Meno ya rangi ya gold au rangi nyingine tofauti na nyeupe huwa ni kwa sababu ya wingi wa madini, mfano calcium ambayo chanzo chake kiasi kikubwa ni maji magumu, na pia aina ya vyakula hasa vinavyolimwa katika ardhi yenye hayo madini. Hayo meno huwa ni magumu sana na imara, sio rahisi kutoboka au kuharibika kama meno meupe.
Very rare mtu mwenye meno ya gold kunuka mdomo, labda awe hapigi mswaki.
Cha ajabu ni kwamba, watu wengi wenye meno meupe na wanaweza kuonekana na kinywa safi kwa sababu ya weupe wa meno, unakuta wananuka midomo.
Na jambo jingine, watu wanaonuka mdomo wengi huwa hawajui, unless atokee mtu ambaye yupo honest ajilipue na kumwambia mtu.
Kunuka mdomo husababishwa na vitu vifuatavyo:
1. Kutokupiga mswaki au kutokupiga mswaki vizuri, na hivyo kinywa hasa katikati ya meno kuwa na mabaki ya chakula, ambayo huoza na kuanza kutoa harufu. Uozaji huo huchochewa na bacteria waliopo mdomoni, wanakuwa catalyst wa kuyashambulia na kuyafanya yaoze haraka, mfano kwa kutengeneza dutu au chemikali kama acidi kutokana na mabaki. Hapa inategemea mabaki yanakaa mdomoni kwa muda gani, hao bacteria ni wengi kiasi gani, na pia wapo active kwa kiwango gani.
2. Kupendelea kunywa vitu vya moto sana mara kwa mara. Hii huua bacteria fulani ambao wapo kwa wingi sana mdommoni, kuwafanya waoze na mdomo au kinywa kuanza kutoa harufu.
3. Tatizo linaloanzia tumboni kwa sababu mbalimbali, mfano vidonda vya tumbo, cancer, etc.,
Kama tatizo la kunuka kinywa sababu ni namba 1, hilo huweza kumalizika kwa kupiga mswaki ipasavyo.
Kunuka mdomo ambako chanzo ni 2 na 3 huwa ni tatizo sugu sana. Ndio maana unaweza kushuhudia dada ana meno meupe na kinywa chake kinaonekana kisafi, lakini akiongea akiwa karibu na wewe unasikia harufi kali.
Wengine wanajua midomo au vinywa vyao hunuka, lakini wengi huwa hata hawana habari.