Juma Nature: Nina miaka 37 sijafika hata 40

Juma Nature: Nina miaka 37 sijafika hata 40

Ninavyomfahamu JUma Nature ni kwamba alizaliwa mwaka 1980 na kwa sasa ana 43, sababu mwenzake Mulla na mmoja wao kwenye kundi lao la muziki la TMK nimemsahau jina, niliwapita madarasa mawili pale Kibasila nilikuwa naishi nao jirani kota za Bora pale Keko
Nature awezi kuwa wa 80 nature ni wa 70s niko tayari kugharamia vipimo vya umri na mifupa kama yuko tayari
 
Nkiwa form five jumanature na kundi lake walipita shuleni kweli na tukawapa ugali wetu wakala tena kwa upendo!

Na kipindi hicho jumanature alikuwa mkubwa katuzidi form five yote tena zaidi ya miaka 12 ukimuangalia tuu…

Sasa leo hii ninaposikia jumanature ana miaka 37 kweli ni habari ya mshituko kwangu pengine wazazi wangu walinidanganya kuhusu umri wangu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkongwe wa muziki wa bongofleva, Juma Kassim Kiroboto maarufu kama Juma Nature anasema watu waache kumzushia kama amezeeka wakati ndio kwanza ana miaka 37 hajafika hata miaka 40. Yeye bado kijana mdogo wasimuite mzee.

My take:
Nature ameingia kwenye mkumbo wa dada yetu Wema Sepetu, ambae hajawahi kuvuka miaka 28 tangu mimi nikiwa mdogo. Kwanini mastaa wanapenda kurudisha miaka nyuma?

Kwa mujibu wa Mtandao
Screenshot_20230614_100352_Google.jpg
 
Mkongwe wa muziki wa bongofleva, Juma Kassim Kiroboto maarufu kama Juma Nature anasema watu waache kumzushia kama amezeeka wakati ndio kwanza ana miaka 37 hajafika hata miaka 40. Yeye bado kijana mdogo wasimuite mzee.

My take:
Nature ameingia kwenye mkumbo wa dada yetu Wema Sepetu, ambae hajawahi kuvuka miaka 28 tangu mimi nikiwa mdogo. Kwanini mastaa wanapenda kurudisha miaka nyuma?

niishie tu kusema pombe ngumu Sigara, Bangi na maisha Bwete vinazeesha!!
 
Back
Top Bottom