JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

Si kweli waingiaji wenyewe hujianda na kuwa fit hasa

Ona askari wa miavuli hawa makomandoo wa kike wa jeshi la ardhini wa Marekani wakiwa kwenye mazoezi hayo unayodharau kuwa ohh kuruka juu ya ndege ni ushamba hao ni askari wa kikosi kabisa cha kijeshi wanaitwa paratropers Army waweza tua popote na kupigana ardhini.Pamoja na Teknolojia yao wana warukaji juu ya ndege!!!

Hao wakiruka kama wa kwetu wa JWTZ

Paratroopers wa Marekani sio wa kike tu mkuu.
 
hata kama unailinda dhidi ya makombora kikosi cha makomandoo cha adui chaweza vamia physically .Unasubiria kombora lije unasikia watu wakishambulia ardhini hapo hapo kilipo na mibomu na mirisasi na askari wa ardhini
Wanajeshi wako vitengo tofauti, so hakuna vile mnavamiwa bila kutarajia, sehemu ya Tech ni specific kuwapa uongozo jeshi la ardhini, la anga hata la majini na pia tech yenyewe ikiwa kwenye vifaa mnavyotumia kama nchi, yaani vifaa viwe advanced kulingana na kisomo cha ujeshi mlichonacho, itakuwa salama kwa taifa kujitetea siku hizi!
 
nenda jerusalemu Israel uone kila ukipishana na watu 10 wanne ni askari waliovaa nguo za kijeshi wakiwa na bunduki kabisa pamoija na teknolojia yao

Hakuna jiji lenye askari wengi kama Jerusalem ISRAEL
Israel, military training is compulsory to every youth. National military service is mandatory for all Israeli citizens over the age of 18, although Arab (but not Druze) citizens are exempted if they so please, and other exceptions may be made on religious, physical or psychological grounds.
Regular Service
Permanent Service
Reserve Service
Special Service
Ndio maana Akari hadi Jeshi wako wengi, na almost kila mtu yuko fit kutumia silaha if needed.
 
Uzi wa hovyo sana Kama ujuwi ni bora ukae kimya umeandika nini.
Tambuwa kuwa kuna jesha la Anga, Nchi kavu na Maji.
Jeshi la Nchi kavu likiruhusiwa kuingia Gaza vita vya kuvunja tofali utaviona ,siyo tofali peke yake mpaka Visu,panga mawe kila sirah inaweza kubebwa kwenye mkono itatumika na Wapalestina.
Tofali limerushwa mwanajeshi wa Israel kabeba bunduku ilo tofali analizuia vipi au ataomba msaada kutoka kwa Iron Dome kuvunja Tofali .

Acha kudharau Jeshi letu
Sasa huyo wa kuvunja matofali, ndio ataacha jiwe limpate sababu ni sugu ama ni vipi? 😂
Once uko ground battle, ni kuoteana tu, rusha jiwe, narusha risasi, nakuzima. Rusha risasi, nami nikujibu na risasi, kwani iko nini. Vita ni vita, physical fitness inakusaidia kukufanya uvumilie kwa mda mrefu hata ukiwa umejeruhiwa, unaweza kufikiria timamu sio ku panic ka mtu asiyejielewa. 😂
 
Dunia ya sasa ni bora uwe na jeshi la watu 1000 wenye IQ kubwa na wenye kuweza kutumia technolojia kuliko uwe na jeshi la watu milioni moja ambao hawajui hata kuwasha kompyuta!

MTU ANAAJIRIWA HADI KUSTAAFU HAJUI KUWASHA COMPUTER, HAKIKA KUNA SHIDA KUBWA SANA
Wakati vitoto vya juzi vinaunda ma rocket ya hataree kule! 🤣 🤣 🤣
 
huna akili kabisa ndg.
acha tukueleweshe. utendaji kazi wa navy seal wanapokuwa ktk operation zao, asilimia kubwa unakuwa supported na zana za kiteknolojia.

huko angani kuna satellite ambazo mmarekani kaziweka ziweze kumsaidia ktk kuspy activities za maadui ili kuwarahisisha kazi navy seal kuvamia ngome ya adui.

katika masuala ya medani, ukusanyaji wa taarifa wa aina hii hufahamika kama imagery intelligence na signals intelligence. kwa asilimia 100 unakuwa supported na zana za kisasa zilizoundwa kwa teknolojia ya hali ya juu.

hoja ya mleta mada ina logic, usiibeze.
Mkuu watu tumezoeshwa "afande katere ova, tumefika LZ ova n out".... 😂 😂 😂 Hawajui vikosi vya nchi developed sahi wanacheza na tactical gear za maana, digital tech equipments na skills hataree.
 
Mleta mada uko very wrong kulinganisha nchi yenye defense budget ya $20 billion dhidi ya nchi yenye $1 billion na point. Bado hatulingani kwenye teknolojia na mambo kibao.

Hiyo Iron Dome unajua kuwa US ndio alifadhiri mradi huo, pamoja na ule mfumo mwingine mkubwa zaidi. Gharama za kufadhiri defense project ni kubwa mno Tanzania hatuwezi.

Kwanza nchi zote ununua silaha kulingana na uhitaji na maadui waliopo. Unanunua air defense nzito vile dhidi ya nani. Vipaumbele havioneshi kama tunahitaji air defense hata hiyo Israel ina silaha zinakoseana idadi kama submarines kwa vile sio kipaumbele na maadui wake hawapigwi kwa hizo wala hawatumii bahari kushambulia.

Nchi inayonunua panpasi na pedi nje ndio unataka itengeneze air defense system?
Mkuu T1, nimekupata sana hapo ila kakako anaongelea Military Modernization sio air defence tu bali vikosi vyote kuwa Advanced kiteknolojia na kuwa na uwezo wa kuvitumia, labda wakipelekwe mafunzo.
 
Ni wapi nimesema tununue iron dome? Hoja yangu ni kwamba tuwekeze kwenye tech na kuwekeza kwenye tech sio lazima kununua iron dome!!
Inaweza anza pole pole kweli, kama kununua vifaa latest na ku replace zile old ones, moja baada ya moja.
 
Vita ni kama game plan ya mechi za mpira wa miguu

Hao waisrael walienda Uganda kimyakimya kuwaokoa watu wao na kuondoka nao kimya kimya mbona hawakuenda na makombora yao
Israel vs Palestine... Sio Uganda, ile ilkuwa spec op kuokoa raia, makombora si ni kuhatarisha maisha ya captives, huoni hilo? Na pia spec ops huwa kimya kimya, sio nchi waenda pigana nayo ni bali kikundi cha watu
 
Mkuu hao makomandoo unaowasema wanavunja tofali ni special force, nadhani kama unayajua majukumu ya special force utaona umuhimu wa wanachokifanya kwa mfano moja ya jukumu la special force ni uokoaji katika mazingira magumu kwa mfano tukio la utekaji wa raia wa Israel nchini Uganda lilishugulikiwa na Mosad, maana yangu ni kuwa hata kama una teknolojia kubwaa kiasi gani bado kuna matukio hayahitaji teknolojia kwa mfano japo Marekani ina teknolojia kubwa ila mission ya kumkamata na kumuua Osama ilihitaji special force ili kutoathiri nchi nyingine hali ambayo ingepelekea vita ndo maana Marekani haikutumia drone, missile au kitu chochote zaidi ya hao makomandoo pia kwa mfano raia wa nchi yako wametekwa au askari wako wametekwa ukitumia makombola au drone utaua hadi raia na askari wako hapo ndo unakuja umuhimu wa special force
Pili Jwtz linawekeza pia kwenye teknolojia na kuna
jwtz lina aina nyingi za silaha na vifaa ambavyo vime advance ila huwezi ukaviona sababu siyo utamaduni wetu kuonesha kila silaha tuliyonayo japo hatuwezi kulingana na hao Israel au Marekani ila kwa maadui zetu na majirani tunaweza kuwa win
NB :ingekuwa vita ni teknolojia pekee basi Marekani kwa ushirikiano na kenya na umoja wa mataifa wangekuwa wameshakimaliza kikundi cha al shabab pia boko haram Nigeria ila jwtz special force ndo ilisaidia kuwaondoa m 23 Congo kwenye maeneo magumu kijiografia ambapo hizo teknolojia zilishindwa
Tech inaweza kutumika kwa njia tofauti tu sio lazma iwe kombora au drones. Hata intelligence inatumia tech nyingi sana, sababu bila tech ya Intel kupitia spy drones, Osama hangejulikani pahali yuko. Hadi siku anauliwa, Waamerika walikuwa na info tayari kwamba jamaa bado ako ndani ya lile jumba, hajatoka, hiyo yote thanks to technology. Kuna spec ops spy's walikuwa kwa ground in disguise kama wenyeji, walikuwa wanapiga picha pia kila siku ile nyumba Osama alikuwepo, kitakachoingia na kutoka, wakitumia Camera yenye kuvuta picha kwa ukaribu, wao wenyewe wilikuwa wamekodi jirani mbali kiasi tu na Osama. Picha zote wanazituma HQ kutumia hiyo hiyo tech, so tech ni muhimu sana kurahisisha kazi ya usalama.
 
Area51 marekan wanakuua kabisa

We unasema kulishwa wali na kuogeshwa lita1..
Aliyewahi kufa ni mmoja na yote hayo sababu hakutii sheria. Ila hawaui watu ukikaribia pale, tayari ushatumiwa wanajeshi wanakuja kukushika na kukupeana kwa polisi ama wakurudishe pahali umetoka.
 
Izo technology zinauzwa lakini kama taifa tukiamua kuwekeza kwenye kuunda zakwetu inawezekana. Control system engineering ni ile ile dunia nzima tatizo ni mtaji na rasilimali watu kutekeleza hayo bahati mbaya sana taifa letu au watu wenye mamlaka wanaamini vitu hivyo ni lazima vinunuliwe nje. Nimeshangaa sana hata mfumo wa luku hatujaunda sisi inamaana vijana wetu tuliwapeleke shule kushangaa vimbeta. China imepeleka chombo mars lakini 80% ya workforce wako below 30 kwa hivyo ni muhimu taifa kuwaamini vijana wake na kuwapa majukumu muhimu na sio kutunanga bila sababu majukwaani bila kuwapa majukumu makubwa Kama hayo
 
Tumekuwa watu wa kulalamika mno.
Ni vema tukaja na solution ya matatizo.
Mfano;kipaumbele kipi maboresho ya jeshi kwa gafla au maboresho ya jeshi kwa hatua kutokana na mahitaji ya wakati na uwepo wa rasilimali pesa?
pili,kuongeza bajeti y jeshi au kuongeza bajeti ya huduma za jamii.
Tatu,kuboresha mahusiano na kukusanya taarifa na kuzichakata na uvumbuzi wa kisayansi au kuboresha vifaa na teknolojia ya kupambana vitani?

Hayo ni machache ya kutafuta majibu kutokana na kipato chetu km taifa.

Kila mtu ana umuhim wake
Una pwenti mwanangu. Hata karate tulishaachana na kuoteshana manundu. Mwenye akili na atie akilini.
 
Jeshi ni siri . Naongea kwa uzoefu
acha kudanganya watu, dunia sasa usiri wa jeshi unabaki kwenye tactics and strategy ila sio kwenye technology.

jeshi linapokuwa na teknolojia yake ni rais kuitangaza teknolojia hiyo kwenye mataifa mengine na kuiuza.

marekani, israeli, urusi na china wanaingiza mapato makubwa kwa kuuza zana za kivita na mifumo ya kiulinzi kwa mataifa mengine.

biashara hii haijawahi kuwa siri. ndio maana mwaka 2014 jwtz iliponunua zana za kivita kutoka china, kila kitu kiliwekwa wazi na dunia ikajua.
Tanzania acquires new amphibious tanks, rockets and other weapons from China - defenceWeb

kuonyesha kwamba ktk dunia ya sasa hakuna usiri unaousema kwenye masuala ya jeshi, mwaka 2019 jwtz ilinunua helicopter za kijeshi na dunia nzima ilijua.
African Aerospace - Tanzania takes delivery of new helicopters
 
Back
Top Bottom