Kabla dini za kigeni kuletwa Afrika, wazee wetu waliabudu nini?

sos_10

Member
Joined
Jun 23, 2024
Posts
7
Reaction score
21
Huwa najiuliza kabla Wakoloni kwa maana ya Wazungu na Waarabu kutuletea dini wakitumia wafanyabiashara, wamishenari na wapelelezi, (traders, missionaries and explorers), wazee wetu huku Afrika waliabudu katika dini gani? Je kwakuwa dini za kigeni hazikuwepo ina maana watu wote walioishi nyakati hizo walienda motoni kwa kuabudu miti, mizimu na wanyama. Je ipi ni dhambi machoni pa Mungu, kutokwenda kanisani na msikitini au kutenda mabaya!
 
Dini kwa Allah ni moja tu. Uislam.
 
1. Waliabudu miungu ya dini za jadi. Dini zipo nyingi, zinazaliwa, zinakuwa na zinakufa.
Dini ni majaribio ya mwanadamu kuufafanua ulimwengu ikiwa hawezi kupata majibu sahihi.

2. Kimsingi hawajaenda popote, wameoza na kurutubisha ardhi. Miungu ni vyombo cha dini, vinatengenezwa na binadamu.

Kwa uelewa mdogo sana wa binadamu wa zamani, alifahamu vitu vingi anavyotumia alivitengeneza yeye, mfano vyungu, mikuki nk...
Na alielewa hivyo vitu kiasili havikuwepo, alivisanifu kwa ubunifu wake mfano alifinyanga udongo kuunda vyungu...

Basi akaona na vile alivyoshindwa kudadisi vimetokea wapi mfano jua, miti, yeye mwenyewe vitakuwa viliumbwa na nguvu flani yenye ubunifu kuliko.

Kwahiyo dini uliyonayo umeambukizwa tu, haimaanishi huyo unaemuabudu yupo, hapana.

Na ndio maana katika kipindi hiki cha sayansi dini hazijitokezi tena. Sayansi sio imani, ni ujuzi utokanao na kuthibitisha.
 
Walikuwa na ibada zao. Walichagua vitu ambavyo havikuwa vya kawaida kwenye jamii kama miti mikubwa, mawe, jua, nyota, mwezi, milima kuwa miungu yao. Ingawa wanaweza kuwa hawakuwa sahihi kwa mapokeo ya sasa lakini bado walikuwa na ibada zao. Nyingine zipo mpaka leo kulingana na makabila yao.
 
Huwa najiuliza kabla Wakoloni kwa maana ya Wazungu na Waarabu kutuletea dini wakitumia wafanyabiashara, wamishenari na wapelelezi, (traders, missionaries and explorers), wazee wetu huku Afrika waliabudu katika dini gani? Je kwakuwa dini za kigeni hazikuwepo ina maana watu wote walioishi nyakati hizo walienda motoni kwa kuabudu miti, mizimu na wanyama. Je ipi ni dhambi machoni pa Mungu, kutokwenda kanisani na msikitini au kutenda mabaya!
Waliabudu hizo hizo dini,

Ukiangalia Historia ya Ethiopia utaona zamani sana walikuwa ni wayahudi, baadae wakawa wakristo na baadae waisilamu, hio Nchi ina dini zote 3. Uisilamu upo Ethiopia kabla haujaenea kwa waarabu tofauti na wengi humu wanazo spread uongo bila Facts za kihistoria. Wazungu na waarabu walikuta Ukristo na Uisilamu huku Africa, wao walileta tu version zao za hizo dini ila dini mama wamezikuta.

Egpty, Ethiopia, na maeneo ya karibu na hapo kuna Dini za kale zilizokua zikiabudu miungu mbalimbali kama Anubis, Isis, Osiris,

Pia kuna miungu ya asili watu wa zamani walikua wakiabudu kama Mungu jua, Mungu mwezi, Mungu Venus, Mungu Bahari etc.
 
Na Uislamu pamoja na Quran vinatambuwa na kukiri Yesu yupo mbinguni na Allah na Muhammad amezikwa Madina.
Mbingu according to Uisilamu na Mbingu according to Ukristo ni vitu viwili tofauti,

Kwenye uisilamu Mbingu si pepo, hata sisi sasa hivi tupo mbinguni, kuna Mbingu 7 na universe yetu ni moja kati ya hizo Mbingu 7

Binadamu anapokufa pia haendi Ardhini, huo ni mwili wake ndio unaenda huko, Makazi ya Roho ni Barzak ambapo ya nasubiria siku ya mwisho kwa ajili ya hukumu.
 
Huwa najiuliza kabla Wakoloni kwa maana ya Wazungu na Waarabu kutuletea dini wakitumia wafanyabiashara, wamishenari na wapelelezi, (traders, missionaries and explorers), wazee wetu huku Afrika waliabudu katika dini gani? Je kwakuwa dini za kigeni hazikuwepo ina maana watu wote walioishi nyakati hizo walienda motoni kwa kuabudu miti, mizimu na wanyama. Je ipi ni dhambi machoni pa Mungu, kutokwenda kanisani na msikitini au kutenda mabaya!
Walimuabudu Mungu huyohuyo, isipokuwa kwa njia (dini/madhehebu) na mazingira (makanisa/misikiti/mahekalu) tofauti.
 
Huwa najiuliza kabla Wakoloni kwa maana ya Wazungu na Waarabu kutuletea dini wakitumia wafanyabiashara, wamishenari na wapelelezi, (traders, missionaries and explorers), wazee wetu huku Afrika waliabudu katika dini gani? Je kwakuwa dini za kigeni hazikuwepo ina maana watu wote walioishi nyakati hizo walienda motoni kwa kuabudu miti, mizimu na wanyama. Je ipi ni dhambi machoni pa Mungu, kutokwenda kanisani na msikitini au kutenda mabaya!
Hakuna dini mpya iliyoletwa Afrika, zimeletwa imani za kikristo.

Walikuta wazee Waislam na historia ipo wazi kwa hilo. Labda ujigfanye huelewi tu.
 
Tulikuwa na taratibu zetu za ibada tena zilikuwa nzuri sana...kwa wachaga walikuwa na vitabu vyenye herufi zinazofanana na Amaric.....ambazo zilipigwa marufuku.....maombi yalikuwa yanajibiwa papo kwa papo mfano ugonjwa...huonyeshwa dawa kwenye ndoto.....ukiomba mvua ikichelewa ni siku 3 tu na si zaidi.
 
Hakuna dini mpya iliyoletwa Afrika, zimeletwa imani za kikristo.

Walikuta wazee Waislam na historia ipo wazi kwa hilo. Labda ujigfanye huelewi tu.
Uislam wa kale ulikuwa wa UPENDO tofauti na huu wa sasa hata uchagani uislam ulikuwepo na ndio maana mpaka leo kanisa kwa kichaga ni msikiti.
 
Back
Top Bottom