Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake


Kwenye hii interview Dr alishazipa jina linalostahili hoja za namna hii.

Mleta mada alishalinganisha akina Mayele kuchezea timu zetu na wageni kuendesha bandari humu jukwaani na huu ni muendelezo tu wa argument za kipumbavu.
 
Soma uelewe sio kukurupuka tu.
 
 
Hilo zee lina "interest" zake sidhani kama hapa litakuelewa.

Linajidai halijui Mkapa hakuuza utu wetu kwa makaburu, wakati Samia ametoa bure utu wetu kwa mwarabu, ajabu lipo kimya.
 
Hebu mleta mada tuambie, mkataba upi wakati wa Mkapa uliwapa makaburu Exclusive Rights?!

Ukiwa mjinga usidhani kila mmoja ni mjinga kama wewe, hata kama unalinda interest zako kuficha uhuni tuliofanyiwa na msaliti, laana ya wajukuu wa hili taifa iko upande wako.
 
Umemaliza kabisaaa.
 
Mkapa amejuta sana kwa Matendo aliyowatendea Watanzania akiwa Rais na kusema angepata nafasi nyingine ya kuwa Rais asingerudia makosa yale!

Mwinyi: Najuta kuuza Loliondo
 
Asante kwa historia. Ila siyo sababu ya watanzania kutokuhoji mapungufu kwenye mikataba.
 
Mbona majibu yametoka..hukusikia?
Imesainiwa IGA.. intergovernmental agreement...Mkataba wa bandari lazima utakuwa na kikomo..na mda wa review utakapo sainiwa.. huelewi nini?Bunge limeridhia serikali iende kuingia mkataba.., mkataba halisi bado...
IGA Kati ya DPw na Tanzania?! Kwani Bandari ya Zanzibar siyo sehemu ya hiyo IGA wakati Zanzibar ipo ndani ya Tanzania?
 
Fanyeni utafiti kwanza,dar port ina berth 7 ya 8 ni ile oil terminal,kwa mujibu wa serikali hapo dar port pekee DP kapewa berth na 6 na 7 tu ambazo ni za cotainer terminal hivi angepewa kuendesha bandari yote ingekuaje!
 
Uwe na Akili. Iko Tofauti ya Mkataba unaogusa Sovereignty na hiyo mingine ya Kimanzese. Sovereignty ndio Taifa, Ndio Sisi. Uwe na akili.
 
Lakini pia tatizo la NBC ni sawa na RTC , UFI, URAFIKI, Tanganyika packers n.k.
Kwamba mashirika yalimilikiwa na serikali tena wakati wa ujamaa.
Kiongozi wa shirika si Meneja ni mwenyekiti wa CCM wa Tawi la kazini.

Pesa za shirika zilitumika kwenye mambo nje ya shirika kama mbio za mwenge na upuuzi wa aina hiyo.
Kukosekana kwa ushindani kulikuza uzembe kwasababu ya monopoly na NBC ilikuwa hivyo.

Hoja ilikuwa Mismanagement. Malalamiko ya kuuza NBC kwa makaburu hayakuwa ubinafsishaji, ilikuwa bei ya kuuza ambayo ilikuwa bure licha ya fedha za umma zilitumika kutengeneza infrastructure za NBC
Mkapa amekiri mara nyingi hadharani na kwenye kitabu chake kuwa ubinafsishaji kwa sehemu kubwa alikosea maana 80% ya mashirika ya umma yaliingia mifukoni mwa matapeli!
Hakuna shirika alilouza linaloonekana zaidi ya maghala kama kule Mang'ula.
In short Mkapa aliuza mashirika 400 kwa hasara tu hakuwa na plan ya monitoring baada ya kuuza.
Ben aliamini sector binafsi inakuwa tu kama uyoga ndio maana akatoa mashirika hayo bila kuwa na plan.
Hoja zile sile waliosimamia watu juu ya uwezo na aina ya mikataba ya hovyo ya ubinafsishaji ndizo zilikuja kuonekana wazi kweli waliopinga walikua na hoja tena kubwa sana.
Yes
Vipi NET group Solutions? ATCL? TRL?
Meremeta? Na mengine?
Nimeshangaa sana mleta mada hajagusa Net group ambayo imetia ulemavu Tanesco hadi leo
Meremeta n.k. Nadhani mleta mada The Boss hapa alighafilikiwa haikuwa makusudi
Shida yetu kubwa tunakimbilia sana kwenye petty issues when it comes to analysis
Kama ambavyo watu wanadhani ubinafsishaji wa Bandari unavyopigwa vita.

Issue si kutoa bandari bali makubaliano ambayo ni msingi wa majadiliano kuwa na loopholes nyingi kiasi kwamba Prof Kitila Mkumbo leo ameshaindwa kujibu maswali ingawa aliunga hoja mkono kule Bungeni.

Hoja zisizojibiwa ni nyingi sana
Mfano, watu wanauliza , je kutoa bandari za Tanganyika na kuacha za Zanzibar si kukiuka katiba?
Ni utaratibu gani unaotumika kuandika mkataba kwa jina la Tanzania bila kuigusa Zanzibar

Na kwanini linapokuja suala la mgao kama Mikopo na Misaada Rais SSH yupo mbele kuwaita Wazanzibar hili la bandari amewaweka pembeni, kulikoni?

Wizara inasimamiwa na Wazanzibar tukijua histotria chafu kama ile ya Loliondo?
Badala ya kujibu hoja, wenye hoja wanaleta vioja vya kumjadili Mbowe bila sababu
Mfano huu mkataba wa Tanzania na DP World ni wa hovyo usioelezeka! Hoja si kubinafsisha bandari Hoja ni mkataba wa hovyo!
100% ! watu wanataka kujua mengi maana hata mwanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza UDSM ataona matobo ya wazi. Ni kama vile Mbarawa aliletewa nyaraka na ikavuja kabla hajaisoma au aliisoma akaminya au aliisoma hakuelewa au aliisoma akishinikizwa! lakini Professor anatetea ubuyu ule.
Madini hadi leo yametufikisha wapi ukitulinganisha na Botswana na SA? Mbona kwao pia kuna sector binafsi?
HOJA sio ubinafsishaji hoja aina ya mikataba ya kishenzi ambayo nchi zetu zinaingia.
good question

Kuna mambo mengi yaliyojificha jificha yanayotia shaka. Spika anakuwa msemaji wa serikali na siyo kiongozi wa serikali bungeni Mh Waziri mkuu Mh Majaliwa . Mwanasheria mkuu wa serikali yupo kimya

Kuna maswali ya kujiuliza, ikiwa Wabunge wakiwemo wa Zanzibar walikwenda Dubai, wale wa Zanzibar walikwenda kufanya nini kwasababu huko Zanzibar hawana habari na DP.

JokaKuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…