Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kama mtu anakutwa na VAZI linalosemekana ni la Jeshi, ni mahakama pekee, ndio yenye mamlaka kuamua vazi hilo ni la Jeshi au la. JWTZ hawana mamlaka KUTAIFISHA vazi (mali) ya raia pasipo IDHINI ya sheria. Kama mtu amekutwa na vazi ya aina hiyo, sheria inataka utaratibu ufuatwe.
Kama mtu huyo anaaminika kutenda kosa, basi sheria inataka akamatwe, afunguliwe mashtaka kisha mahakama itamke wazi kuwa mtu huyo amekosa au la. Mahakama ndio hutoa adhabu kwa mkosaji au kutoa amri ya KUTAIFISHA mali na si JWTZ ama Jeshi la Polisi.
Angalizo:
Ni jambo gumu mno KUTHIBITISHA mahakamani vazi la Jeshi, hata kama yanafanana vipi na vazi RASMI! Kuna VIELELEZO vinavyotofautisha vazi rasmi kati ya Majeshi ya nchi moja na nchi nyingine. Vielelezo hivyo ni lazima viwepo kwenye vazi lenyewe ili lifanane na vazi la Jeshi.
Lakini, ufanano si wa mwonekano tu! Ukisoma sheria za PENAL CODE, The National Defence Act, 1966 & National Security Act, zote nimeeleza vyema. Kuna "key words" zimetumika kwenye sheria ili kusaidia utambuzi wa mavazi RASMI ya Jeshi.
Sio kwa namna ambavyo wengi wenu mnaaminishwa! Ni vyema sana sheria zikasomwa na KUELEWEKA vizuri. JW kisiwe chombo cha kuleta taharuki kwa raia. Mwisho, mahakama & sheria za nchi hii haziwezi kumkuta mtu na hatia endapo atakutwa na vazi RASMI la Jeshi la nchi nyingine.
Sheria ya Tanzania, inalinda "VAZI RASMI" & "SINAZOFANANA NA VAZI RASMI" tu. Hapa "zinazofanana" ndio imekuwa KIZUNGUMKUTI kueleweka JWTZ au labda wameamua KUPUUZA tu! Hili neno "zinazofanana" lina maana TOFAUTI kabisa na wanachowaambia raia. Sheria zisomwe vyema, zieleweke.
#BabaMwita
Sent using Jamii Forums mobile app