Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

Unaangaalia sampuli tuu za sehemu walizofanya vizuri. Hivi huyo mkapa alishindwa nini kuanzisha bank na aziuze? Tena unajua hili jambo lilimliza nyerere? Je watanzania wazalendo wangeshindwa kuendesha bank hizo na kuzifanya kuwa kubwa? NMB unayo sifia ndio hii inayo tupangisha foleni?

By the way ningekuwa someone leo... ila kutokana na madhira yawawekezaji kutoka bala asia huko mufindi maisha yangu Tangu utoto yamekuwa ya shida sanaa. Siwez kuelewa mambo ya uwekezaji
 
Toka huu mjadala uanze, pande zote mbili za debate zinaongelea leaked agreement wewe unasema dunia ya leo iko transparent?
Leaking ni part ya transparency

Umesahau whistleblower kama part ya good governance?
 
Hilo ndo jibu la swali langu?
 
Hiki ni nini tena?
 
Umeandika mengi sana. Umesahau kusema Kwamba Mkapa alijutia maamuzi Yake..

Pia NBC Makosa mengi yalifanyika kwenye ubinafisishaji.


Halafu usilinganishe mkataba wa bandari na hizo mambo. Tanzania Bandari ni bandari na wanazitaka zote bahari, maziwa na nchi kavu milele na milele what the hell.

Banks tunazo nyingi sana options kibao, acheni uchuro waarabu wakafie mbele
 
Mkapa alianzisha mifumo mingi TRA ikiwemo wakati Awamu ya 6 ikibuni tozo kwenye Miamala ya kibenki.

Umenukuu wawekezaji walioletwa na Mkapa, walimiliki hisa chini ya 50%. Awamu ya 6, Ngorongoro na bandari haijulikani Serikali Ina hisa kiasi Gani!!!
 
kwanza mkataba wa bandari una shida gani?
 
TBL ilikuwa kampuni binafsi hata kabla ya Uhuru na ilikuwa ikifanya biashara vizuri tu kwa mafanikio.Ilitaifishwa na serikali ya Nyerere enzi za ujamaa hivyo Mkapa aliirudisha sekta binafsi ilipokuwa mwanzo.

Benki ya NBC pia ilitokana na kutaifishwa taasisi zote za kifedha zilizokuwepo mwaka 1967. Haikuwa benki iliyoanzishwa na serikali kutoka zero, Hivyo Mkapa alikuwa akifanya reset tu kuirudisha sekta binafsi.
 
Wamuombe radhi Role Model wangu BWM
 
Hivi kweli The Boss umemtumia akili zako zote kufanya mlinganisho huu na kuja na hoja hii ya kipumbafu kama hii? Swali linakuja kwako sasa; Je Kuna mfanano wowote wa kimikataba na ubia wa serikali kipindi cha mkapa na wawekezaji juu ya hizo banks ulizozitaja na ubia wa Sasa wa serikali na hawa DP World?
Hakuna haja ya kuingia ndani sana kwasababu vifungu vya masharti ya mkataba vimejiweka wazi tena kwa lugha rahisi kabisa. Kwa utanzania wako na uzalendo wako unadiriki kusema kuwa huu mkataba tutafaidika nao kwa vipengere hivyo vinavyoifunga nchi na kuinyima haki juu ya bandari zake hata mwekezaji akifanya maamuzi yoyote yale?
Wewe ni mjinga wa mwisho katika hili.
 
Now this is The Boss I used to know.
Jemima Mrembo come see the real The Boss
 
Wanaomtetea Samia wengi ni waislamu kwa sababu wameamua kufanya hivyo kwakuwa ni wa dini yao siyo kwa uzuri wa mkataba.

Aliyoyazungumza Rostam jana yalionyesha wazi maslahi yake ya wazi wazi.

Aliyoyazungumza Zitto jana ni picha halisi ya mtu tapeli na asiye na msimamo.

Tunaacha kujadili hoja za wakosoaji tunaanza kutafuta vijisababu vya kijinga jinga kudivert mjadala wa maana.

Lakini yote kwa yote Tanzania ni nchi yenye kundi kubwa la watu waliokufa kiroho na kubakiza viwiliiwili tu.
 
Majibu murua kabisa, tumtetee Samia kwa uzuri wa kazi zake siyo kwa dini yake.

Tusivae joho la dini na uzanzibar kwenye maslahi ya nchi
 
Watu wanashindwa kujadili hoja ya wanaopinga mkataba kwa sababu hata wao hawakubaliani nao ila wanaamua kujitoa akili tu kumtetea wa kwao.

Kwanini kila anayeunga mkono uwekezaji huu ana Baragashia tu ?

Jambo lenye tija kwa nchi linavishwa joho la dini na watu wenye fikra mfu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…