Uchaguzi 2020 Kabla ya hii miaka mitano haijaisha, uwezo wa Mungu utakuwa umejidhirisha kwa wanaotuhumiwa kuhujumu uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Kama ambavyo uwezo na maajabu ya Mungu yamejidhihirisha katika tukio la Lissu kupigwa risasi na yote yaliyofuata baada ya hapo mpaka anakuja kugombea uraisi, ndivyo ambavyo uwezo na Mungu utajidhirisha kwa wale wote wanaotuhumiwa kuhujumu huu uchaguzi na hii itakuwa ni ndani ya miaka hii mitano.

Hint: Mungu ataonyesha kuwa yeye ndio mpangaji na mwamuzi wa kila kitu na kwamba kisicho riziki hakiliki na zaidi riziki ya mtu haipotei.

Kuna wakati unakuja tutaanza kuwahurumia hawa watu na wakati huo huo Mungu atakuwa ametoa soma kwa dunia nzima kupitia Taifa letu.

Tukumbuke pia Mungu huwa na makusudi kwa kila jambo -- huruhusu mambo au matukio fulani yatokee ili aje adhihirishe utukufu wake.

Hifadhi hii thread kwa ajili ya kuja kufanya reference wakati utapofika/matukio yakianza kujitokeza.

Time will tell.
Hoja ishabadilika hiyo kutoka kwenye uchaguzi na kuchukua mamlaka.
 
Niliuona huu uzi nikaupita tu. Mara nyingine kujibizana sana hakuna tija.

Ila kwa kuwa umeniita kwa mualiko maalum, nitachangia.

Kumtegemea Mungu - kama kweli tunaongelea Mungu, na si "figure of speech" tu- atusaidie kuwapatiliza waliohujumu uchaguzi, ni kuwawezesha hao waliohujumu uchaguzi waendelee kuhujumu uchaguzi.

Hivi huyo Mungu alikuwa wapi asizuie hujuma hizi? Alisinzia kazini? Aliishiwa betri? Alienda likizo? Alikuwa kwenye lockdown ya Covid?

Hii mentality ya kumtegemea Mungu hatuoni kwamba inatudumaza?

Yani pale watu wanapotakiwa kufanya harakati, kufungua kesi, kupigana, wanabaki kusema "hewala, Mungu atalipa".

Waliohujumu uchaguzi wakisikia hivyo wanafurahi sana. Wanajua hakuna kitakachotokea, huyo Mungu hayupo.

Angekuwepo Mungu wa haki, wasingeweza kuhujumu uchaguzi in the first place.

Tuache kumlundikia majukumu yetu Mungu ambaye hayupo.

Kama unataka kuleta mabadiliko, fanya kazi mwenyewe, acha kumsingizia na kumtegea Mungu.

Hakuna aliyeweza kuthibitisha Mungu yupo.
Yesu wangu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
We jamaa !
 
Tarehe ngapi, mwezi wa ngapi mwaka gani? Tuiweke kwenye kalenda na kuhakiki maneno yako.

Akinitokea nitamuuliza kwa nini anajifichajificha mpaka watu wanapigana vita za kidini kuuana kwa kubishana habari za Mungu?

Hujanijibu.

Hivi huyo Mungu alikuwa wapi asizuie hujuma hizi? Alisinzia kazini? Aliishiwa betri? Alienda likizo? Alikuwa kwenye lockdown ya Covid?
Mungu wangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Imebidi nicheke
 
Kama ambavyo uwezo na maajabu ya Mungu yamejidhihirisha katika tukio la Lissu kupigwa risasi na yote yaliyofuata baada ya hapo mpaka anakuja kugombea uraisi, ndivyo ambavyo uwezo na Mungu utajidhirisha kwa wale wote wanaotuhumiwa kuhujumu huu uchaguzi na hii itakuwa ni ndani ya miaka hii mitano.

Hint: Mungu ataonyesha kuwa yeye ndio mpangaji na mwamuzi wa kila kitu na kwamba kisicho riziki hakiliki na zaidi riziki ya mtu haipotei.

Kuna wakati unakuja tutaanza kuwahurumia hawa watu na wakati huo huo Mungu atakuwa ametoa soma kwa dunia nzima kupitia Taifa letu.

Tukumbuke pia Mungu huwa na makusudi kwa kila jambo -- huruhusu mambo au matukio fulani yatokee ili aje adhihirishe utukufu wake.

Hifadhi hii thread kwa ajili ya kuja kufanya reference wakati utapofika/matukio yakianza kujitokeza.

Time will tell.
Kule Zanzibar naamini litatokea jambo kutokana dhulma kubwa iliyofanyika kwa sababu ya kumnyima maskini haki yake na kumpa Tajiri .
Machozi ya wazanzibari mayatima na wajane yamekua mengi sana kwa kweli.
Zanzibar kuna watu hata wakilia wanaonekana kama kungunguru tu wasio na thamani mbele ya Watu wa daraja la kwanza wa CCM.

Naamini Wazanzibari hawaachi kusoma Albadiri usiku na mchana ili Kodi zetu zikiliwa na mwizi wa kura Basi iwe laana kwake.
Wanaiba kura halafu wanatudhihaki na kujigamba.

Tanzania Bara napo inabidi wapinzani kwanza watubu mana wengi hata dini hawaijui . Wapinzani wengi wa Bara hawana tofauti na CCM kwa Tabia. Watubu kwanza.
Mbowe atubu na kumrudia Mungu.
Mdee atubu.
Sugu atubu.
Baada ya toba warudi kwenye maombi ya kuomba haki,Uhuru na maendeleo ya watu wote.
Zipo Zaburi maalumu za kuomba ili Mungu alipe kisasi kwa wakati wake ili atukuzwe yeye pekee mana vyote duniani ni vyake.

Kwa Wakristo na waislam wanaoamini katika Mungu muumbaji na mfalme wa wafalme basi wasiache kumlilia Mungu kwa udhalimu uliofanywa kwenye uchaguzi wa wabunge na ule wa Serikali za Mitaa na madiwani .

Vitisho vya serikali na vyombo vyake vya dola vilikua ni vikubwa sana.
Yani mpaka neno Haki lilionekana kulitaja kwenye nyumba za ibada ni usaliti . Mana Mchungaji au Shekhe akijisahau tu akataja neno haki alionekana Mpinzani na adui mkubwa wa nchi .
Mungu tusaidie nchi yetu isije ikafanya uchaguzi kama huu tena na walioufanya uwe uchaguzi wa machungu na kuacha hofu na vifo na majeruhi wapate laana za damu zilizomwagika mpaka vizazi vyao vya pili na vya tatu.
 
Manase Adam kutusha
 
Tarehe ngapi, mwezi wa ngapi mwaka gani? Tuiweke kwenye kalenda na kuhakiki maneno yako.

Akinitokea nitamuuliza kwa nini anajifichajificha mpaka watu wanapigana vita za kidini kuuana kwa kubishana habari za Mungu?

Hujanijibu.

Hivi huyo Mungu alikuwa wapi asizuie hujuma hizi? Alisinzia kazini? Aliishiwa betri? Alienda likizo? Alikuwa kwenye lockdown ya Covid?
Kwanza Mungu ni mkuu mno.
Mungu ana mambo Mengi sana.
Mungu ana viumbe wengi kwa matrilion na matrilioni.
Binadam alishaasi na kujichagulia njia zake mwenyewe.
Ni sawa na chakula kilichochacha hata kikiingia mjusi au mende hakimuumi mpishi .
Binadam wakimwacha Mungu hua Mungu anawaacha waumie mpaka siku watakapo mkumbuka na kutubu.
Mungu ni mtakatifu sana hivyo ni lazima binadam aache madhambi ili akubalike.

Lakini hata hivyo kila jambo Mungu analiruhurmsu kwa sababu zake Mwenyewe.

Mungu yupo hilo halina Ubishi. Ukimjua Mungu na kumwelezea kinagaubaga kama vile jirani yako basi huyo sio Mungu.
Ili awe Mungu ni lazima awe mtata.
Mungu ni Mtata.
 
Hiki kizazi cha umri wa miaka 35 mpaka 60 ni kizazi kilichokua kimeiba sana mitihani Mashuleni na vyuoni. Hivyo kinadhihirisha uhalisia wake.
 
Kwanza Mungu ni mkuu mno.
Mungu ana mambo Mengi sana.
Mungu ana viumbe wengi kwa matrilion na matrilioni.
Binadam alishaasi na kujichagulia njia zake mwenyewe.
Ni sawa na chakula kilichochacha hata kikiingia mjusi au mende hakimuumi mpishi .
Binadam wakimwacha Mungu hua Mungu anawaacha waumie mpaka siku watakapo mkumbuka na kutubu.
Mungu ni mtakatifu sana hivyo ni lazima binadam aache madhambi ili akubalike.

Lakini hata hivyo kila jambo Mungu analiruhurmsu kwa sababu zake Mwenyewe.

Mungu yupo hilo halina Ubishi. Ukimjua Mungu na kumwelezea kinagaubaga kama vile jirani yako basi huyo sio Mungu.
Ili awe Mungu ni lazima awe mtata.
Mungu ni Mtata.
Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Kama ambavyo uwezo na maajabu ya Mungu yamejidhihirisha katika tukio la Lissu kupigwa risasi na yote yaliyofuata baada ya hapo mpaka anakuja kugombea uraisi, ndivyo ambavyo uwezo na Mungu utajidhirisha kwa wale wote wanaotuhumiwa kuhujumu huu uchaguzi na hii itakuwa ni ndani ya miaka hii mitano.

Hint: Mungu ataonyesha kuwa yeye ndio mpangaji na mwamuzi wa kila kitu na kwamba kisicho riziki hakiliki na zaidi riziki ya mtu haipotei.

Kuna wakati unakuja tutaanza kuwahurumia hawa watu na wakati huo huo Mungu atakuwa ametoa soma kwa dunia nzima kupitia Taifa letu.

Tukumbuke pia Mungu huwa na makusudi kwa kila jambo -- huruhusu mambo au matukio fulani yatokee ili aje adhihirishe utukufu wake.

Hifadhi hii thread kwa ajili ya kuja kufanya reference wakati utapofika/matukio yakianza kujitokeza.

Time will tell.
Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu. Daima Mungu yuko upande wa Watanzania wengi walioichagua CCM kwa kimbunga. Utaumia sana na kusubiri sana hayo mabaya unayoyaombea taifa letu hili linalopendwa sana na Mungu. Mungu ameagiza tuheshimu mamlaka zilizopo
 
Ukiona kitu kimetengenezwa kwa ustadi mkubwa.
Kina mifumo inayotegemeana na haijichanganyi changanyi ujue kuna fundi wake.

Mungu ni yule aliyeumba hivi vitu vya asili akiwemo binadamu. Haiingii akilini kuwa binadam ametokea mwenyewe tu bila kuumbwa.
Hata magari ,simu ,Computer n.k. Vina mifumo maalumu na huwezi kusema kuwa eti vimejitokeza tu kwa nasibu eti kwa sababu tu mgunduzi wake humjui kwa kumwona.
Watangulizi wetu walimwona Mungu kupitia Malaika au viumbe vya ajabu na vikakiri kuwa vimetumwa tu na Mungu Mkuu.

Mungu angejulikana na kila Mtu angedharaulika mana watu wangemzoea na kumuona wa kawadi.

Nimesema Mungu ni lazima awe Mtata na asiyeweza kujulikana kirahisi kama binadam
 
Hint: Mungu ataonyesha kuwa yeye ndio mpangaji na mwamuzi wa kila kitu na kwamba kisicho riziki hakiliki na zaidi riziki ya mtu haipotei.

Kuna wakati unakuja tutaanza kuwahurumia hawa watu na wakati huo huo Mungu atakuwa ametoa soma kwa dunia nzima kupitia Taifa letu.
Kwamba huenda tukawa na siku kadhaa za mapumziko?
 
Kuna watu mnateseka sana moyoni na Magufuli kuwa Rais.
Tunateseka mwili mpaka roho,
Tanzania kuna utulivu na siyo amani.
Amani huanzia ndani ya nafsi na kisha huonekana mwilini mtu akifurahi.
Ametunyang'anya amani ya nafsi zetu na furaha pia.
Zamani tulikula ming'oko na uwele,lakini tulikuwa na amani na furaha. Tulitembea kwa miguu kwa maili kadhaa huku tukicheka na kufurahi.
Safari ikiwa ndefu kijiji chochote waeza kulala maana wote tulikuwa ndugu.

Awamu hii ukionekana popote kila mtu anapata mashaka.
Ukiongekea siasa watu wanakukimbia.

Ukivaa sare ya cdm, ccm wanakuona gaidi mtumwa wa wazungu.
Ukivaa jezi za ccm,cdm wanakuona mtawala wa mkono wa chuma,muuaji mtekaji.

Ametuharibia umoja na mshikamano
Ukiona ccm anamsema cdm maneno machafu ujue hatanii anamaanisha
Mungu ataamua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom