June 30, 1993 alifariki Gavana Rutihinda na kuzikwa Buguruni Malapa. June 15, 2024 anafariki Balozi Ruhinda na kuzikwa Kinondoni

Hili hua la msingi sana tatizo wengi watoka vijijini hujifanya kwao mjini
Kuna Vijiji vya kujenga.Kuna maeneo ukijenga unajiwaisha mapema.Hawataki Kuna hata bati.Usione watu hawataki kujenga kwao ukawaona mafala.Kijana wangu Baada ya kupata kazi yake ya ualimu akapangiwa Mwanza,mshahara wake wa kwanza akaja kurekebisha kijumba Cha wazazi wake kukandika Tena na udongo kupiga ripu,akayatoa makuti na kupiga bati.kiasi kilichobaki akaoa na kuanza safari ya kurudi kazini,kufika Tabora kipere chini ya pua kimeiva ghafra tu mkewe si kamtumbua wakiwa kwenye basi.Kichwa kichwa ikabidi washuke njiani kwenda Hospital akutoboa kafia Tabora njiani.Msimba unarudi Pwani Kwa Mazishi kumbe Shangazi ndio Sterling.
 
Mwanangu maiti inasikia aibu! Unasutwa msibani mpaka unahisi joto kwenye jeneza! Jitahidi ujenge kwenu mkuu!
 
Haya mambo yamekwamisha sana watu aisee! Miaka ile Usukumani ukiona mtumishi amejenga kwao basi ujue nyumbani kwao nao wako vizuri kwenye ndumba! Ilikuwa shida sana, tena hawa hawa shangazi zetu ndio walikuwa wanatushughulikia! Mwanga tumeanza kuuona miaka ya 2000, sasa hivi mambo mazuri vimebaki vijiji vichache sana!
 
Huko unapooaota kwenu unamjengea nani? Mnaona ni busara mtu anayetafuta hela yake kwa jasho machozi na damu atumie hela yake kwenda kujenga sehemu ambayo hatoishi?
Narudia kusema hili...angalia mifano mbali mbali ya viongozi wengi na watu mashuhuri mbali mbali wakifarik Wana prefer kuzikwa kwenye ardhi ya nyumbani kwao..

NB.
Humu Jf tunapishana umri,dini,mitazamo,kipato, upeo,maono, malezi, experience N.K

Wengine humu unakuta mama alikua changudoa au barmaid au housegirl akapigwa PAIPU Bahati mbaya ikatunga mimba na ikakataliwa na akazaliwa mtoto so unakuta mtoto anae zaliwaa Hana IDENTITY & vise versa is true..
 
Hakika tunatofautiana UMRI na MITAZAMO.
Sasa inakueaje unataka wengine woye waishi kwa preference za wengine?
Mwenye mama Changudoa au Barmaid unadhani hana Identity au unadhani maisha yake ni pungufu kuliko wewe? Au unadhani wewe una ukamilifu kuliko wenyewe?
Hujui inawezekana unayemuita Babu kumbe ndiye baba yako mzazi? Au inawezekana kweli wewe ni wa Kishua na wazazi wako wanaishi pamoja kwenye ndoa lakini yule babu wa kazi au wa shamba, au mlinzi, au yeyote hapo mtaani ndiye baba yako.

Unadhani wewe unaifahamu vizuri historia ya kupatikana kwako? Au unadhani unafahamu baba yako alimpata vipi mama yako?
Hakika humu tunatofautiana Umri, Dini na Mitazamo….pia uzoefu wa maisha.
 
Kigogo Kuna mtaa unaitwa Rutihinda,Kuna uhusiano wowote wa eneo Hilo na jina la Gavana??
Sio mtaa tu na shule ya msingi Gilman Rutihinda,vyote vipo kigogo karibu na kigogo sambusa,ndio vilipewa jina baada ya kifo cha huyo gavaba wa BOT
 
Umeandika Mambo mengi japo mengi ni ujinga.
Kwanza mi binafs cwalaumi wasiojenga kwao coz kuna sababu nyingi nyingine kulogana na ushenz kama huo. Lakini kusema kujenga home ni kupoteza inategemea na huko kwenu ni wapi. Mi kijijin nimejenga na nimepangisha tena wanaingia na kutoka maana nimeiweka Airbnb. Ni Kilimanjaro. Ishu ni kuwa unaweza kujenga wewe ukawasaidia wengine uthubuti wa kujenga na wao. Kwamba inakulipa nini inaweza isikulipe lakini ukaisaidia jamii yako kubadilika maana kuna watu wanajifunza kwa kuona zaid. Huwez kuwa mbinafs kias hicho kwa kujifikiria wewe tu kwamba utapata nini sio kila kitu utapata wewe vingine unaangalia namna ya kusaidia jamii kwa mapana. So ni muhim sana kujenga kwenu kwa mustakabali wa jamii yenu yenyewe.
 
Kweli wewe ulimfahamu.

Unajua kuna kitu waZungu na watu wenye uwezo wao, wanakiita retirement homes. Yaani unakuwa na nyumba mji mwingine tofauti kabisa…siku ukistaafu unaelekea huko. Na hii inakuwa influenced na Hali ya hewa, huduma za jamii nk.

Kama pesa au kipato chako ni cha kuungaunga, basi wewe pambana ustaafie hapo hapo mwanagati au Mbagala, ulipoweka nyumba ya ujana wako.

Ila kama uko vizuri kiuchumi, mda ukifika jitahidi uondoke mjini. Maana umri ukienda hukawii ukaona vijana wote hawana adabu…just kwa sababu umekutana na kijana hajakusalimia. Au mmekutana benki hajakupisha kwenye foleni.
 
Duh, mkuu hii lugha yako hii haina staha kwa kweli, sijui wanajisikiaje watoto wa single mazeri?
 
Ukistaafu usikae zaidi ya 100 km kutoka muhimbili,maana kunavijiji vinginemafua tu unakufa,zahanati haina hata panadol,huo ni mtazamo wangu tu,mtanizika babati ila nitafia muhimbili
 
Maelezo meengi..ila umepuyanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…