Nashangaa zaidi kuona ni sisi sisi wanaume wenye nafasi mabalimbali kwenye jamaa tumamsahau mwanamme na kumtukuza mwanamke kiasi kwamba tunatamani mwanamme aishi na kuact kama mwanamke nashindwa kuelewa izi agenda zinatoka wapi so sad
Ni ajenda ya dunia nzima kumwondoa mwanaume kutoka katika kiti chake cha ufalme, ubaba na ukuhani. Na haijaanza leo.
Mizizi yake ilianza kusimikwa kwenye mvuvumko wa feminism - wanawake walipoamua kuinua nyuso zao na kuanza kupambania haki zao na usawa. Baadaye feminism hii iliyokuwa na malengo mazuri iliingiwa na uyai viza pale ilipotekwa na radical feminists ambao walianza kudai si haki tu na uhuru wao kama wanawake bali usawa kamili na wanaume 50/50; wakaenda mbali zaidi mpaka kudai kuwa hata miili yao ilikuwa ni "mitakatifu" sana kuweza "kuchezewa" na wanaume. Inasemekana tapo hili ndilo hasa lilipalilia usagaji na mambo mengine tunayoyaona leo ambayo lengo lake ni kumkuza mwanamke na kumfanya kuwa "kichwa"
Baada ya hapo vita sasa vilielekezwa kwa mwanaume mwenyewe. Wakati karibu dunia nzima imeungana ili kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anapata kila kitu; hata zaidi ya mwanaume, mtoto wa kiume yeye yupo yupo tu ametelekezwa mpaka wazazi sasa wanakiri kuwa siku hizi ni chalenji zaidi kulea mtoto wa kiume kuliko mtoto wa kike. Ajenda za ushoga kila kona. Kujibadilisha jinsia. Kuwa soft. Kulelewa. Usawa.
Matokeo yake ni vurugu tupu. Ndoa hazieleweki. Familia hazieleweki. Jamii pia haieleweki.
Kwa ujumla kuna mvuvumko na juhudi za makusudi kumwondoa mwanaume kutoka katika kiti chake cha kifalme, ubaba na ukuhani. Ndiyo maana wanakwambia
the future is female!. Na kwa agenda hizi za makusudi na matokeo haya tunayoyaona, ni kweli the future is female!
Kama Waafrika kuna lo lote ambalo tunaweza kufanya ili kuzuia ajenda hizi za wakubwa wa dunia? Au inabidi tukubali tu kuwa ndiyo dunia inakokwenda; na kwamba ajenda hizi ni sehemu ya haki za binadamu maana kila binadamu ana uhuru kamili wa kuwa vile anavyotaka kuwa na kuishi vile anavyotaka kuwa bila kuingiliwa na mwingine? Na kwamba hakuna absolutes bali kila kitu ni relative (kama kwenye relativity) ya Albert Einstein?