Sema katika jamii ya wasukuma uke wenza ni nje nje na jambo la kawaida sana pamoja na Kwamba ni wakristo.
Sijui ni Kwanini ??
Tuseme kanda ya ziwa kote huko bara iko hivyo.
Nimekuja kujua hilo Mwaka Jana Sijui Mwaka juzi tu.
Mimi nilijua sababu ni wakristo ni mke mmoja kumbe thubutuuu yake !
Ukimuuliza msukuma yeyote randomly “ kwenu mmezaliwa wangapi ?
Atakuuliza kwanza ;
“ kwa mama tu au kwa baba “ ??
Maana yake kwa baba huwa ni zaidi ya mama mmoja.
Kwa hiyo wale wanawake mnaotegemea kuingia kwenye uhusiano na wanaume wa kisukuma kuweni na hiyo provision 👌👌👌
Na wanaume wa bara wakurya, wahaya n.k
Na uzoefu unaonesha mke ukiolewa ukijitia choyo na jeuri mma mkwe anamtafutia mwanae mwanamke mwingine wa kumpa furaha na utulivu,
Shoga yangu ukijakujua na watoto walishazaliwa siku nyingi.
Kaza roho.