Kaa kimasta kijana, hisia sio mzigo mzuri kwako

Kaa kimasta kijana, hisia sio mzigo mzuri kwako

Hakuna noma mkuuda, hata wewe upunguze matumizi ya hisia, ulikua mahabusu ya jf kwa sababu ya kushindwa kuzidhibiti hisia zako.
Umeniwahi. Siku ile hisia zilimzidia mpaka aka-mean malice to everybody na kuvuka mipaka. Ajabu sasa hata waliojitolea kumkanya nao hakuwasikiliza. Hisia!

Mimi nadhani hisia hazizuiliki maana ni sehemu ya uumbaji. Hata watu wa Evolutionary Biology watakwambia kwamba hisia ni kitu cha lazima. Hata ukienda Serengeti utaona. Dume la Simba pure Alpha male tena kwenye prime yake na linaloongoza familia yake kubwa kibabe kuna wakati linazidiwa na hisia hasa kwa watoto, wake zake, marafiki n.k. Madume ya nyani, hali kadhalika. Na viumbe wengine.

Cha muhimu nadhani ni kujua wapi hisia zinafaa kutumika; na wapi hazifai. Na hili si jambo rahisi maana hisia na uchanuzi wake kunachangiwa na mambo mengi sana mchangamano yakiwemo mazingira, malezi, mtazamo wa jamii, makuzi, mfumo wa elimu, peer pressure, mtazamo wa dini na mengineyo mengi.

Kwa sasa hali ni mbaya zaidi kwa sababu mtoto wa kiume ni kama vile ametelekezwa na jamii ili ajipambanie mwenyewe. Nguvu zote zimewekezwa kwa mtoto wa kike wakati ukiangalia kwa hali ya sasa mtoto wa kiume pengine ndiye ana changamoto zaidi hasa ukizingatia kuwa yeye ndiye bado anategemewa kuwa mlinzi, mtoaji, kuhani na baba wa familia yake huko mbele ya safari.

Kusema tu kwamba mwanaume hapaswi kuwa na hisia hasa katika mazingira haya ya sasa sidhani kama inasaidia sana maana hisia siyo kitu halisi kinachoota na kukua tu ghafla katika ombwe bali ni majumuisho ya jumla ya uzoefu wote wa mtu anaoupata katika miaka yake yote aliyoishi hapa duniani.

Inabidi kuwaza kwa kina zaidi kama kweli tunataka kumsaidia mtoto/kijana wa kiume ili aweze kujinasua kutoka katika mitego mingi inayomkabili hasa katika dunia hii ya sasa iliyojaa mambo ya kike kike na uke uke!
 
Back
Top Bottom