Kinachonisikitisha ni kushindwa kufahamu kwamba uendeshwaji wa benki za kibiashara (Commercial Banks) ndani ya nchi, hutegemea sana sheria na sera za uchumi (Fiscal & Monetary Policies) ambazo zinaratibiwa na benki kuu ya nchi ya Tanzania. Mabenki ni makampuni, lakini uendeshwaji wake hauko sawa na makampuni mengine.
Hivyo unavyotoa mifano ya CRDB na NMB kufanikiwa, fahamu fika kwamba BOT imefanya kazi kubwa mno hadi hizi benki kusimama. Raisi Mkapa ataendelea kulalamikiwa kwasababu yeye aliziuza hizi benki kiholela jambo ambalo halikuwa sahihi kabisa. Halafu kama umefuatilia vizuri, kuna sababu nyingine kadhaa wa kadhaa, zinazofanya benki ya NMB kufanikiwa, mbali na mitaji ya wazungu.
Lakini mwisho kabisa nashangaa wewe umeshindwa kung'amua jambo rahisi kabisa ambalo hata mtoto wa chuo angeweza kuling'amua. Mkataba wa bandari na mkataba wa ubinafsishwaji wa mashirika ya ummah kipindi cha Mkapa ni tofauti kabisa. Kwenye mikataba mingi ya Raisi Mkapa, Tanzania bado inamiliki hisa za kutosha ambazo zinaipa nchi nguvu kubwa ya maamuzi hasa kwenye upigaji wa kura. Kubwa zaidi ni kwamba maamuzi ya mwisho ya usimamiz wa hizi benki uko chini ya usimamizi wa BOT na siyo wawekezaji wa nje.
Mkataba wa DP World, unainyang'anya Tanzania haki ya kufanya chochote kile. Tena hata kufikiria walishindwa wakasaini mkataba baina ya Tanzania na DP World ambalo ni shirika binafsi. Kule Djibouti, serikali iliunda kampuni ambalo liliingia ubia na DP World na kumiliki hisa zaidi ya asilimia 60%. Sisi huku tumefanya mambo ya hovyo kupita kiasi, ambapo zaidi ya kukusanya kodi hatuna chetu. Hivyo hata wafanyakazi wa bandari wanaweza kufukuzwa na tusiseme chochote kile.
Kikubwa mkataba huu wa bandari ni LOCK-OUT AGREEMENT, ambapo imewekwa bayana kabisa kwamba mashirika mengine ya ndani au kutoka nje hayataruhusiwa kuja kuwekeza kwenye bandari za Tanzania. Hivyo DP World wamepewa EXCLUSIVE RIGHT OF OWNERSHIP WHICH CREATES A MONOPOLY. Mtu yoyote yule mwenye akili timamu na mwenye uzalendo na hii nchi, kamwe hawezi kushabikia huu ufedhuli.
Kule Uingereza ambako haki za binadamu zimeshika hatamu, DP World ilifukuza maelfu ya wafanyakazi wa kizungu wa shirika la P&O Ferries baada ya kulinunua. Sasa huko ni Uingereza, hapa Tanzania unadhani kitawakuta nini wale wafanyakazi wa bandari ? Mambo mengine muwe mnatumia akili nyie watu, siyo matumbo. Sasa hebu nikupashe kidogo:
Mwaka 2020, serikali ya Djibouti ilifunguliwa mashitaka na shirika la DP WORLD kwasababu lilivunja haki yake ya umiliki wa bandari za Djibouti bila kuingiliwa (Breach of Exclusive Rights), kwasababu serikali ilitaka kulipa shirika la China Merchants haki ya kuwekeza kwenye bandari ya Doraleh. Serikali ya Djibouti na China Mechants ziliburuzwa kwenye mahakama za kimataifa na kuamriwa walipe dola za Kimarekani milioni 200.
Ikumbukwe China Merchants ndiyo shirika linalotaka kuanzisha mradi wa bandari ya Bagamoyo, lakini baada ya huu mkataba kupita hiyo haki hawana tena. Unafahamu nini kinaenda kutokea hapa ? Bandari ya Bagamoyo inaweza ikaenda kujengwa nchini Kenya na tusibaki tunaamini chochote hapa. Ikumbukwe mpango wa serikali ya Uchina kipindi cha Raisi Hu Jintao ni kwamba bandari ijengwe kule Kenya lakini wakaamua kujenga Tanganyika. Sasa hapa unadhani nini kitawazuia wakenya kuwaruhusu wachina wajenge Kenya ? Subirini muone...
MWISHO KABISA:
Leo nimemsikiliza Tundu Lissu akichambua kuhusu mkataba wa DP World, ambapo amesema kwamba huu ndiyo mkataba wa ajabu kuwahi kusainiwa na serikali ya Tanganyika tokea mwaka 1920. Mimi nasema amekosea na hajafanya tafiti za kutosha. Mkataba kama huu ulishawahi kusainiwa na serikali ya Muingereza, Mbelgiji na Mfaransa juu ya matumizi ya bandari ya Dar es salaam.
Mkataba ulihusisha makoloni ya Tanganyika, Rwanda, Burundi na Congo DRC na uliitwa THE BELBASE TREATY, ambao ulisema kwamba makoloni ya Rwanda, Burundi na Congo yataruhusiwa kutumia bandari ya Dar es salaam kwa kipindi kisicho na ukomo (Infinitely/Indefinate Time), huku wakilipa kiasi cha paundi 2 za Uingereza kwa serikali ya Tanganyika. Mwalimu Nyerere kawa Waziri Mkuu akaukuta huu mkataba, yeye na Mzee Lusinde akiwa waziri mwenye dhamana waliuvunja huu mkataba bila kufikiria mara mbili kwasababu ulilenga kuiumiza Tanganyika na kuuza uhuru wake.
Hii IGA baina ya Tanzania na Dubai, ina mahadhi hayohayo ya The Belbase Treaty, kwamba waarabu wapewe bandari zetu zote za Tanganyika kwa kipindi kisicho na ukomo. Halafu wakaenda mbali zaidi kusema kwamba "Even in case of state succession, a new state shall be bound by the same treaty." Wakimaanisha kwamba hata leo hii muungano ukivunjika, serikali ya Tanganyika itakuwa imefungwa na huo mkataba ambao umesainiwa na watu watatu kutoka Zanzibar. Sasa kama huku siyo kuiuza Tanganyika ni nini ?
NB 1: Kila siku nilikuwa najiuliza nini kilipelekea wafaransa (The Jacobins) wakachanganyikiwa na kuwa na hasira kiasi cha kumuua mfalme wao Louis IV na familia yake bila huruma, kumbe mambo huwa yanaanzaga hivihivi.
Kule Yugoslavia muungano wao ulikuwa na amani kwelikweli kipindi cha mkomunisti Josep Broz Tito, lakini huwezi kuamini jinsi ambavyo wakristo wa kutoka Serbia walifanya ukatili kwa kuua maelfu wa Waislamu kutoka Bosnia na Kosovo kisa tu hawa waislamu walikuwa wanataka uhuru wao, hivyo wakaanza kushirikiana na mataifa ya kiislamu kama Uturuki ili kuhujumu nchi. Hadi leo Serbia, Bosnia na Croatia ni maadui utadhani siyo ndugu (Slavs) waliowahi kuwa nchi moja.
NB 2: Ukweli tunaufahamu kwamba mbali na kusingizio cha kufungua nchi na kuita wawekezaji kutoka nje, nyuma ya hizi siasa za Raisi Samia kuna kaharufu kakali ka UDINI. Wengi mnamtete Samia kwasababu tu ni mwenzenu kwenye imani. Hata wengine wanaomponda wanafanya hivyo kwasababu za kidini, hata kama watapinga. Sasa kama mambo ndiyo yako hivi, siku siyo nyingi Tanzania itakuwa imejaa chuki kubwa mno ya DINI.
Watanzania meingizwa kwenye mtego na ninyi mmejaa mazima.....Nawapa pole!