Kama ambavyo uwezo na maajabu ya Mungu yamejidhihirisha katika tukio la Lissu kupigwa risasi na yote yaliyofuata baada ya hapo mpaka anakuja kugombea uraisi, ndivyo ambavyo uwezo na Mungu utajidhirisha kwa wale wote wanaotuhumiwa kuhujumu huu uchaguzi na hii itakuwa ni ndani ya miaka hii mitano.
Hint: Mungu ataonyesha kuwa yeye ndio mpangaji na mwamuzi wa kila kitu na kwamba kisicho riziki hakiliki na zaidi riziki ya mtu haipotei.
Kuna wakati unakuja tutaanza kuwahurumia hawa watu na wakati huo huo Mungu atakuwa ametoa soma kwa dunia nzima kupitia Taifa letu.
Tukumbuke pia Mungu huwa na makusudi kwa kila jambo -- huruhusu mambo au matukio fulani yatokee ili aje adhihirishe utukufu wake.
Hifadhi hii thread kwa ajili ya kuja kufanya reference wakati utapofika/matukio yakianza kujitokeza.
Time will tell.
Kule Zanzibar naamini litatokea jambo kutokana dhulma kubwa iliyofanyika kwa sababu ya kumnyima maskini haki yake na kumpa Tajiri .
Machozi ya wazanzibari mayatima na wajane yamekua mengi sana kwa kweli.
Zanzibar kuna watu hata wakilia wanaonekana kama kungunguru tu wasio na thamani mbele ya Watu wa daraja la kwanza wa CCM.
Naamini Wazanzibari hawaachi kusoma Albadiri usiku na mchana ili Kodi zetu zikiliwa na mwizi wa kura Basi iwe laana kwake.
Wanaiba kura halafu wanatudhihaki na kujigamba.
Tanzania Bara napo inabidi wapinzani kwanza watubu mana wengi hata dini hawaijui . Wapinzani wengi wa Bara hawana tofauti na CCM kwa Tabia. Watubu kwanza.
Mbowe atubu na kumrudia Mungu.
Mdee atubu.
Sugu atubu.
Baada ya toba warudi kwenye maombi ya kuomba haki,Uhuru na maendeleo ya watu wote.
Zipo Zaburi maalumu za kuomba ili Mungu alipe kisasi kwa wakati wake ili atukuzwe yeye pekee mana vyote duniani ni vyake.
Kwa Wakristo na waislam wanaoamini katika Mungu muumbaji na mfalme wa wafalme basi wasiache kumlilia Mungu kwa udhalimu uliofanywa kwenye uchaguzi wa wabunge na ule wa Serikali za Mitaa na madiwani .
Vitisho vya serikali na vyombo vyake vya dola vilikua ni vikubwa sana.
Yani mpaka neno Haki lilionekana kulitaja kwenye nyumba za ibada ni usaliti . Mana Mchungaji au Shekhe akijisahau tu akataja neno haki alionekana Mpinzani na adui mkubwa wa nchi .
Mungu tusaidie nchi yetu isije ikafanya uchaguzi kama huu tena na walioufanya uwe uchaguzi wa machungu na kuacha hofu na vifo na majeruhi wapate laana za damu zilizomwagika mpaka vizazi vyao vya pili na vya tatu.