Kabla hujanunua godoro pitia hapa ujue lipi litakufaa

Mbona comfy sioni kwenye maoni yakoo au lenyewe halina kasoro yoyote?
Naomba utuchambulie kwa kina kuhusu magodoro ya comfy hata kwa machahe tu.πŸ™πŸ½
 
Unapatikana wapi nijaribu Hilo la ujazo hio maana kuhusu Chaga na karatasi sio Sahihi
 
Tatizo mnaouza vitu humu wengi mnauza vitu vya wizi...Kuna jamaa alikua anauza tairi nikataka nimuungishe anadai ofis ipo Vingunguti nikamuambia niletew tairi 4 Sinza saa 4 asubuhi akasema poa. Mpaka inafika saa 7 anasema yupo njiani. Baadae nikamuambia nakuja huko huko. Ile nafika Baracuda nishuke Vingunguti kazima simu mazima.
 
Ndugu katika kutaja watu nakushauri usipende kuweka kwa jumla

Binafsi biashara yangu ipo huru na imesajiriwa na sio kwamba inategemea humu tu wapo wanaofika physically hata jf hawaijui
Kiufupi
Binadamu wana tabia tofauti ila nikukaribishe ofisi zetu
 
Nitajuaje ujazo wa godoro nikifika pale dukani
Kujua kama sio mzoefu ni ngumu ila baadhi ya viwanda wamesaidia kuweka label zenye kuonyesha ujazo wa godoro
Mfano dodoma qfl density 24
Comfy density 23
Vita raha density 23
Vita supreme density 28
 
Nimeelewa halafu sijaelewa

Huo ujazo ni nini (kipimo) na nautambuaje au umeandikwa kwenye magodoro?
Nikuweke kwenye kundi la walioelewa pia nikuongezee uelewa kidogo kwa kukupa mfano wa soda zilivyo katika ujazo tofauti
Kwamba ipo soda ila ml 350 na nyingine kubwa ml 500 mpaka vile vidogo vilikuwa ml 250 wengi tuliziita bambucha

Sasa hata godoro nazo zina ujazo ukinunua lenye ujazo mdogo hata kudumu kwake hivyo hivyo ni muda mfupi
Ukilinganisha na ujazo mkubwa
Nadhani sasa umeelewa in fully
 
Godoro ni tanform Arusha pekee au Banco mwaka wa 15 huu lishabeba coaster za kutosha lakini kama jipya
Hapana sio pekee bali kuna vingi vya kuzingatia kwako boss huenda hata uzito wako sio mkubwa
Pia rate yako ya kulala sio kubwa
Ila zipo nyingi nzuri kama TAN foam na Banco
Kama
Dodoma
Comfy
Vita raha
Deluxe Arusha
 
Mbona comfy sioni kwenye maoni yakoo au lenyewe halina kasoro yoyote?
Naomba utuchambulie kwa kina kuhusu magodoro ya comfy hata kwa machahe tu.[emoji1431]
Comfy ni godoro nzuri boss na pia ni kiwanda cha zamani lenyewe ujazo wake ni 23 linawafaa sana chini ya kg 70 na kama zaidi ya hapo basi uchukue lenye unene mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…