JWTZ msifanye makosa DRC, haya ndio yatakuwa madhara yake

Kagame naye ana - back up ya kisirisiri Israel, US, UK na wengine. Huu mtifuano utaishia wapi?
Kama ni hivyo anatafutwa mshirika wa Urusi na China ambaye ni Afrika ya kusini hapo.
 
Acha bangi.
Sir you need to get your self together and stay focused
Huwezi kuishi katika hii dunia kama ujaewekeza Rohoni vya kutosha, and there is no shortcut ndio maana imeandikwa wataukumiwa kwa sheria zao hata wasio ijua sheria watapotea pasipo na sheria
Warumi 2:
 
Nakazia tuwe na makubaliano kimaslahi na serikali ya DRC …. Mana hii oparation nizaidi ya uwanachama
 
NARUDIA TENA KWA ELUFI KUBWA, NCHI PEKEE INAYOWEZA KUMALIZA HAKO KAMGOGORO CONGO NI TANIZANIA.
HII NCHI KWA SASA INAUWEEZO WAKUTATUA MGOGORO WOWOTE KATIKA TAIFA LOLOTE IKIAMUA NA KWA SASA RAIS SSH NDIYE RAIS MWENYE NGUVU DUNIANI!!!!!
NAJUA MTABEZA NA KASHIFA NYINGI LAKINI UKWELI NDIO HUO. MKITAKA MAELEKEZO NITAFUTENI.
MIMI NASEMA HIVYO NIKIMAANISHA WALA HAMNA KIFICHO.
BAHATI MBAYA SAAANA WATU WENGI HUMU HATA ELIMU YA KIROHO HAMNA WAKATI IMESISITIZWA MTU ATAISHI KWA MKATE TU BALI KWA KILA NENO LITOKALO JINYWANI MWA BWANA ( NAJUA AMUELEWI MAANA YA HILI ANDIKO)

NIMEWEKA MAJINA YANGU NA NAMBA ZANGU ZA SIMU HILI WENYE HAKIRI/HEKIMA TIMAMU WAENDE KWA MUNGU WAO WAULIZE HUYU JAMAA NI NANI?????
YAANI HAKO KATATIZO KA CONGO TANZANIA/RAIS WA TANZANIA ANAUWEZO WA KUKATATUA ATAKAVYO YEYE AKIAMUA NA HAKUNA WA KUPINGA.
MGEJUA SIRI ILIYOPO KWENYE TAIFA KILA MTANZANIA MAOMBI YENU YANGEKUWA YAKUSHUKURU

IMEANDIKWA WANA MACHO HAWAONI WANA MASIKIO HAWASIKII.

VITU VYOTE VIKO WAZI LAKINI WENYE NCHI HAWAONI.
 
Dah kazi kweli kweli
 
Bila shaka wataamka na kuanza kuona kwa maono ya miaka 50 hadi 100 huko mbele.

Warundi na Wakongo wanatuita sisi Watanzania ndugu zao wanataka tuungane ila wenye mamlaka ya kufanya maamuzi hawajiongezi kwa kuona umuhimu wa kuunganisha huu undugu uliopo.

"Tuanze kazi sasa hivi,siasa zao ziendelee lakini jicho letu livuke nje ya Ziwa Tanganyika."
 
Acha wachukue kila wanachotaka. We linda mpaka wako wekeza kwenye elimu ya watu wako
 
Sasa jamaa kutwa kukatika mauno na uchawa
Wabongo nao wanaelekea huko huko

Ova
 
Ni kumfiagia mpaka kigali, apigwe pande zote ila aachiwe upande wa kaskazini akimbiliea afrika ya kati. Asiruhusiwe kukimbilia uganda ataenda kujipanga upya. Ni kitisho nchi za maziwa makuu
 
Mithali
29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
Acha kujifanya mtu wa rohoni ili kutuzuga hapa. Zamani mataifa kibao ya Africa yaliingilia huo mgogoro ukaitwa the great African war lakini mbona haukuisha. Ngoja nikupe elimu kuhusu huo mgogoro.

Hapo zamani za kale Kongo ilikuwa inaongozwa na Mobutu Seseko kwa bahati mbaya au nzuri kulikuwa na waasi wanampinga wakiongozwa na Laurent Kabila. Mapambano yao waliyaanzisha mashariki mwa Kongo.

Pia hapo zamani za kale (sorry mpaka leo miaka 40 sasa madarakani) Uganda inaongozwa na Yoweri Museveni hata hivyo kulikuwa na waasi wanampinga wanaitwa ADF. Waasi hao baada ya kuzidiwa na majeshi ya serikali ya Uganda walikimbilia mashariki ya Kongo.

Pia hapo zamani za kale kulikuwa na waasi wanaitwa RPF walikuwa wanaipinga serikali ya Rwanda iliyokuwa inaongozwa na Juvenal Habyarimana. RPF walikuwa kambi zao zipo Uganda na lengo lao nafikiri ilikuwa kupigania haki za watutsi kule Rwanda. Serikali ya Rwanda ilikuwa na wahutu zaidi enzi hizo. Kuna baadhi ya watu ndani ya serikali ya Rwanda walianzisha kikundi kinaitwa Interahamwe (maana yake wale walioshikamana) hao waliamini kwamba ili kumaliza changamoto ya uasi wa RPF inabidi waue watutsi wote Rwanda ndio chanzo cha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Basi wakaanza project chinja chinja ndani kama ya wiki moja waliua watutsi kama 800,000 (utamu wa vita huo) hivi kinachotisha zaidi ni kwamba walikuwa wanatumia zaidi mapanga kuua. Ili kumaliza hayo mauaji RPF wakaingia Rwanda wakafanikiwa kukamata mji mkuu wa Kigali wakaunda serikali. RPF ndio chama cha siasa kinachoongoza Rwanda hata sasa (hapo mwanzo kilikuwa kikosi cha waasi). Wale wabaya wao yaani Interahamwe walipigwa wakakimbilia mashariki ya Kongo. huko inasemekana walianzisha kikosi cha waasi kinaitwa FDLR kupinga serikali ya RPF.

Kwahiyo waasi wa Uganda na waasi wa Rwanda wapo mashariki ya Kongo. Basi Uganda na Rwanda waliamini ili kuwashinda wale wa waasi kwanza wamsaidie Laurent Kabila kuipindua serikali ya Kinshasa na wakafanyo hivyo. Laurent Kabila akawa rais wa Kongo. Kishapo sasa Uganda na Rwanda waendelee na msako dhidi ya waasi wao walio mashariki ya Kongo. Lakini bwana Kabila hakupenda majeshi ya kigeni yaopareti kwenye mipaka yake, kwa hiyo kwa hiyo akawaambia Uganda na Rwanda wasepe. Nafikiri Uganda na Rwanda wakawaza huyu jamaa mjinga nini, basi ukawa ugomvi baina Kongo ya Kabila dhidi ya Rwanda na Uganda. Kabila akaomba msaada kwa mataifa mengine wakaja Zimbabwe na Angola kumsaidia. Mataifa kibao ya Afrika yakawa na majeshi ndani ya Kongo ikaitwa the great African War. Yule bwana Kabila atauawa na mmojawapo wa walinzi wake na washirika wake watampa nchi mwanae anaitwa Joseph Kabila.

Mataifa kama Zimbabwe sijui nani wataondoka Kongo lakini waasi wa serikali za Rwanda na Uganda bado wataendelea kuwepo mashariki ya Kongo. Hivyo tegemea majeshi ya Rwanda na Uganda bado yataendelea kuwepo pale mashariki ya Kongo kupambana na wabaya wao. Hata hivyo baadhi ya watu wataanza kusema majeshi ya Uganda na Rwanda hawapo tu mashariki ya Kongo kwa ajili ya kulinda usalama wao bali pia wanabeba rasilimali pale. Kuna madini pale yanatumika kutengeneza betri za Kompyuta na Simu.

Aisee nachoka kutype sana stori haiishii hapo. Ila hicho ndio kama kiini cha ugomvi
 
Uchawa na kulinda maslahi ya chama tawala unaanza kumeza focus na credibility inapotea. Acha tuone
 
Acha wachukue kila wanachotaka. We linda mpaka wako wekeza kwenye elimu ya watu wako
Mithali
29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
Tatizo wewe unaenda kwa historian wakati maneno ya Mungu hayabadiriki. Imendikwa pasipo na Roho sisi hatuwezi lolote. Ukikataa kuwa wa Rohoni then your nithing
 
Na kumbuka anaposema mkamate sana Elimu aimaanishi Elimu Dunia ya Bachelor , masters, Doctor, PhD, na professor hapana anamaanisha mkamate sana Roho mtakatifu yeye anakupa uzima in everything you deliver
 
Nadhani wanaona. Mtulize kabla hajakutuliza kudadeki.
 
Duh nimekubali sana aisee. Hivi unajuwa ukianzisha kanisa alafu ukawa mbishi hivyo halafu unaongea mavitu ambayo hayaeleweki watu wanaweza wakakufuata ukakusanya sadaka ya kutosha.

Lakini kuhusu migogoro kama hii, suluhisho ni maelewano lazima uongee vitu ambavyo watu wanaelewa. Siri ya kuleta amani ni maelewano, watu wakishaelewana tu wanaweka silaha chini. Ndio maana rais JK (sitaki kukumbushia maugomvi ya zamani Mungu aepushie mbali) alishauri RPF wazungumze na FDLR wayamalize. Lakini RPF walikasirika sana kwa hiyo kauli kwa sababu ya kile ambacho watu wao walifanyiwa mwaka 1994 wakasema rais Kikwete ni FDLR sympathizer kidogo kiwake. Lakini viongozi wa Tanzania wamejaliwa busara moto ukazima.

Ukiongea mavitu yasiyoeleweka unazidi tu kuwatia watu gizani na kutengeneza confusion itakayochochea ugomvi. Ila ukiongea kitu kinachoeleweka unawaweka watu nuruni.

Tambua wewe ni mkristo unakuja na habari zako kuhusu roho mtakatifu. Lakini siyo kila mtu ni mkristo na hata si kila mkristo atakuelewa, kwanza wakristo wamegawanyika kwa madhehebu tofauti tofauti. Imagine akaja mtu anayefuata dini za asili za Afrika akaja na habari zake kuhusu mizimu, wewe utamsikiliza. Si utasema shetani toka.

Tambua kutofautisha field tofauti tofauti, kuna sayansi ya siasa, kuna teolojia na kuna mambo ya kijeshi kila kimoja kina nafasi yake. Huwezi tatua kila changamoto kwa kutumia teolojia peke yake utakuwa ni mpumbavu.
 
munosco wko pale kusimamia wizi wa rasilimali za congo. M23 anapata support kubwa ya mabeberu unataka jwtz achokoze moto? Ukiona mbwa amepanda juu ya mti ujue kuna mtu amempandisha. Kinachoendelea congo sio rwanda anaempga mkongo bali kuna mtu nyuma ya mgongo wa rwanda anataka madini ya congo na ukimpga mrwanda huyo mtu nyuma yake atakufanya mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…