KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
- Thread starter
- #61
Yule kijana wa Tunisia aliuawa kweli? Kumbukumbu yangu inanikatalia kuwa ilikuwa hivyo, ila alichofanyiwa ni kweli ndicho kilichokuwa chachu ya yaliyotokea.Watanzania sijui tuna roho za namna gani tofauti na nchi nyingi duniani. Angalia waarabu walivyofanya kijana mmoja tu tena mmachinga aliuawa Tunisia, nchi zote za kiarabu kuanzia Algeria hadi Syria zilisisimka na kuanzisha vita dhidi ya watawala wanyanyasaji. Hapa kwetu kitendo cha Tundu Lissu kupigwa risasi kilitosha kuamsha vuguvugu la kudai haki lakini haikuwa hivyo. Halikadhalika uchaguzi mkuu uliopita usingewaacha baadhi ya viongozi wetu wa sasa salama.
Binafsi huwa sielewi ni malezi yetu au ni wingi wa makabila madogo madogo tuliyonayo yanayotufanya kukosa umoja na ushirikiano! Watanzania wengi hushangilia sana kusikia mwenzao mmoja kafukuzwa kazi hata bila sababu ya msingi na kufuata sheria. Tumejaa ubinafsi na kila mmoja anajijali binafsi na familia yake. Cho chote kinachomsibu jirani hakimuhusu na pengine hufurahia. Akionyesha kusikitika ni kwa unafiki tu.
Sasa ili kijinasua hapa tulipo kelele hazitasaidia sana. Kwanza kabisa hizo kelele hazitakuwepo zaidi ya kutoka kwa wapinzani wachache kama Mbowe na Lissu. Lakini pili kwa sababu ya propaganda za serikali dhidi ya hao wachache. Serikali itatumia dola kukandamiza kila aina ya kelele kama ilivyo sasa.
Tunachotakiwa kufanya ni kuyaomba mataifa makubwa kiuchumi na mashirika ya kimataifa kutusaidia. Tuliopo nchini tuendelee kukusanya ushahidi usioshaka namna ambavyo uhuru na haki zinavyogandamizwa. Waliopo nje ya nchi waendeleze harakati za kuelimisha kupitia vyombo vya habari na forums mbalimbali.
Chachu yetu bado mkuu. Kila kitu na wakati wake
Hata hivyo ninakubaliana kwa mengi uliyoandika kutuhusu tabia zetu waTanzania, lakini nina imani kwamba ni 'cheche' moja tu inayohitajika kuuwasha moto.
Hata mimi, kama wewe, nilitarajia kwamba hii cheche ingetokea wakati wa Magufuli kutokana na mengi yaliyotokea yaliyostahiri kuianzisha hiyo cheche, lakini haikuwa hivyo.
Mimi ninazo nadharia tofauti na zako kwa nini hiyo cheche haikutokea, lakini haina maana kwamba haitaweza kutokea kamwe wakati mwingine wowote hali ikiendelea kuwa mbaya.
Mimi bado nasisitiza mabadiliko yatokane na sisi wenyewe bila ya kuwategemea kwa kiasi kikubwa hao wa mataifa ya nje. Hawa kwa vyovyote hawawezi kutuletea mabadiliko yoyote ya maana, hata kama tukiamua kujiuza kwao kwa bei yoyote ile.Hivi uliwasikia jamaa wa Umoja wa Ulaya walivyoeleza msimamo wao juu yetu hivi karibuni?
Huko nje hakuna mategemeo yoyote mkuu, tutasubiri sana na hakuna lolote linaloweza kutokea bila ya juhudi zetu sisi wenyewe.
Ninachokubaliana nawe moja kwa moja, na mara nyingi nimekuwa nikiwasihi CHADEMA wakifanye kwa makini kubwa, ni kuweka kumbukumbu nzuri zenye ushahidi wote juu ya matukio yote yanatofanyika nchini. Kumbukumbu hizi ni muhimu sana kama ushahidi wakati zikihitajika huko mbele ya safari katika juhudi za kujikomboa kwa wakandamizaji, iwe CCM au kiongozi wao.
Ndiyo, kwa waTanzania waliopo nje, wao pia wana mchango maalum katika kuendeleza mapambano huko waliko.
Mwisho: Kazi kubwa waliyonayo vyama vya upinzani (CHADEMA) kwa sasa hivi, ni kutokata tamaa, bali waongeze juhudi kufanya kazi na wananchi kwa karibu zaidi ili wapate kuaminiwa nao kwamba wao ni tofauti na CCM. Kwamba, maslahi ya nchi hii hayashikiliwi na chama kimoja cha siasa.
Wananchi wanatakiwa wasikie na waamini hivyo. Ni kazi ngumu, lakini hakuna njia za mkato au mbadala wa kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.
Wakimudu kuifanya vyema,utaona cheche zinaibuka kila sehemu ya nchi toka kwa wananchi wenyewe.