Kabla hamjafuta somo la Uraia (Civics) naomba nijibiwe maswali haya

Kabla hamjafuta somo la Uraia (Civics) naomba nijibiwe maswali haya

JIBU SWALI
KILIMPINDUA NANI? au kimeleta MAPINDUZI GANI?
Hujaulizwa historia ya chama
Mapinduzi yaliyofanywa kwenye sekta zote huyaoni au unaleta ubishani tuu mkuu
Angazia sekta zote kijamii ,kiuchumi,kielimu,kisiasa,kiteknolojia na yote kwa yote na ndomaana miaka sitini na upuuzi bado kina tawala na kitaendelea kuwepo tuuh😂
 
Kwanini mwenge usikae tu makumbusho hadi umalize hela?Na swali la kwanza hata mimi sijaelewa jibu lako
Nilikua nakupa maana mkuu lakini ukitaka mapinduzi ghani iliuelewe nini maana ya chama cha mapinduzi
Zitazame sekta zote kiuchumi,kisiasa,kijamii n.k tangu 1977 till now😉
 
Kabla hamjafuta Civics nataka nijulishwe,
1. Chama Cha Mapinduzi kilimpindua nani?
2. Tanganyika tunafaidikaje na muungano?
3. Mwenge wa uhuru uko kwa ajili ya maslahi na faida ya nani? Na una faida gani kwa taifa? Kwanini usizimwe na kuhifadhiwa kwenye makumbusho ya Taifa?
1. Chama cha Mapinduzi ni muungano wa TANU na ASP. TANU ilimpindua Mkoloni Muingereza kwa upande wa Tanganyika, na ASP ilimpindua Mkoloni Mwarabu kwa upande wa Zanzibar.

2. Hilo swali sio sahihi. Swali sahihi ni Muungano una faida gani kwa waTanzania? Masuala ya Tanganyika inafaidikaje, au Zanzibar inafaidikaje hayana maana. Hatujaungana ili kuhesabu Tanganyika inafaidikaje na Zanzibar inafaidikaje. Kuhesabu hayo ni sawa na kutoungana.

Faida ya kwanza ya Muungano kwa Tanzania ni fahari ya uAfrika. Kwamba Tanzania ni mojawapo ya dola mbili pekee barani Afrika ambazo zimeundwa na waAfrika wenyewe. Nyingine ni Ethiopia. Dola zilizosalia Afrika zimeundwa na wakoloni.

Faida ya pili ni tumelinda na kudumisha udugu wa watu wa pande zote mbili za muungano.

Faida ya tatu ni tumepata himaya kubwa ambayo ni msingi wa fursa kubwa kiuchumi.

3. Mwenge wa Uhuru unahamasisha maendeleo. Kila mahali unapopita huwa unaambatana na uzinduzi wa miradi ya maendeleo. Hivyo basi unakuwa ni chachu kwa viongozi na watendaji wa maeneo husika kujituma wawe na miradi ya kuzinduliwa na mbio za mwenge.
 
Chama cha Mapinduzi ni muungano wa TANU na ASP. TANU ilimpindua Mkoloni Muingereza kwa upande wa Tanganyika, na ASP ilimpindua Mkoloni Mwarabu kwa upande wa Zanzibar
CCM ilizaliwa mwaka 1977 haikupindua chochote. Tanu haikuwahi kumpindua mkoloni, kasome vizuri historia.
Faida ya kwanza ya Muungano kwa Tanzania ni fahari ya uAfrika. Kwamba Tanzania ni mojawapo ya dola mbili pekee barani Afrika ambazo zimeundwa na waAfrika wenyewe. Nyingine ni Ethiopia. Dola zilizosalia Afrika zimeundwa na wakoloni.

Faida ya pili ni tumelinda na kudumisha udugu wa watu wa pande zote mbili za muungano.
Hizi kweli ni faida? Yaani hata ni aibu kuzitaja kwa kujigamba mbele ye watu.
Kenya inapata hasara gani kwa kuukosa muungano kama wetu? Hili swali la Kenya ni check and balance ya hizo unazoziita faida
 
Mwenge wa Uhuru unahamasisha maendeleo. Kila mahali unapopita huwa unaambatana na uzinduzi wa miradi ya maendeleo. Hivyo basi unakuwa ni chachu kwa viongozi na watendaji wa maeneo husika kujituma wawe na
Gharama za kuukimbiza mwenge ni kubwa sana ukilinganisha na thamani ya hiyo miradi. Rwanda hawana mwenge, wana maendeleo makubwa kuliko sisi. Chini ya CCM limezaliwa taifa la watu magoigoi, wavivu kufikiri, wasio na uwezo wa kuhoji, wapo tu kwa ajili ya kusifu na kuabudu ili wavimbishe matumbo yao
 
Mapinduzi yaliyofanywa kwenye sekta zote huyaoni au unaleta ubishani tuu mkuu
Angazia sekta zote kijamii ,kiuchumi,kielimu,kisiasa,kiteknolojia na yote kwa yote na ndomaana miaka sitini na upuuzi bado kina tawala na kitaendelea kuwepo tuuh😂
Haya unayoyasema unalinganisha na taifa gani kama benchmark? Ushakaa kijijini ukaona maisha yalivyo?
 
1: chama cha mapinduzi (CCM)tan ni chama cha ukombozi ndio muunganiko wa TANU kwa tanganyika na ASP kwa zanzibar

2:Tanganyika tunanufaika zaidi na muungano kiusaalma zaidi na nadhan ndolilikua lengo kuu la muasisi wa uo muungano kwa upande huu wa bara ukitoa madhumuni mengine

3: Mwenge =uhuru(9 december ) ,ni mojawapo ya vitu vinavopatikana kwenye nembo ya taifa hili ukitaka tuutoe mwenge maana yake tutoe na vitu vingine kwenye nembo ya taifa letu tukufu la TANZANIA

Alama zingine ni PEMBE ZA NDOVU,MWANAMKE NA MWANAUME,RANGI NYEUPE NA BULUU,RANGI NYEKUNDU,NGAO, ,MAJEMBE MAWILI pamoja na MKUKI.
Uraia ukifutwa Ili tukawe raia wa wapi au ndio kuuzwa kwenyewe?
 
CCM ilizaliwa mwaka 1977 haikupindua chochote. Tanu haikuwahi kumpindua mkoloni, kasome vizuri historia.
Wewe ndo inatakiwa usome vizuri jibu nililoandika. Naona hujalielewa.
Kenya inapata hasara gani kwa kuukosa muungano kama wetu? Hili swali la Kenya ni check and balance ya hizo unazoziita faida
Kenya wanaweza wakatuiga sisi. Sio lazima sisi tuwaige wao. Na pili unadhani ni kwanini Kenya ikalazimika kuvamia Somalia, au unadhani ni kwanini wakakubali kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki kutengeneza soko moja kubwa zaidi huku wakipiga debe uhuru wa kutembea na uhuru wa kumiliki ardhi uwepo kwenye Jumuiya yote?

Tafakuri kwa kina, weka kando kwanza chuki zako kwa Chama cha Mapinduzi.
 
1: chama cha mapinduzi (CCM)tan ni chama cha ukombozi ndio muunganiko wa TANU kwa tanganyika na ASP kwa zanzibar

2:Tanganyika tunanufaika zaidi na muungano kiusaalma zaidi na nadhan ndolilikua lengo kuu la muasisi wa uo muungano kwa upande huu wa bara ukitoa madhumuni mengine

3: Mwenge =uhuru(9 december ) ,ni mojawapo ya vitu vinavopatikana kwenye nembo ya taifa hili ukitaka tuutoe mwenge maana yake tutoe na vitu vingine kwenye nembo ya taifa letu tukufu la TANZANIA

Alama zingine ni PEMBE ZA NDOVU,MWANAMKE NA MWANAUME,RANGI NYEUPE NA BULUU,RANGI NYEKUNDU,NGAO, ,MAJEMBE MAWILI pamoja na MKUKI.
Umejibu vizuri sana
 
Back
Top Bottom