Juventus Special Thread

Juventus Special Thread

Mpira wa Italia umebadilika sana.

Jamaa walishaacha Catenachio kabisa. Jana nimefurahi kwamba nimeona mechi ambayo at least mtu unaweza kukaa chini ukatazama.

Milan walitupa wakati mgumu kwa pasi fupi fupi na kutukaba kwenye half yetu,sikutegemea Milan wacheze vizuri vile,ndio maana Ancelloti na warembo wake walikaa 4! Bahati mbaya yao kwa jana tu,ni kwamba Juve wako kwenye dunia yao misimu hii,ni wakali sana,kama jana walikuwa wakikamata mpira ni hekaheka kwa akina Alex na wenzie.

Kombinenga ya Tevez,Morata,Pogba,Marchisio,Vidal,Padoin na Evra ilikuwa kama circuit ya elektroniki vile,ukigusisha umeme kwenye njia moja,basi circuit nzima imejaa umeme!walikuwa fast paced na wanaelewana sana,yaani wakivuka half tu,goli la Milan linawaka moto!

Chiellini was on form pia.Ilikuwa mechi nzuri,kasoro Pirlo hakuniridhisha sana.Pia Pazzini bado mzuri,na Cerci na Honda wako njema sana.
 
What are they smoking in Milan? Eti juve2012, Gang Chomba Ziroseventytwo, mmeziona hizi ngonjera za 'Anko Festa'?

Juventus and Milan in bizarre row over television graphics
AC Milan have accused Juventus of manipulating television graphics to show that Carlos Tevez was onside when he scored the first goal for the Turin club in their 3-1 home win on Saturday.

In a bizarre row between the old Serie A rivals, Juventus retorted that Milan's chief executive Adriano Galliani was creating a "farcical" controversy to mask his team's defeat.

Tevez scored Juve's first goal when he was sent clear from near the halfway line and slotted the ball past Diego Lopez with the Milan defence unable to catch him.

Television replays appeared to show that Tevez was just in line with the last defender, however Milan then said the computer-generated line drawn across the field was slightly skewed and not parallel to the halfway line.

"According to the television pictures produced by Juventus, the two lines are parallel. For us, no," tweeted Milan.

Galliani was quoted by Italian media as saying: "Unlike the other Serie A teams, the production of the television pictures of the Juventus matches are managed by the club itself."

But champions Juventus replied in a statement that they had nothing to do with the graphics.

"Mr Galliani has returned to two of his favourites passions, television and geometry," said the club, before launching into a complicated explanation of who is responsible for the pictures at Serie A matches.

"Galliani is throwing food to the media to fuel a spurious and farcical controversy because he is trying desperately to hide from the Milan supporters the very clear result on the pitch in yesterday's game. Three to one."

It added that Galliani was at the Serie A assembly which unanimously agreed the rules for the broadcasting of matches.

"He seems to ignore that all the rules and regulations about use of technology and adaptations passed under his eyes, or were even decided by him," said the statement.
 
Last edited by a moderator:
Very low from that Mzee.

Hizi propaganda sasa imekuwa ni excuse kwa kila afungwaye na Juve! Labda atueleze kama hizo graphic manipulation ndio zimesababisha wao kufunga goli moja kwa dk zote 90 na Juve kupiga 3?au Juve pia wanahusika kwenye mpangilio wa jedwali hadi ionekane Juve ya kwanza na Milan ya tisa?

very poor from this guy!mwaka 2006 waliishusha Juve daraja kwa kudai inashinda kwa wizi,lakini mwaka huo huo kikosi cha Italia kilichosheheni wachezaji wale wale wa Juve wanaotuhumiwa kubebwa kwenye ligi,tena wakiwa na kocha toka Juve kilitwaa world cup!Wakainyang'anya taji la serie a la 2002 kwa kudai kupanga matokeo,lakini kikosi kile kile msimu mmoja nyuma(2001) kilikuwa kwenye fainali ya ulaya dhidi ya Milan!

huko nako walibebwa?!mwaka huu Juve ni the only team iliyoqualify second round ya Ulaya,nako wanabebwa?hivi aina ya wachezaji walioko Juve,akiwalinganisha na wa kwake pale Milan,Galliani haoni formula ya 2 in 1 ilivyowatesa jana?kulikuwa na wachezaji wangapi wa Milan ndani ya Tevez mmoja?wangapi ndani ya Pogba mmoja?

Vidal, Morata, Evra, Chiellini, Buffon, Marchisio?yaani pamoja na timu yake kucheza vizuri,Galliani hajagundua ni wapi Milan yake ilizidiwa kete?hajajua ni kwa nini Tevez aliwakimbiza mabeki watatu wa Milan hadi kufunga bila kudhibitiwa?

Milan ilicheza mpira mwingi jana lakini mara zote walipokuwa na mpira,ilionekana mpira umeshikwa na wacheza mpira,ila possession ilipokuwa Juve,ilionekana dhahiri MPIRA UPO KWA WENYE MPIRA,ukitii kila ulichoamriwa kufanya na kuleta desired effects!hili hakuliona?

Serie A idhibiti huu mchezo wa kuichafua Juve for nonsense,it's not good for Italy and soccer!
 
juve2012


Umemaliza Mzee, waswahili wanasema mfamaji haachi kutapatapa, maumivu yanakua maradufu ukichukulia ni kocha wao waliyemtimua ndio kaifanya Bianconero itandaze soka la uhakika, lazima ashikwe na kwikwi.

Tukiwafunga Roma wanaanza mipasho wakiongozwa na Totti, Napoli tushawazoea wale ni bandits, Inter ndio wapiga majungu wakuu, sasa hadi Milan?

Ama kweli mti wenye matunda.
 
Last edited by a moderator:
Juventus Di Torino .original name of the club.yani Javananeh Torino shahreh kheili ghashang dar Italy.
 
Aisee Mourinho hii Napoli yangu ina homa za Mara kwa Mara. Aieleweki kwa kweli. Game za kushinda tunapigwa za kupigwa tunashinda.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mtoto Alvaro Morata mafisi yataanza kumnyemelea sasa hivi
 
Vidal anayo majibu

hivi hatuna mpigaji penati mwingine zaidi ya huyu baba?ngojea tu nimwite baba kwa heshima ya jukwaa manake nikimuita majina kulingana na upuuzi aliofanya juzi,ntapigwa ban tu hapa!
 
hivi hatuna mpigaji penati mwingine zaidi ya huyu baba?ngojea tu nimwite baba kwa heshima ya jukwaa manake nikimuita majina kulingana na upuuzi aliofanya juzi,ntapigwa ban tu hapa!

Pirlo is THE best Duniani katika hilo, siku ile sio penati tu, aliniboa match nzima. Alikua anacheza kama kalazimishwa, we should've cashed in kwa kweli, na yule mspain mrefu arudi tu kwao au tumpeleke Sassuolo kwa mkopo akapiganie namba na Zazza
 
Karibu ntapumzika kwa muda kushabikia club za Italy, nadhani umemsikia Arrigo Sacchi.

yule mzee nilimuheshimu sana kwa soka yake ya 1994 kule Marekani,lakini nimemdharau sana kwa comments zake za juzi,na si yeye tu,hata Tavechio,rais wa FIGC naye ni racist,yanayotokea viwanjani unayaona mwenyewe.Mino Raiola,yule agent maarufu wa big players ulaya kawapasha ukweli,kwamba soka ya Italia iko kaburini kutokana na kuongozwa na watu wenye akili finyu kama mzee Sacchi,akaenda mbali kwa kusema anajisikia aibu kuitwa mtaliano kama uitaliano ndio huu wa akina Sacchi.Ngoja tuone itakavyokuwa ila Juve wenyewe wamejaza madogo waafrika kwenye timu zao za vijana,hawaendekezi ujinga,wako kibiashara,na club nyingi Italia ziko hivyo,tatizo liko kwa fans na chama cha soka Italia.
 
Pirlo is THE best Duniani katika hilo, siku ile sio penati tu, aliniboa match nzima. Alikua anacheza kama kalazimishwa, we should've cashed in kwa kweli, na yule mspain mrefu arudi tu kwao au tumpeleke Sassuolo kwa mkopo akapiganie namba na Zazza

Vidal wanachompendea pale yuko combative sana,anajua kupambana,ila hivi karibuni hajitumi.Sijui ni nini tatizo!wachezaji wengi wa Juve hawako reactive,especially wanapokuwa hawana mpira.Llorente aende tu,ila Pogba,Morata,Marchisio,Lichsteiner tuna kazi kuwabakiza.
 
juve2012


Sacchi kaharibu sana, na Juventus yetu ndio haipendwi na FIGC in fact Serie A inatudumaza na kikwazo cha team kusonga mbele, hakuna upinzani kabisaaa.

Fans wanachoka kama sisi Mkuu, kwa kauli kama hizi au ile aliyotoa juzi Rais wa Lazio, kwanini fans wasichoke? Nani atawekeza kwenye vilabu vya Itali kama hali yenyewe ndio hii? Subiria kuona kina Pogba, Pjanic, Dybala wakifuata nyayo za Cuadrado msimu ujao, na sitasikitika a bit
 
Last edited by a moderator:
juve2012

Hivi kina Pogba unadhani wanajisikiaje kusikia kauli kama hizi? Morata ni kama yupo kwa mkopo pale, kina Marchisio bora wakacheze Spain au wakapige bingo EPL kuliko hii ligi yetu, it's not fair kwa hawa vijana kwa kweli.

Vidal kashajiona keki, kajiona bora zaidi ya wenzake kutokana na Conte kusepa akiprotest kuuzwa kwake. Kashatutumikia vyema, atembee, akajaribu bahati yake kwingine
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom