na akipendacho.

Hao wasafi kumfata nature kuna jambo wameliona na nature kakataa sababu anajua thamani yake.
 
Huenda akastahili zaidi ya hiyo, ila wasafi nao ni wafanyabiashara, hivi kweli watoe mamilioni kwa juma nature? Mtu wimbo wake wa mwisho hata hatujui ulitoka lini, kwanza kibiashara kabisa asingefikiriwa kabisa
Wasafi wamemfata wakaona ana hadhi ya laki 5, ye nature kaona sio thamani yake hakuna kesi hapo.
 
Hizi nchi maskini ni tabu kwa kwenda mbele, najaribu tu kuwaza catalogue ya Sir Nature, kuanzia nyimbo zake, nyimbo za kundi mpka zile za kushirikishwa!

Kwa nchi kama US ilibidi awe anakula tu maokoto ya digital platforms na angekuwa tajiri bila hata hizo shows.
Sasa kwa mfano ukienda spotify nyimbo zake hata 10 hazifiki, na sina hakika kama acc ni yake kweli.

Hapa kwetu hata Museum tu ya Bongo fleva ilikotoka hakuna, hizi nyimbo unakuta hata wasanii wenyewe hawana, kwahiyo dharau za kulipana laki 5 lazima ziwepo.

Ifike muda tuupe thamani muziki wetu, Sugu ameonesha njia na Bongo Flava Honors japo katuwekea stage ya hovyo sana hata stage ya bar ina afadhali.

Hata tukiamua kutenga mji mmoja uwe ndo kitovu cha Bongo Fleva inawezekana, Leo hii ukienda Nashville, Tennessee kuna kumbukumbu zote za muziki wa country, producers, song writers na record label za Country zipo Nashville na wameupa heshima kubwa muziki wao.
 
Huenda akastahili zaidi ya hiyo, ila wasafi nao ni wafanyabiashara, hivi kweli watoe mamilioni kwa juma nature? Mtu wimbo wake wa mwisho hata hatujui ulitoka lini, kwanza kibiashara kabisa asingefikiriwa kabisa
Tatizo unaona kitendo cha wasafi kumualika Nature ni kama cha msaada.

Kwenye show hakunaga hizi story za wimbo wako wa mwisho.

Angalia juzi hapo Best Naso aliwafunika mainstream wote kwenye show. Na hadi Roma mwenyewe ali appreciate.

Wasanii wa zamani ndio wanaoweza kuleta vibe zaidi kwenye show kuliko hao mainstream artists.

Kwasababu miziki ya zamani kwanza huamsha kumbukumbu na hisia ya kipekee kwa kukumbuka nyakati za nyuma kipindi huo wimbo una hit.

Kwa hiyo kama unafikiri Nature alipaswa kukubali malipo ambayo kwake aliona hayana maslahi kwa kigezo cha kutokuwa na ngoma mpya ambayo ipo kwenye chart basi utakuwa unakosea.
 
Back
Top Bottom