Kabla ya kuja watu weupe waafrika tuliamini uwepo wa Mungu ila hatukuamini uwepo wa shetani

Kabla ya kuja watu weupe waafrika tuliamini uwepo wa Mungu ila hatukuamini uwepo wa shetani

Kama unamuamini Mungu wa kweli, sasa kabuli la babu yako nila nini?? unaenda kutafuta nn??
mtu aliyekufa anaweza kukusaidia kitu..? wakati yupo huko na yeye anasubr hukumu yake.


NAONA UNAFANYA OPOTOSHAJI TU
Wewe kwako huyo mungu wa kweli ni yupi, na anakusaidiaje
 
Waafrika tupo tulivyo sababu maisha yetu yapo connected na mizimu. Mizimu haitaki maendeleo thus ukijenga nyumba kijijini unalogwa, ukienda kijijini ukiaga ufiki salama.
 
Kwanza, ningependa kutoa pongeza kwa mleta mada na wachangiaji wote.

Pili na heshimu mchango na mawazo ya wachangiaji wote kuna msemo waswahili wanasema "muwamba ngozi uvutia kwake" nimeona wachangiaji wengi wanavutia kwenye MIZIMU kwa sababu ni asili kutoka kwao

ila naomba wanajamvi muangalie hii point yangu , KIUPANDE WANGU NAONA MZUNGU NI MTU ALIYE BARIKIWA SANA NA MUNGU .sisi wa afrika kuna muda tunakaa mpaka tunasema kwa nini yeye karusha ndege, kapitsha chuma ( meli) kwenye maji na vitu vingi sana

NIRUDI KWENYE MADA TAJWA HAPO JUU, kabla kuja kwa wageni tulikuwa na IMANI zetu za MIZIMU , MATAMBIKO na nk na tulikuwa na imani inafanya kazi LAKINI tangu aje mzungu ya dini zake tumezipokea na kuzifata tukaachana kabisa na MIZIMU

mu AFRIKA hasa MBONGO sio FARA kiasi icho aone pirau ale ugali kizembe ( wengi wape) , KWA BARAKA ALIZO PEWA MZUNGU NDIO IMETUFIKIA NA SISI KUPITIA WAO NA SISI TUMEKOMBOLEWA

MIMI NIMEMCHAGUA YESU NA NITANG'ANG'A NAYE HADI MAUTI ( KUTWALIWA ) KWANGU ....AMEN.

Asanteni.
 
Kuhusu Kuabudu bikira maria ilo mbona liko wazi ni Ni ufedhuli unao fanywa na makanisa ya kiroma wabudu sanamu.
pili aliitwa bikira keasababu alibeba mimba bira kumjua mwanaume
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] Mimba iliingiaje
 
Kama unamuamini Mungu wa kweli, sasa kabuli la babu yako nila nini?? unaenda kutafuta nn??
mtu aliyekufa anaweza kukusaidia kitu..? wakati yupo huko na yeye anasubr hukumu yake.


NAONA UNAFANYA OPOTOSHAJI TU
Ila Wazungu waliokufa kuitwa Watakatifu na watu wanafundisha kuwaabudu ni sawa?
 
Kuzuru makaburi ya wazee wetu sio mbaya wala haikatazwi hata kiimani,kinachokatazwa ni kuiomba roho ya marehemu, tunaomba kupitia jina la Yesu pekee.Kuyaenzi makaburi ni kuenzi historia yao maana still tunaunganiswa nao kupitia vitu walivyofanya mfano watoto hawa ni nyumba hizi ni za fulani.
Tunazuru makaburini kama historia na si kiimani.Mtu akishakufa kaburini pale ubakia mwili tu hasa mifupa roho yake haipo pale
Ila kupiga magoti mbele ya masanamu ya watakatifu wa kizungu na misalaba kuomba ni sawa si ndio??

#MaendeleoHayanaChama
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] Mimba iliingiaje
Sio mimba tu,hata nyumba ulio nayo ilikuwa form of energy kwenye austral world kabla ya kuvaa mwili.
Kupata mimba bila mwanaume ni ishu ndogo sana, kigoma mtu alijifungua kuku, Jesus God in flesh.
 
Kama unamuamini Mungu wa kweli, sasa kabuli la babu yako nila nini?? unaenda kutafuta nn??
mtu aliyekufa anaweza kukusaidia kitu..? wakati yupo huko na yeye anasubr hukumu yake.


NAONA UNAFANYA OPOTOSHAJI TU
Mkuu naona kila mtu asimame kwenye imani yake iliyoletwa na wazungu na waarabu,

Swali la kujiuliza ikiwa mababu zetu hawakuwa sahihi kuiomba mizimu je Romani wanaoomba marehemu wa waombee kwa Mungu usahihi wao ukowp

Au ndio tuludi kwenye msemo wa Kiswahili usemao kuku akinya kanya ila bata akinya kaharisha, ipo sala ambayo Roman huwa wanaisali kwenye Rozari takatifu

Mtakatifu Yosefu utuombee
Magdalena wak utuombe
Na majina mengine mengi hutajwa ili tu wawaombe na hiiyo niimani iliyo kwisha kujengeka katika waumini wa rc
Sasa ikiwa kwao ni ushaidi wa imani yao kutaja majina ya watakatifu walio kwisha kufa ili wawaombee

Sasa ikiwa ndio hiyvo je nini sasa tofauti ya hawa mababu zetu waliokuwa wakiomba mizimu na hawa wanaomba marehemu

Angalizo huu ni mjadala wa kuelimishana hivyo isijengeke dhana ya kashifa ya imani za watu🙏
 
Hili jambo linafikilisha sana....
Waafrika bado tunasafari ndefu ya kujikomboa

Kuna maswali yameulizwa hapo juu paka mada inapoa bado hayajapata ufumbuzi,mimi niliwahi uliza kwa viongozi wangu wa dini nikaishia kuchimbwa biti
 
Back
Top Bottom