Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Hatimaye nimefika...Jana nilibahatika kufanya maongezi na mzee moja wa zamani sana age inakimbilia kama miaka 90 now.
nilimuuliza maswali mengi sana yanayohusu imani ila tukaenda mpaka miaka ya nyuma kidogo kutokana na maelezo yake niligundua aya.
kuwa waafrika kabla ya kuja waarabu, wareno , waingereza, waberigiji, wafaransa, wahindi na wachina. waliamini uwepo wa mungu ila swala lilikuja pale kumuabudia huyo mungu.
Nini maana halisi ya neno "Mzimu"?
Mzimu ni marehemu, ambapo Kiafrika kiasili tuliamini kuwa wafu wapo karibu na Mungu hivyo tulikuwa tunaomba mizimu utusaidie maana wao wapo karibu na Mungu. Ni sawa na Wakatoliki wanavyoamini katika saints.
lakini kwenye dunia ya leo tunaamini
"Maana ya neno "Mzimu", ni Mashetani ambao ndio humuongoza kufanya maasi, wakati mtu anakata roho hao Mashetani hutoka, hao ndio "Mizimu". Mizimu ni Mashetani walio toka kwa WAFU, kutii Mizimu ni kutii Mashetani, na si kutii WAFU."
ila ukweli wa mambo ni kuwa neno SHETANI sio neno lenye asili ya kiafrica . Concept ya shetani imeletwa afrika. waafrika walikuwa hawaamini uwepo wa shetani.
Mzimu imefananishwa na shetani baada ya dini za kigeni kufika afrika ila
imani ya uwepo wa shetani imeletwa hapo mwanzo haikuwepo.
Waafrika wengi wanaamini mababu zetu hawakuamini Mungu bali mizimu. Kumbe sio kweli Mungu alikuwepo ila tuliamini ndugu zetu waliokufa walikuwa wanatuunganisha sisi na Mungu, hivyo ili maombi yako yafanikiwe unaongea na mizimu (marehemu wa ukoo wenu).
Waafrika tuliamini Mungu, ila tukaamini Mungu yuko karibu na wafu (mizimu/mababu na ndugu walokufa) ambao tuliamini wanaishi katika mibuyu na miti nk. Sio kwamba tuliabudu miti
Ndio maana dini za Kiafrika hazikuwa na wamisionari wa kusambaza kwasababu, kila mtu aliomba Mungu kupitia mizimu ya ukoo wao. Mizimu ya ukoo wa mwezako ulikuwa hakusaidii hivyo hakukuwa haja ya kusambaza dini za asili, kila mtu aliomba kikwao.
Ila watu weupe ndio wakatufunza kuwa Mungu kwa imani zetu sio sahihi. Kwahiyo wasingekuwa wao bado tungeamini Mungu kinamna yetu.
nakualika kaka Mshana Jr katika kutoa mawazo yako katika hili andiko
Kwa sehemu kubwa waafrika hatukuwa na Mungu mmoja japo kuna Mungu mmoja ndio alijulikana kama mkuu wa Miungu huyu akiwa ni mwanaume (Mungu jua) ambaye naye alikuwa na msaidizi wake mwanamke (Mungu mwezi)
Halafu ikafuata miungu mingine kulingana na hadhi zao, nguvu na nafasi zao kwenye jamiii
Hawa miungu waliombwa neema, tiba ulinzi, mvua, ukwasi, ushindi nk kwenye mambo yote ya kijamii.. Na iliaminika kwamba jamii yoyote ilipopatwa na jambo lolote baya basi mungu fulani alikasirika na taratibu za kimila zilifanyika kwenda kumuomba msamaha
Level ya tatu ni mizimu yenye nguvu ya kuweza kuwasiliana na mungu fulani.. Si kila roho ya mfu iliweza kugeuka roho ya mzimu wenye nguvu bali ni wale watu waliokuwa mashuhuri kwenye jamii kama
Wafalme
Watemi
Majemadari wa vita
Wazee wa kimila
Viongozi nknk
Hawa mafanikio yao kwenye lolote yaliunganishwa moja kwa moja na baraka za Mungu mkuu kupitia miungu mbalimbali, na hivyo kuaminika nguvu yao kwenye kufikisha ujumbe wa maombi yoyote kwa miungu kisha kwa Mungu mkuu
Maombi hayo yalifanyika sehemu maalum tu zilizoaminika kama makazi ya miungu/mizimu... Makazi hayo yakiwa ya kudumu ama kinyume chake
Level ya nne ni wazee wanaoaminika kuwa na hekima, usafi ama nguvu nyingine za ziada kwenye jamii.. Hawa walisimama kama viongozi wa kiimani kama ilivyo leo hii.. Na hawa ndio walitumika kufanya patano, kusuluhisha kesi za kijamii kutibu kiroho na kimwili nknk.. Na hawa ndio ambao wakifa hupanda level na kuwa level ya tatu
Level ya tano ni miungu/mapepo waharibifu, wenye ghadhabu, kisirani na waliojawa na hasira sana.. Hawa ni mizimu maroho yaliyogeuka kuwa na nguvu ya maangamizi kutokana na kuwa na mwisho mbaya/kikomo cha kuwa hasa kubwa likiwa mauaji ya kukusudia, mapigano, visasi nk
Hawa ndio kwa wazungu walipewa jina la shetani