Kabla ya Bagamoyo, Palikuwepo na mpango wa Bandari ya Mwambani, Tanga

Kabla ya Bagamoyo, Palikuwepo na mpango wa Bandari ya Mwambani, Tanga

Mradi wa Bagamoyo haukuwa na mpango wa shares za Serikali, walioenda ku-negotiate walipewa chao kisha mwekezaji akapewa kila kitu: Tittle deed 99 years, no land rent, no property tax
View attachment 1750319
Kama haya anayoyaongelea Bwa.Kakoko ni ya kweli basi huo Mkataba ni wa Ovyo

Ndugai kwenye hili la Bagamoyo kavuta mlungula
 
Wachina walialikwa ili mwalikaji apate chake, na alipata ndiyo maana aliyekwamisha anatukanwa kila aina ya mabaya, na bado, watu wake wataipata: Mungu atuhurumie
Mkuu Gama.

Naomba tuanze jambo.

Kwa sasa inaweza ikaonekana kwamba hatuna msaada na wala nguvu zozote za kuwazuia hawa wapuuzi, majizi wa nchi hii.

Tutafute njia za kupambana na hawa watu, tusikubali kamwe kuwaacha wakichafua nchi yetu.

Kwa kuanzia naomba tutafute mchango wa mawazo, njia za wananchi za kuwakomesha hawa majizi. Tukusanye maoni.

Na kila inapowezekana, tusiwaonee haya, tuwataje tu kwa majina yao na vyeo vyao wanavyoshikilia serikalini au kwingine kokote.

Naomba yeyote mwenye mchango wa mawazo tafadhali tuungane kupambana na hawa wahujumu.

Mwanzo ni sasa, kabla hawajaungana tena huko serikalini na kufanya kazi ya kuwasambaratisha kuwa ngumu.
 
..niliwahi kumsikia Rais Kikwete akisema kwamba mradi wa bandari ya bagamoyo uliletwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kufanya ziara nchini China.

..tunatakiwa tujiulize kama tunahitaji bandari ya bagamoyo au la. kama tunaihitaji tuangalie option ya kujenga wenyewe, au kujenga kwa ubia na muwekezaji mwenye masharti mazuri.

Tujiulize kweli kweli. Mkataba, mapendekezo yote yawekwe wazi.
 
..niliwahi kumsikia Rais Kikwete akisema kwamba mradi wa bandari ya bagamoyo uliletwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kufanya ziara nchini China.

..tunatakiwa tujiulize kama tunahitaji bandari ya bagamoyo au la. kama tunaihitaji tuangalie option ya kujenga wenyewe, au kujenga kwa ubia na muwekezaji mwenye masharti mazuri.
Mkuu JokaKuu,

Uhitaji wa bandari kama hiyo upo sana, lakini haya yanayosikika sasa hivi yanatia wasiwasi sana.

Inakuwaje mara tu baada ya kuondoka aliyewanyang'anya wapigaji, hata mwezi haujapita kukawa na kelele nyingi kiasi hiki kwenye hii miradi miwili ya Bandari na ule wa umeme?

Hii inaonyesha wazi kwamba walaji hawana subira hata kidogo?

Hii ni hatari sana, hasa kwa huyu mama, sijui kama na yeye yumo kwenye kundi hilo, au yupo tayari aunganishwe, vinginevyo naona hali yake ikiwa ngumu sana kama asipokaza shingo kikwelikweli!

Hawa watu hawana aibu kabisa, wanajitoa waziwazi kusukuma mipango yao iende mbele!
 
..Je, mradi wa bandari ya bagamoyo ni mzuri au mbaya?

..kama ni mradi mzuri, je tujenge wenyewe, au tushiriane wa wawekezaji?

..Nini hatima ya bandari ya Dsm ikiwa tutaamua kujenga bandari Bagamoyo?
Na mimi nikuulize swali, Mwambani ina ubaya gani, kwa nini iwe Bagamoyo, ambayo ipo jirani sana na Dar es Salaam.

Pale Kenya wanayo ya kwao Lamu imekosa mwekezaji, pamoja na kuipigia promo nyingi sana.
Wameanza ujenzi wenyewe, ghati moja tayari, na ujenzi unaendelea taratibu. Kwa hiyo hata sisi tunaweza kuanza wenyewe taratibu haina haja ya kusubiri mwekezaji.
Kama wao, hata sisi tukiamua kujenga wenyewe, usitegemee kuiona bandari yenye michoro ile iliyokuwa ikionyeshwa hapa mara kwa mara ndani ya miaka ishirini!

Lakini elewa, hawa wanaousukuma mradi huu kwa haraka ni wapigaji, wanataka wapate chao chapchap.
 
CONCESSION KWA VASCO DAGAMA YA KUMTOA MWANAE KUTOKA KWA WACHINA BAADA YA KUKAMATWA NA NGADA!!!
Tumeiuza nchi kwa wachina sababu ya toto lililopaswa kuuawa!!! Tena toto lenyewe tukalipa na ubunge!?! Kwa maneno ya maalim Seif "huu ni uha.ni.thi."
 
Bagamoyo Kwanza.
hatuwezi kutegemea bandari ya dar miaka yote dunia inakua.
 
Tunaweza kuwa na Bandari tatu kubwa. Maslahi ya Watanzania yawe mbele , kwanza.

Mikataba yote tuione.

Tunaweza kuwa transit ya madawa ya kulenywa kama hatuna usimamizi.

Watoto wetu wakaathirika vibaya.
 
Mkuu JokaKuu,

Uhitaji wa bandari kama hiyo upo sana, lakini haya yanayosikika sasa hivi yanatia wasiwasi sana.

Inakuwaje mara tu baada ya kuondoka aliyewanyang'anya wapigaji, hata mwezi haujapita kukawa na kelele nyingi kiasi hiki kwenye hii miradi miwili ya Bandari na ule wa umeme?

Hii inaonyesha wazi kwamba walaji hawana subira hata kidogo?

Hii ni hatari sana, hasa kwa huyu mama, sijui kama na yeye yumo kwenye kundi hilo, au yupo tayari aunganishwe, vinginevyo naona hali yake ikiwa ngumu sana kama asipokaza shingo kikwelikweli!

Hawa watu hawana aibu kabisa, wanajitoa waziwazi kusukuma mipango yao iende mbele!

Unajua tuna viongozi wa ajabu sana. Hawajitambui.

Hii nchi itakuwa chini ya China, US, Europe baada ya miaka 200. Weusi wote wataķuwa wameuwawa.

Kama walivyofanya kwa Red Indians in USA, Australian blacks, and South America.

Ni nchi yenye rasilimali nyingi sana iliyobaki huru. Ila uzalendo umekwisha.
 
Unadhani hawajitambui; wanajitambua sana. Tatizo lao ni ubinafsi, ulafi na kusahau maslahi ya wengi.

Hili ndilo tatizo.
 
Tunafanyaje?
Tuwafichue na tuwaaibishe.

Tukiwa na ujasiri zaidi, hata mahakamani tuwafikishe panapokuwepo ushahidi wa kutosha.

Kosa litakuwa ni kuwaacha tu na kuendelea kuwachekea, na wakati mwingine hadi kuwasifu kabisa kwa ujasiri wao wa kufanya ufisadi!

Huwezi kucheka na nyani anayetafuna mahindi yako.
 
Hivi kuna ugumu wowote mkataba huu wa bandari ya Bagamoyo kuwekwa hadharani ili Watanzania wenye nchi yao wajue kila kilichomo ndani yake? Kuna nini ndani ambacho kikiwekwa hadharani kitafanya nchi iwe hatarini? Ni nini hicho, ambacho hakitakiwi kujulikana hadharani Bali kiwe sirini daima.?
 
Mwanzo ni sasa, kabla hawajaungana tena huko serikalini na kufanya kazi ya kuwasambaratisha kuwa ngumu
Tuanze na kumuondoa mnafiki "KAZI" kwenye kiti cha mbele maana yeye amejitanabaisha
 
Hivi kuna ugumu wowote mkataba huu wa bandari ya Bagamoyo kuwekwa hadharani ili Watanzania wenye nchi yao wajue kila kilichomo ndani yake? Kuna nini ndani ambacho kikiwekwa hadharani kitafanya nchi iwe hatarini? Ni nini hicho, ambacho hakitakiwi kujulikana hadharani Bali kiwe sirini daima.?
Beneficiaries watakutoa roho🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓

Fikiria kama mtu aliitoa mbadala wa mwwnaye aliyekamatwa na NGADA ambapo hukumu yake ingekuwa kukatwa kichwa🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️⁉️

Mengine semeni tuuuuuuuuuuuuuu

Chato watatukanwa hadi vitukuuu
 
Tuwafichue na tuwaaibishe.

Tukiwa na ujasiri zaidi, hata mahakamani tuwafikishe panapokuwepo ushahidi wa kutosha.

Kosa litakuwa ni kuwaacha tu na kuendelea kuwachekea, na wakati mwingine hadi kuwasifu kabisa kwa ujasiri wao wa kufanya ufisadi!

Huwezi kucheka na nyani anayetafuna mahindi yako.
Baada ya mwendazake kwenda zake sasa nyani wana mamlaka juu ya mahindi yetu
 
..Nini hatima ya bandari ya Dsm ikiwa tutaamua kujenga bandari Bagamoyo
Moja ya utashi wa mchina ni nchi kutoendeleza bandari nyingine yoyote ndani ya nchi huku bandari ya bagamoyo ikifanya kazi bila kodi yoyote hivyo bila revenue yoyote kwa nchi
 
Moja ya utashi wa mchina ni nchi kutoendeleza bandari nyingine yoyote ndani ya nchi huku bandari ya bagamoyo ikifanya kazi bila kodi yoyote hivyo bila revenue yoyote kwa nchi
Hata kama mapendekezo ya mkataba hatujayaona na kuyasoma.

Hiki ulichoandika ni zaidi ya uongo.

Inaonyesha hata sheria za kodi kwa mujibu wa nchi yako huzijui.
 
Back
Top Bottom