Kabla ya Bagamoyo, Palikuwepo na mpango wa Bandari ya Mwambani, Tanga

Kabla ya Bagamoyo, Palikuwepo na mpango wa Bandari ya Mwambani, Tanga

"Moja ya utashi wa mchina ni nchi kutoendeleza bandari nyingine yoyote ndani ya nchi huku bandari ya bagamoyo ikifanya kazi bila kodi yoyote hivyo bila revenue yoyote kwa nchi."

KAMA HIVYO NDIVYO TUNABISHANA NINI HAPA. PIGA CHINI HAO CHINESE NA WOTE WANAOWAPIGANIA.
 
CONCESSION KWA VASCO DAGAMA YA KUMTOA MWANAE KUTOKA KWA WACHINA BAADA YA KUKAMATWA NA NGADA!!!
Hizi story ukute umekaa kwenye kikochi kwa mume wa dadako unatype tu ndi ndi ndi na kitecno chako na ukute muda huu shemeji yako kakupita hapo sebuleni. Yaan wabongo kwa kutunga story sijui shida nini. Kama huna kazi sema watu wakutafutie uache kuchukia waliokuzidi kipato.
 
Kwani mmekatazwa kujenga mwambani Tanga, haya nendeni mkajenge kwani shida iko wapi?

Mnaizungumzia bandari ya bagamoyo as if lengo ni bandari tu, wakati plan ya pale ni kuweka EPZ, ikiwemo mamia ya viwanda.

Lengo la bandari ya Bagamoyo kuwa karibu na Jiji kubwa linalochangia pato la Taifa kwa more than 70% hamuijui? —Bagamoyo ni extension ya jiji la Dar, na mji wa dar unakua kuelekea uelekeo huo!

Hata Magufuli ukimsikiliza kwenye video hii hapa chini anausifu mradi wa bandari ya bagamoyo na anamsifu Kikwete kwa kuuanzisha. Sasa Msgufuli kwa bahati mbaya alikuwa kigeugeu ni mtu wa ndimi mbili, baadae aligeuka!


View attachment 1752197
Hii sio njia bora ya kujadiliana jambo.

Ni kama sasa unalazimisha watu, au unazila na kuwasusia hao wenye mawazo tofauti na yako.

Hakuna asiyejua umuhimu wa Bandari na miradi yote hiyo ya viwanda, n.k..

Lakini, kwani kuuliza ni nini kiliitokea bandari ya Mwambani ni kosa?

Au Mwambani haiwezi kubeba yote yanayotarajiwa kuwa Bagamoyo?

Hilo swala la ukaribu wa Dar sio hoja muhimu kama unavyoichukulia hivyo.

Kama uchumi wa Dar unabeba sehemu kubwa ya uchumi wa nchi nzima 70%, kwa nini sehemu nyingine nazo zisipewe nafasi ya kuchangia angalao kwa 5%?
 
Kwa vile Magufuli alifanya yote yasiyokibalika bila kukemewa na chama chake wala kuzomewa na wananchi, sasa kuna watu watapenda kuiga na hasa ndani ya CCM. Kwa sababu wameona inawezekana kufanya maovu bila kichukuliwa hatua.
Hapa ndipo tunapopishana kati yetu.

Nimeeleza vizuri tu, kwa tabia alizokuwa nazo Magufuli, hakuna aliyekuwa tayari kuthubutu "kuhoji wala kuzomea" iwe kwenye chama chake au kwingine kokote. Si uliona yaliyompata Lissu?
Hii ndiyo tabia/sifa iliyomtofautisha Magufuli na mtu mwingine yeyote (ni wachache sana ndani ya nchi hii wenye aina hiyo ya tabia).

Kwa hiyo haiwezekani kamwe kumlinganisha Kikwete, Mkapa, Mwinyi na hulka ya kipekee aliyokuwa nayo Magufuli.

Hakuna mtu anayeweza "kuiga" kiasi kile cha tabia na kudiriki kuyafanya aliyofanya Magufuli bila ya roho kumsuta kwa vile sio tabia yake asilia.
 
Hapa ni porojo tuone mikataba na terms na conditions zake tujue nani anatudanganya nani mkweli la sivyo ni ushabiki usio na maana
 
..fedha tulizotapanya kujenga dodoma, na kununua midege toka kwa mabeberu, zingetumika vizuri kama zingeelekezwa kujenga bandari mpya ya Bagamoyo. Tusingelazimika kukubali masharti mabaya ya kinyonyaji toka kwa Wachina.

Cc Nguruvi3
Lamu, wenzetu wametembeza bakuri ikashindikana, hakuna anayeweka hata senti tano.

Wameamua wao wajenge ghat tatu za mwanzo kati ya 32 za bandari hiyo. Mategemeo yao ni kwamba huenda huko mbeleni wawekezaji wakavutiwa kuwekeza.
Wao nguvu yao kubwa ilikuwa kuwahudumia Sudan Kusini na Ethiopia, lakini hawa tayari wanahudumiwa vizuri na bandari nyingine.

Kwa hiyo sasa wanajaribu kupanua wigo, kuifanya Lamu iwe ya mameli makubwa yanayopokeza mizigo kwa vimeli vidogo na kutusambazia sisi.

Hili nalo waombe sana sisi tuendelee kulala usingizi, kwa maana Mwambani au Bagamoyo, zote zinauwezo wa kuwa na hadhi ya aina hiyo kiurahisi zaidi, tena zikiwa sehemu nzuri zaidi ya kusambaza hivyo vimizigo vidogo kuliko ilipo Lamu.
 
Bila shaka. Bandari ya Tanga ni bandari ya asili kabisa hivyo hatutakuwa na kazi kubwa ya kuchimba kina cha bandari. Bandari ya Bagamoyo tutapata kazi kubwa ya kuchimba kina cha bandari hivyo kuingia gharama zisizo na msingi.
Turudi kwenye bandari ya Tanga tufanye kweli
 
..niliwahi kumsikia Rais Kikwete akisema kwamba mradi wa bandari ya bagamoyo uliletwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kufanya ziara nchini China.

..tunatakiwa tujiulize kama tunahitaji bandari ya bagamoyo au la. kama tunaihitaji tuangalie option ya kujenga wenyewe, au kujenga kwa ubia na muwekezaji mwenye masharti mazuri.
Hatuhitaji bandari ya Bagamoyo kabisa. Tena hatutaki kuisikia maana inavyoonekana mapema hivi ni dili la watu wachache tu. Tunaihitaji sana bandari ya Tanga ili ihudumie kwa ushindani kamili kanda ya kaskazini ya na kutoa ushindani wa kweli kwa bandari ya Mombasa
 
kwani huo uwekezaji hauwezi kuhamia Tanga ?
Haiwezekani Bandari ya Tanga ni ya serikali
Bila shaka. Bandari ya Tanga ni bandari ya asili kabisa hivyo hatutakuwa na kazi kubwa ya kuchimba kina cha bandari. Bandari ya Bagamoyo tutapata kazi kubwa ya kuchimba kina cha bandari hivyo kuingia gharama zisizo na msingi.
Turudi kwenye bandari ya Tanga tufanye kweli
Bandari ya Tanga ni ya serikali sio ya uwekezaji
Hatuhitaji bandari ya Bagamoyo kabisa. Tena hatutaki kuisikia maana inavyoonekana mapema hivi ni dili la watu wachache tu. Tunaihitaji sana bandari ya Tanga ili ihudumie kwa ushindani kamili kanda ya kaskazini ya na kutoa ushindani wa kweli kwa bandari ya Mombasa
Naskitika kusema mm na ww hatuna mamlaka juu ya maamuzi hayo, hiyo ni mamlaka ya viongozi.., mamlaka na haki tulionayo ni ya civil rights tu.
 
Hiyo mwambani port inaenda sambamba na bombo la mafuta na pia ilitakiwa ijengwe sgr via Moshi Arusha to Musoma sasa mwendazake alizingua
 
Bagamoyo imekuwa Bagamoyo, kisa, Kikwete alivunja ahadi ya ujenzi wa bandari Mwambani, Tanga.

Sasa makelele yanasikika kila sehemu kuhusu Bagamoyo, na hakuna anayekumbuka Mwambani ilikuwaje?

Eleza, Mwambani haikuwa na vigezo ilivyonavyo Bagamoyo?

Ile bandari itapitisha bidhaa za Uganda, Rwanda, hadi DRC, kama inavyoweza kufanya Bagamoyo, tena kwa umbali wa karibu zaidi.

Tuiache Dar ihudumu bila mwingiliano. Jenga Mwambani, achana na Bagamoyo.
Aiseeee !
 
Back
Top Bottom