Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Juma Njemba: Sangoma aliyeishi maisha ya peponi akiwa duniani

Mwaka 2001 huo nikiwa naishi kibondo,kuna siku nikatumwa kwenda kasulu kutoa photocopy na kuprint document za ofisini.nilikuwa toyota landcruza GX za UN kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa bado na wakimbizi kwenye makambi kama nyarugusu.
Asubuhi mapema nikaondoka nikiwa na jamaa mwingine.
Kufika kasulu nikanunua na mananasi ya kutosha waliopo kipande hio watajua.mwidiweee salam niliipata sana wakati narudi.
Kufika njiani nikamkuta jamaa flani huwa namuona sana pale mjini kibondo akiwa peke yake porini!nikasimama ili nimpe lift akagoma.
Anyway mi nakachapa mwendo barabara ilikuwa rafu rodi lakini kwa GX nilitembea hadi spidi 140.
Kufika kibondo namkuta jamaa kafika kitambo anakunywa kahawa anacheza draft.sikuamini ilibidi nimtafute anieleze alifikaje kabla ya gari na hakukuwa na gari lilinipita njia??!!mambo aliyoniambia hadi siyaamini
Tililika mkuu
 
Njembaa!hakuwa wa spotispoti ubaya tu ni vitu ambavyo hatuwezi kuleta ushahid wakushikika au wakuonekana ila mh!Hv ujiji yote ile hyo elim inayotetewa alikuwa nayo peke yake?aliipata wap?kwa nn aliogopwa?something was not right 100%
 
MMH
Kwenye issue ya koti ofisini kuna alilosema la kweli na lipo hakusema kweli nenda kasome komenti yangu vema.

Kweli ni kukamatwa kwa mwanae kwa kutuhumiwa kuzurura

Isiyo kweli ni kutundikwa kwa koti
Zaidi issue hiyo ya koti Ujiji ni maarufu sana kwa wazee Zaidi ya mmoja kiasi watu walishaamini kuwa hizo ni ngano zinazohusishwa na watu Fulani kuwakuza au kuwapa utajo kuwa ni wenye nguvu za miujiza.
UNAJARIBU KUFICHA UKWELI LAKINI BABA YAKO NJEMBA ALIKUWA MCHAWI MGANGA NA ALIUA WATU. AWE AMEUA KWA MATAKWA YA MTEJA AU KAMA SEHEMU YA MATIBABU LAKINI NI MUUAJI TU.
HAKUNA MGANGA WA JADI ASIYEKUWA MCHAWI, UNAFUNZWA UCHAWI ALAFU NDO UGANGA.
LAKINI KUKUBALI KWAMBA U MCHAWI HUWEZI MAANA NI AIBU
 
Sio muhimu kujua jina, ila kama we ni mtu wake wa karibu lazima unaelewa kuwa alikufa kwa PIGO, pigo kuu zaidi ya uchawi, hakuna mchawi ambaye angeweza kumgusa, hapo ndipo alipotokea Mungu aliyempiga mapigo kumi ya Kimisri ghafra, Mungu wa Israel, ni baada ya Mtumishi kupunga mikono juu...
hata sheikh Yahya alifyekwa baada ya wakristo kumlilia MUNGU, Lakini haya ni mambo ya rohoni
 
mimi niluwahi kwenda kwa huyo mzee lakini niliogopa kumalizia zindiko la milango saba ya ziwa tanganyika, nikaondoka kwa kutoroka tukiwa mlango wa tatu , nadhani umenikumbusha mbali mno wala hujakosea kitu.
Waweza toa angalau mwanga kidogo namna yalivyofanyika hayo mazindiko hadi milango mitatu ikafikiwa??
 
Nakumbuka visa viwil vya huyu bwana wakati nipo kigoma ni pale alipomtuma mwanake akanunue migebuka soko la buzeba zeba then askari wakamkamata kwa uzururaji,mzee baada ya kuskia akamfata RPC,nakumbuka alikwa ni mgeni but mjeda kufika tu ofisini akaliweka koti lake kwenye ukuta bila kuwepo na msumari then akamwambia nmekuletea kapu langu hil ukaninunulie mboga maana nnayemtuma mmemkamata,ndani ya 20minutes dogo aliachiwa na kupelekwa na escort ya polisi sokoni hadi kwao

Mkuu samahani.
Tukio hilo limetokea mkoani kigoma peke ake??

Kuna masimulizi mengine yanaonyesha tukio kama hilo lilitokea kati ya RPC wa Mbeya na Wazee wa Mbeya
 
Ila ukisema ufatilie majina ya hao watu wa Kigoma Mjini utakuja kugundua wengi ni Wacongomani kiasili mfano Lwamba, Yemba, Anzuruni, Nondo, Kabwe hayo ni majina ya Kikongomani typical tena ndugu zao wengi wapo Nyarugusu Refugee Camp,na wengine walikuwepo Lugufu Refugee Camp..
 
Hivi bado kuna magwiji kama zamani zama hizi kufikia nguvu za bibi fisi wa Igogo bugando Mwanza,au Juma njemba.
 
mi kazi yangu kutoa ushahidi niliouona kikweli bwana likud yuko sahihi kuwa hakuna mwenye uwezo ule tena na hilo nimesikia kwa nduguze wenyewe narudia niliishi kigoma 2 years ,ila wajukuu zake pia waganga ila tukirank top 20 ya waganga noma kigoma hao wajukuu hamna kitu hii aliniambia rafiki yangu marehemu kassim said tajiri wa mabot miaka hiyo so msimfate yoyote inbox hata mm mtaliwa sana
Huenda ukafuatwa utaje hiyo top 20 rank.
Jiandae mkuu
 
Sasa kwanini unadhani unafaa tukuamini?
1.Umefail kwny tarehe yake ya kufa na kuzikwa
2. Ulichioweza ni kuleta majina na idadi ya familia ya huyo Juma, ambayo ni ngumu kwa yyte humu ku verify kama usemacho ni kweli.
3. Umejikita only kuongea positive side bila ya angalau kijihusisha na anacho kiongea mleta mada na member wengine humu waliofika kilingeni kwake na kukubaliana na Likud
4. unakanusha tu anachosema Likud basi, yaani kama kuna kitu au jambo hutaki lisimwe

Swali la 1. Hata mie nasubiri majib yake baba faiza.

2. Hili swala lingemalizika kama wale wanaomjua wangeleta pia list ya majina ya wake zake pamoja na watoto.
Likud kasema idadi ya wake walikuwa 200 lakini sijaona sehemu angalau ametaja wake zake 10 tuu kwa majina yao (nilitegemea ningeona listi sababu hili swala alilifanyia utafiti zaidi)

3. Watu wanaomjua humu na wanaosema wameenda kwenye kilinge chake kusaka tiba pia wameshindwa kusema mazingira ya kilinge kama alivyohitaji baba faiza(AbuFizzer)

4. Nafikiri Likud akimalizia sehemu iliyobaki tutapata mwanga
 
Hata mwambao Ziwa upande wa Rukwa nako kuna mafundi wengi balaa ambao wengi ni hybrid ya kalemii(DRC) na ufipa,ukiipataa hii hata ni hatari

Ile story ya kuiba mwenge wa UHURU nayo ushawahi isikia mkuu, Na kuna ile ya mwewe kubeba ng'ombe japo siiamini sana,
Fanya dokezo la kuibiwa mwenge wa uhuru kiongozi
 
Back
Top Bottom