JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

Tahadhari
Jeshi linapotoa matamko aina hii mjue si jeshi la wananchi tena.

Jeshi la wananchi litaelimisha na kuviachia vyombo vya kutekeleza sheria kufanyakazi zao.

Jeshi linapotoa amri kwa raia ni majaribio ya kiimla yapo nyuma yake.

Amiri Jeshi Mkuu anapodhani haya matamko ya Jeshi dhidi ya raia ni sahihi ni wazi kuwa tuna ombwe kubwa la uongozi nchini.

Mkuu wa Majeshi ni busara akayasahihisha haya mambo au akaachia ngazi ili kupisha wenye weledi, utii na mahaba lwa nchi kuongoza jeshi
 
Halafu ni nani kawapa mandate jeshi kufanya kazi ya police ,?
Hii ni banana republic ?
Kwa kweli hii nchi hii !
 
Halafu ni nani kawapa mandate jeshi kufanya kazi ya police ,?
Hii ni banana republic ?
Kwa kweli hii nchi hii !
Jeshi linapaswa kutimiza wajibu wake wa kikatiba na kosheria au sivyo litafahamika ni la kihuni
 
Haya majamaa ni maoga hatari. Nakumbuka maandamano hewa ya Mange kimambi... Majitu mazima eti yakaingia mjini eti yanafanya usafi.

Yani Mamjeshi wakazuga kama BUDEGE wanakusanya vinyesi barabarani....

Pathetic
 
Jeshi linapaswa kutimiza wajibu wake wa kikatiba na kosheria au sivyo litafahamika ni la kihuni
Sidhani kama ni wajibu wa JWTZ kupita uraiani kusaka nguo zinazofanana na zao. Wana Jukumu kubwa sana la kulinda taifa na mipaka yake... Sio kusaka vitambaa
 
Sidhani kama ni wajibu wa JWTZ kupita uraiani kusaka nguo zinazofanana na zao. Wana Jukumu kubwa sana la kulinda taifa na mipaka yake... Sio kusaka vitambaa
Hawana kazi ya kufanya.
Wanataka kufqnya mechi ya kirafiki na wananchi.
Mawe huwa ni adimu mijini lakini wenye kiu huyapata fasta🤣
 
Hawana kazi ya kufanya.
Wanataka kufqnya mechi ya kirafiki na wananchi.
Mawe huwa ni adimu mijini lakini wenye kiu huyapata fasta🤣
Ina maana wameshamaliza kufyeka zile nyasi pale Lugalo?
 
Kuna jirani yangu mgambo kanimegea siri ya jw kukagua nguo zao mtaani kuwa ni mbinu ya kuichukua nchi kama wanavyofanya wenzao wa gaboni,Mali na Burkina Faso.wameona huyu mkizimkazi nchi anaipeleka korongoni
 
Wacha waingie mtaani ndo vzr tena nyumba kwa chumba
 
ila ni kwamba: wakimkuta mwenye hizo nguo hawana mamlaka kisheria kumwajibisha! wanapaswa wampeleke kituo cha POLISI kwa hatua za kisheria. Hawatakiwi kujichukulia sheria mkononi.

Yesu anaokoa!
 
Wenzao wanapindua serikali huko wao wanasaka sare huku [emoji28]

I don't condone mapinduzi ila hii ni task ya kiboya sana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hadi nimeogopaa.
 
Samahani naomba kuuliza, haya ni majukumu ya jeshi au Polisi? Kadri ya maelezo yako.
 
ila ni kwamba: wakimkuta mwenye hizo nguo hawana mamlaka kisheria kumwajibisha! wanapaswa wampeleke kituo cha POLISI kwa hatua za kisheria. Hawatakiwi kujichukulia sheria mkononi.

Yesu anaokoa!
Nadharia ndio inavyo amini hivyo. Lakini kwenye vitendo sio. Jaribu kufuatilia stories za vijiwe mishoki mishoki upate uzoefu wa wale ambao kwa bahati mbaya/makusudi waliingia kwenye aga zao ima kwa kujua au kutokujua.
 
Samahani naomba kuuliza, haya ni majukumu ya jeshi au Polisi? Kadri ya maelezo yako.
unavyosikia jeshi wataingia mtaani kukagua sare zao unadhani polisi hawatuwepo,
kuna muda itifaki inavunjwa kulingana na mazingira jeshi anapewa sehemu kubwa ya kufanya kazi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…