JWTZ, kweli mtu wa Jeshi la Polisi anawateka kama si kuwakamata your brothers na MPO kimya tu...

JWTZ, kweli mtu wa Jeshi la Polisi anawateka kama si kuwakamata your brothers na MPO kimya tu...

Hajasema kawakamata kwasababu wamekataa kubandika mabango kwenye nyumba zao, kasema amewakamata kwasababu wamechana mabango ya Samia

Na kuchana mabango ya mgombea yoyote ni kosa la jinai linaloweza kupelekea kufungwa, kupigwa faini au vyote viwili kwa mujibu wa Sheria The National Elections Act.

Kwahiyo kitendo cha wao kuchana mabango ni kujihusisha na siasa na pia kutenda kosa la jinai kwa wakati mmoja kitu ambacho ni kinyume hata kwa maadili ya jeshi.

Mwenye jukumu la kupeleleza kesi za jinai na kupeleka mahakamani ni polisi kwahiyo ni sahihi polisi kuwakamata na kuwaweka mahabusu, ila hawatapelekwa mahama za kiraia hadi taratibu za mahakama za kijeshi kukamilika wakikutwa na hatia wanaweza kufukuzwa kazi na wakakabidhiwa kwa polisi tena ili kuendelea na kesi yao ya kuchana mabango ambalo ni kosa la jinai.

Kwahiyo siyo suala la ushabiki sijui polisi wanaonea jwtz ni masuala ya kisheria na hamna aliejuu ya sheria isipokua dhana watu walizojijengea mitaani ndo tofauti na utaratibu/uhalisia ulivyo.
Jeshi halijihusishi na siasa, alafu mnaenda bandika mabango ya chama pasipo ridhaa yao katika nyumba zao ( hamuoni kuwa mna waingiza kwenye siasa ? ) kwa kufanya hivyo . Wangekuwa wamebandua kwenye nyumba za wengine sawa
 
Tunakoelekea nikutamu sana , jeshi limejengeka kwa misingi ya nidhamu na utii , kwa mazingira ya sasa hawapaswi kujibu ila nawahakikishia majibu tutakutana nayo soon ,tusipoteze heshima kwa Jeshi letu .tusipoteze matumaini kwa Jeshi letu .

Jeshi huwa halijui kupiga taarabu kama hao wengine ,wao wakilianzisha ujue damage yake nikubwa.
Mkuu unawapa heshima wasioistahili, hamna lolote Kwa hao!
 
Katika mahojiano exclusive Luteni Mwamba Luchembe anafunguka miaka mingi baadaye nini kilimsukuma kuvamia studio za Shirika la Habari la Zambia ZBC mwaka 1990 kutangaza mapinduzi ya kungoa serikali ya chama dola UNIP iliyokuwa inaongozwa na Rais Kenneth Kaunda baba wa taifa hilo.


27 May 2022
Luteni Mwamba Luchembe

View: https://m.youtube.com/watch?v=yY6JDPWaHuY
Former Zambian army officer Mwamba Luchembe reflects on the day he tried to overthrow Kenneth Kaunda in a military coup. (This interview was recorded while PF were in power and Kenneth Kaunda was still alive.)
Tulikuwa katika kambi yetu kilometa 500 kutoka mji mkuu wa taifa la Zambia, jiji la Lusaka.

1990 hali ya kisiasa na kiuchumi ilikuwa mbaya, wananchi walikuwa na manunguniko mengi ikiwemo ugumu wa maisha, ughali wa bidhaa muhimu kama unga wa sembe, ukandamizaji wa kisiasa uliokuwa unafanywa na chama dola kongwe kimoja UNIP

Maandamano yakatokea jeshi la Polisi likatumwa kudhibiti mandamano hayo lakini wakazidiwa na nguvu ya umma uliojitokeza .

Rais Kaunda akatoa amri jeshi la ulinzi la Zambia watoke kambini kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Hivyo mimi nilikuwa katika Battalion 5 Kaoma, nasi tukapewa amri tuende Lusaka kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Wakati tukiwa mesi tunakula chakula cha jeshi ambacho hatulipii, mawazo yetu yakaguswa na madhila ya wananchi wasiokuwa na uwezo wa kula ambao walijitokeza kwa wingi kuandamana huku sisi tukila chakula kwa uhakika kupitia kodi zao.

Hivyo tukaona nchi inaenda kubaya kutokana na kuwa na chama kimoja kongwe tawala kilichoishiwa mawazo ya kutanzua changamoto za raia.

Wazo letu likawa kuchukua nchi na kuiongoza kwa miezi sita huku tukijenga mazingira vyama angalau vitatu makini viundwe ili demokrasia iwepo nchini. Hatukutaka kuona vyama zaidi ya vitatu maana tunajua vyama vingine ni vya mfukoni ( briefcase) siyo vyama vya ukweli vya mawazo mbadala

Tukiamini demokrasia ya uwazi, uchaguzi huru, bunge makini vingeweza kuiondoa nchi ktk changamoto iliyokuwa nchi inapitia ...

Ndiyo maana niliongoza platoon iliyokuwa na wanajeshi 32 huku mimi ni kiwa ofisa wao hivyo jumla ya wanajeshi 33 tulivamia kituo cha taifa cha ZBC nami nikatoa tangazo la serikali kupinduliwa...

Tulikuwa tumekubaliana na kambi zingine za Kitwe, Mufulira n.k nao waingie ktk sehemu nyeti za utawala wa kiserikali ktk majimbo ili kukamilisha mapinduzi hayo...

Wananchi walijitokeza kwa wingi mtaani kufurahia tangazo la mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo wenzetu tuliokubaliana kuikamilisha kazi hivyo kote nchini walitugeuka.

Akatumwa askari mmoja mwandamizi atushawishi kuwa mapinduzi yetu hayakufanikiwa.

Nilikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha Central police nikafungiwa katika mahabusu upande wa wanawake, na wale mahabusu wote wanawake kwanza walihamishwa.

Wakaja wanajeshi wa idara ya utambuzi, maofisa wa usalama wa taifa na wa vyombo vingine kunihoji kwa muda wa wiki moja ktk selo hiyo ya wanawake.

Baada ya hapo walinipakiza ktk helicopter tukaelekea katika kambi nilitotokea iliyopo kilometa 500 kutoka Lusaka. Wakafanya upekuzi katika ofisi nikiyokuwa natumia kambini na katika nyumba niliyokuwa naishi kambini.

Wakanirejesha Lusaka hata hivyo usiku ulikuwa umeanza kuingia hivyo rubani wa helicopter akazima mawasiliano yote na kutua eneo mojawapo kwani rubani alitoa taarifa ya kuwa helicopter haina uwezo wa kusafiri usiku wa giza kufika Lusaka. Walizima mawasiliano ili kama kuna njama za wenzangu kuja kuniokoa zisifanikiwe.

Alfajiri na mapema tukamalizia safari yetu kwa usafiri wa barabara hii yote ikiwa ni njia ya medani, kwa waliopanga nami kufanya mapinduzi wasijue nilipo wala nini kimetokea kwangu mimi.

Mahojiano yakaendelea mjini Lusaka ktk nyumba maalum (safe house) kujaribu kupata habari zote za Mapinduzi na wahusika wote katika njama hii ya kupindua nchi.

Walitumia koleo / pliers kutoa meno yangu kavukavu bila ganzi, lakini situwasaliti wala kutaja wenzangu waliotayarisha jaribio la kuangusha serikali.

Baada ya kunisulubu hivyo, wakanirudisha kwa kificho kituo kikuu cha Polisi huku nikiwa na maumivu makali. Wakanipandisha ghorofani, watu wa Idara ya Usalama na wale wa Idara ya Utambuzi jeshini wakapanga mipango watawaambia nini raia hata polisi na wanajeshi watakaoniona.

Hivyo basi wakanivua nguo zote tukiwa ghorofani na kuzitupa kupitia dirishani. Kutoka juu ghorofani wakanitelemsha mzobemzobe mbiombio uchi wa mnyama nikiwa mtupu, kisha wale wote walikuwapo kituo kikuu cha Polisi wakanishangaa si polisi, raia na waandishi wa habari hata wapita njia wakabaki wanajiuliza kulikoni..

Watu wa Idara na Vyombo wakasema huyu ni kichaa aliyewehuka siku nyingi kabla ya mapinduzi, faili lipo jeshini na kwa vile alikunya sana Pombe na bangi ndiyo maana akatimka kwenda, kutangaza mapinduzi yale.


Baada ya miezi miwili nikastaafishwa jeshi kwa sababu za 'kiafya' yaani ugonjwa wa akili. Hata hivyo vyombo vya usalama vikamwambia rais pamoja na hii hadaa tuliyoitengeneza ukweli watu wanataka na wanaamini mabadiliko ya kuleta vyama vingi vya kisiasa. Hivyo ni bora rais aanzishe mchakato wa mabadiliko ya katiiba kuruhusu na kuafiki kwa moyo mkunjufu vyama vingi, demokrasia na uchaguzi huru kupitia tume huru ya uchaguzi.

Hivyo mwaka 1991 mchakato wa vyama vingi na katiba mpya vikapitishwa na bunge la Zambia kwa usimamizi wa karibu wa rais Kenneth Kaunda.

Mapinduzi yale yaliyoshindwa hata hivyo yalileta jambo chanya kuwa watu wanataka mfumo wa vyama vingi, yalionesha kuwa ukiritimba wa chama dola kongwe cha UNIP na rais nguvu yao ya ushawishi wa chama kimoja umepungua na wajitayarishe kuwa chama cha upinzani.

Kwa ujasiri wa Luteni Mwamba Luchembe kuongoza jaribio la mapinduzi , sasa anahesabika kama baba wa mabadiliko / reforms za kupatikana katiba mpya na demokrasia ya vyama vingi nchini Zambia.

Katika mitaala vya masomo ya uraia / civic Luteni Mwamba Luchembe anatokea ktk vitabu mashuleni kuwa alikuwa chachu ya mabadiliko yaliyoleta vyama vingi kuruhusiwa nchini Zambia.

Mbali ya watoto wa shule kusomeshwa mchango wake Luteni Mwamba Luchembe kuleta mabadiliko, sasa katika Makumbusho ya Taifa mjini Lusaka na makumbusho ya majimbo mbalimbali nchini Zambia picha yake ipo miongoni mwa watu waliotoa mchango kwa taifa la Zambia hadi kufikia lililopo sasa.

Rais Frederick Chiluba aliposhinda uchaguzi wa vyama vingi kupitia chama cha upinzani alimrejesha Luteni Mwamba Luchembe kazini na kumpa cheo mserereko hadi kuwa Captain kisha kumstaafisha kwa kumpatia pensheni stahiki ya cheo alichofikia.

Source :
 
Hili siyo Jeshi la Wananchi tena bali ni Jeshi la Kulinda Mafisadi.
 
Kisa mtu ama watu na nyumba zao wamekaa kuweka mabango ya Samia kwenye kuta zao...

halafu ni kama yeye Sasa ni Mwenyezi Mungu Sasa yeye kusema biashara yao imeisha...kwamba ana Haki miliki na maisha ya watu...

Aisee ..halafu hivi mnajua linaitwa jeshi la WANANCHI ...NA SIO jeshi la ccm ama jeshi la kikundi Cha watu
Tuliwaambia hao wanajeshi wa Tanzania hawana tofauti kubwa sana na raia.

Wengi wenu hamkutaka kusikia.

Mkataka wanajeshi wachukue nchi.

Mtaelewa tu.

Nyani Ngabu
 
Wanajeshi makini si watu wa kujibizana. Kwahiyo sitaki kuwabagaza kuwa ni waoga. Ngoja tuwape muda tuone… kujibizana na mwafele ni kujikosea heshima. Unamkamata unamtia ndani na anapokea fimbo mijeredi 50 kila siku iendayo kwa Mungu.
Sio JWTZ
 
Wenje anasema vijana wa Chadema ni wajuaji na wachonganishi. Kwa kifupi ni miongoni mwa kundi la wapuuzi kupindikia. Hawatakuelewa mkuu tena subiri kuitwa huna akili. Sjui wanataka nini maana likifanyika jambo kisheria wao wataponda? Wao ndio wenye haki ya akili, uelewa, ujuaji, uzalendo nk nk.
Wenje ana akili gani nambie mchango wa Wenje katika taifa ili maana ni sigara nyota haeleweki ni upinzani au chama tawala huyo ni takataka
 
Back
Top Bottom