Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Kiingilio kikiwa buku siwezi kwenda kweli sababu najua itajua ni local show, ila akiweka kuanzia elfu 50 naenda tena na familia yangu,

Angekua hana jipya Wasafi wasingemualika.
Show yake ya Heshima kwa Legends wa Bongo Fleva inayosimamiwa na Sugu alijaza fresh tu na maokoto ni 20,000/- kwa kichwa sasa unampaje 500,000/- yeye akiingia chaka moja huko bush anaibuka na maokoto kuzidi hio 500,000/- tena kwa zile zile album zake, ikipigwa 'Mtoto Idd' watu wote wanasimama 😆
 
Washamba wengi humu hawamjui Nature, wala sio utoto ni vile kipindi hicho wao walikua sigimbi wanalima magimbi,

Vyuo ndio vimewaleta wengi jijini, basi wanajikuuuuta na wao wamo, ndio utaona michango mingi ya walugaluga wanaona kiroboto anastahili hiyo laki 5.
Umesema ukweli dada,laki Tano Ndo alikua analipwa miaka ya elf 2 Leo Tena wampe laki Tano

Hawamjui nature Hawa wanaropokwa tu
 
Wasafi wamemvalue kwa hicho kiasi kulingana na soko na yeye Ndio ana choice na yeye ameona sio kiasi kizuri sijaona shida ni nini?
Shida yeye ni legend na ana wapenzi wengi wa nyimbo zake kwa hio ni kivutio cha show mwingine anaenda kwenye show kumuona Nature tu akiperfom alafu basi akishuka na yeye anaondoka au hujui?
 
Na huyo ni kwasababu tu ya aibu ndio wameamua kumtunuku tano.

Wale kina boshoo wanaosaka kujulikana sidhani kama hata laki wanapewa.

Wengine wakilipwa msosi tu na kupandishwa kwenye flight basi hiyo inatosha.

Kwasababu malengo ya wasanii wengi chipukizi ni kuanza kutengeneza fanbase. Sasa wanaona kupitia hii festival na ukubwa wa Diamondi basi anaweza kupata fans wengi wakumsapoti.

Ni ngumu sana kuwaona wakina P Mawenge, Nikki Mbishi kwenye hii festival kwasababu wako smart sana kwenye ishu ya malipo.

Hawawezi kuacha familia zao nyumbani wao wakaruke ruke mikoani halafu warudi home bila hela au kufanya show kwa dau la kitonga.
Fact
 
Cha ajabu ww hata Nature akitangaza kiingilio buku hutothubutu kuudhuria hiyo show, nature alikuwa zamani sasa hivi Hana jipya kwanza hao wasanii wenyewe unafikir kipi Cha ajabu ambacho Huwa wanafanya stejini zaidi ya kugandamizia kwenye playback na Kila muda kuwaambia mashabiki mikono juu!! Sema yeiaaaa, sema yoyoyo.
Wenye jipya ndio wamekubali malipo ya kausha damu ambayo Nature kayaona hayana maslahi kwake.

Wakina Bilnas ambao wewe unaweza kuwaona wapo kwenye peak ndio wamekubali malipo hayo.

Unaweza ukawa una nyimbo zilizo trend lakini zisikusaidie kuamsha kwenye show.

Mfano mzuri tu Wakazi sio msanii ambaye nyimbo zake zinaingia kwenye trend lakini kwenye show ya live band sijamuona msanii wa Hip Hop Afrika mashariki wakumfikia.

Kuburudisha kwenye show hakutegmeani na jinsi nyimbo zako zipo kwenye currently peak.

Nimeweka mfano wa Best Nasso aliyefanya show kwenye jukwaa na wasanii wengi ambao wapo kwenye mainstream.

Lakini ilipofika muda wake wakupanda stejini aliwafunika wote tena kwa ngoma zile zile za zamani.
 
Back
Top Bottom