Kabendera, unakoseaje kwenye kitabu mwaka aliofariki Sokoine, tena mara mbili kwa mpigo?

Ac
 
Kwa unavyofikiri ni sawa kabisaa no 1 kwenda kumbaka no 2? Yaani akili yako haikwambii kwba hapa kuna tatizo? Maana makazi Yao ynalindwa na vyombo mbali mbali vya uslama. Tena ilikuwa usiku! Kuna mawili amepotoshwa au kafanya makusudi ili auze. Sasa shida siyo kwake, shida ipo kwa editors na proofreaders. Je waliona, wakamwambia, akakataa au hawakuona maana kuna vitu vinakosa mtiririko sawa wa mawazo kama kweli havikuonwa.
 
JokaKuu, Nguruvi3 , Nyani Ngabu, Pascal Mayalla hebu njooni mtoe maoni yenu hapa wakuu.
Ni kosa lakini si tatizo linaloathiri habari ya kitabu.
Ni kosa kwasababu wanaotafuta sababu wamepata!

Sokoine alikufa, ni Kweli. Tarehe 12, ni kweli. Mwezi April, ni kweli. Mwaka 1983 si kweli, na imerudiwa page zinazofuatana kwasababu mwandishi na ''reviewers'' walikuwa ''fixated' kwamba ni kweli
Laiti ingalikuwa 1983 na page inayofuata 1984 waliopitia kitabu wangehoji mbona kuna tarehe tofauti?

Someni kitabu kwa maudhui yake kuna mengi sana ya kuelewa.
 
Copy tushanunua tayari zipo kwa watu, atazikusanya vipi?
Ilikuwa tuu ni sababu ya kuki promote tuu, ila hakuna lolote!! Absalom kibanda kapewa kakaa nacho wiki nzima na hakufanya chochote,

Paskali mayala naye kapewa na hakugundua lolote!!

Meena naye alipewa na hakuona shida!

Balile, to mention the few, Hawa wote hawajaona chochote, inabidi tutajiwe angalau wanasheria wawili waliopitia hiki kitabu
 
Nguruvi,

Kuna tatizo la "all or nothing" false dichotomy fallacy.

Kitabu ni muhimu, kina habari nyingi, kina tija sana, kilihitajika sana.

At the same time, hilo halimaanishi kuwa Kabendera hana room for improvement katika kufanyia editing na proofreading.

Of course kuna watu watakaotaka kutumia any small mistake ku discredit kitabu kizima.

Lakini pia, kuna watu tunaopenda Kabendera awe makini zaidi, tunataka kuweka constructive criticism, tunachambua kitabu pamoja na makosa yake, ili second edition isirudie makosa haya, au kitabu cha pili cha Kabendera (amesema kamaliza kuandika vitabu viwili) kisiwe na makosa haya unayoweza kuyaondoa kwa Google search.

Kuondoa makosa haya kutaondolea msemo hata wale watu wanaotafuta makosa kisiasa ili kuondoa credibility tu.
 
Bongo unaweza kumpa mtu kazi ya kupitia kitabu yeye anapiga bia bar tu, anakwambia kapitia kiko poa tu.
 
Ni kosa dogo! Hilo haliondoi maudhui ya Kitabu.
Hakuna niliposema linaondoa maudhui ya kitabu, kosa kama dogo ndiyo linawez akuwa baya kabisa kwa sababu ni dogo na linaepukika kirahisi.

Hilo lilikuwa ni kosa ambalo Google search moja tu ingelifuta.

Jamani, tuache this all or nothing false dichotomy.

Ninaweza kukipenda kitabu na kuona uzuri wake halafu pia nikaona makosa aliyoyafanya Kabendera kwenye editing na proofreading strategy, na nikataka Kabendera na timu yake wafanye kazi nzuri zaidi hapo.

It's not like nasema kitabu kimekosea mwaka, hivyo mambo yote yaliyosemwa kuhusu Magufuli ni uongo.

Nuance please, tuwe na perspective, context na sophistication kidogo.
 
Yeye kaandika amekamatwa lini??!
 
Huyu Magu kamvuruga itakuwa, nguli mpaka kashindwa ku Google tarehe ya kufariki Sokoine?
Bora hata hilo, hili la kusahau kuwa kakamatwa lini sio mchezo, ikiwa lake mwenyewe binafsi anasahau, vipi hao watu 250, waliompa taarifa??!!

Ila mkuu kwenye maandishi nmeona sehem kuwa alipewa taarifa na opposition leaders kuhusu kupigwa risasi za kichwa Ben, (Kuna kitu najiuliza hapa, ingawa ni nje ya mada kidogo)
 
Naunga mkono hoja, sometimes, even the greatest magicians runs out of tricks!, kwa level ya ubobezi wa EK, no proof reader would have doubted the dates!.
P
Mpaka za matukio yaliyomhusu yeye binafsi??? Hatari sana!!
Utetezi wake kule X pia haueleweki!!

Kajifichia sehem ya "majina Yao nitaenda nayo kaburini"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…