Mkuu unachokisema ni kweli lakini sio kweli ni maneno yaleyale ya tozo za miamala. Unachokisema ni sawa kama watanzania wangekuwa wamesambaziwa hiyo gesi nchi nzima na wanatumia gesi viwandani, kuzalisha umeme wa bei nafuu, kupikia, magari yao yanatumia ges badala ya diesel. Lakini mpaka Sasa ni zaidi ya miaka 20 Tanzania Ina gesi lakini watanzania wanatumia umeme ghali kuzalisha bidhaa, wanapikia mkaa na Kuni na wananunua mbolea kutoka nje. Wewe unadhani Kenya ni wazembe wa kiasi hiki?
Urusi inasafirisha gesi kwenda Ulaya lakini warusi wahatumia Kuni Kuni kupikia majumbani, hii ni tofauti sisi ambao tutasafirisha gesi nje wakati sisi wenyewe tukiwa bado tunatumia mkaa kupikia.
Wakenya wataichakata hiyo gesi na kuwauzia umeme, gesi ya viwandani, bidhaa nafuu za viwandani Sudani kusini, somalia na Ethiopia faster na kupata faida mara 12 ya sisi wenye gesi.
Hapa sisemi kuwa gesi isiuzwe nje bali ninachokisena ni Tanzania kuitumia gesi hii zaidi kuliko wengine katika uzalishaji bidhaa, kulinda mazingira na kwa kilimo hata kabla ya kuwauzia majirani zetu.