Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

[emoji457]
 
Cha ajabu wewe hata Nature akitangaza kiingilio buku hutothubutu kuhudhuria hiyo show, nature alikuwa zamani sasa hivi Hana jipya kwanza hao wasanii wenyewe unafikir kipi Cha ajabu ambacho Huwa wanafanya stejini zaidi ya kugandamizia kwenye playback na Kila muda kuwaambia mashabiki mikono juu!! Sema yeiaaaa, sema yoyoyo.
 
Hata kama hayuko kwenye trend, mtu hawezi kutoka Dsm au popote hadi Mtwara.
Apande jukwaani. Halafu malipo laki 5.
Bila shaka wanagharamiwa na waandaaji wa Wasafi festival,hiyo ni hela ya jukwaani tu. Aisee mi namuonea huruma, upepo umebadilika, ajitokeze kwenye platforms mbalimbmbalimbali kama hizo, aonekane..
 
Kiingilio kikiwa buku siwezi kwenda kweli sababu najua itajua ni local show, ila akiweka kuanzia elfu 50 naenda tena na familia yangu,

Angekua hana jipya Wasafi wasingemualika.
 
Mimi sio mwendaji wa hayo matamasha ila Nature Ana vibe lake takatifu ndyo maana wasafi wakamuita
Tatizo wengi humu wakati nature anatrend wao ndyo wanazaliwa...ndyo maana wanaona laki 5 kubwa kwa nature....Juma apewe heshima yake jamani...show yake huwezi fananisha na kina Chino
 
Thank you Missy,
Kama hawajaelewa na hapo basi tuwaache tu na kina Chino wao, lol
 
Tuwe wakweli hivi Juma nature sasa hivi atangaze show kiingilio 2000 kwa kichwa wangapi humu wataenda?
Kama inapigwa PROMO ya maana halafu amuweke jamaa INSPECTOR HAROUN
watumbiize lile dude (haya sasa nini ugomvi huo mtoto wa MZEE WA BUSARA kila siku anakula kwetu
Tukianza kula wa kwanza kudokoa nyama
Ukimkataza mamaaa anaenda kusema
Kivumbi sasa USIKU) na KUNDIZIMA la TMK wawepo mm hata KIINGILIO ELF 50 nalipa
Mana ninauhakika hao jamaa hautakaa kwenye kitako itakuwa kamua tu BANDIKA bandua na VIBAO vyao vikali

Yaaaan ile STEVE B NATURE VENTURE mafundi wa kukesha #@%%kwinyokwinyo%&*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…