Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari

Si sahihi kusema hivyo kwa sababu hata wawekezaji wanakopa na mitaji inakufa. Mungu mwenyewe huwapa watu wake. Pia tukiwa wawekezaji wote nani atanunua kwa mwingine?
Mitazamo tu mkuu wangu, niwazacho mimi na wewe vinaweza tofautiana lakini wote tukawa na lengo la kufikia sehemu fulani nzuri.
 
Hakika umenena Robert!
 
Ndio kikubwa uwe njiani tu usijifungie ndani maana mtu wa kukupa mchongo wa kutoka ni mmoja tu. Unakutana nae kwenye harakati zako tu.
 
Hapo napingana na wewe Kikwete alitegemea urais na kweli akawa rais
Hapa kwa kikwete kuna cha kujifunza katika angle nyingine.

Kikwete aliutaka urais 1995 (kumbuka hii ilikuwa ndoto yake hapa ameshafanya lobbing za kutosha mpaka 1995)

Lakini Mungu akamwambia NO
umri bado unahitaji kuimarika zaidi kwenye hekima busara na subira.

Kikwete hakukata tamaa akaendelea na UTHUBUTU NA UJASIRI hatimaye

Ndoto yake ikafanikishwa na Mungu 2005 akawa president.

Mungu hubariki wenye Subira, wanyenyekevu na uthubutu.

Hivyo tusiache ndoto zetu ikiwa Mungu ametutaka tufikie destinations zetu.

Bahati hutukuta katika harakati zetu.

Mimi huwa namwomba Mungu anifanikishe mambo flani flani

Naona-ga kama ananicheleweshea ila nikajifunza kwamba.

Wakatu mwingine kabla hujainuliwa unapaswa uwe umeeondoa kiburi, madharau na umejua matatizo ya watu pia uwe na subiria, uvumilivu, unyenyekevu na hekima ili ukiinuliwa umkubuke Mungu uwatendee watu haki.


Lakini hili linashangaza zinaweza kuwa ni fikra tu but ukiangalia humu duniani
Kuna watu wamefanikiwa licha ya uovu wao na tabia zao mbaya.

Lakini hilo linatokea ili lile neno lipate kutimia "Mungu huwanyeshea mvua wenye dhambi na wasio na dhambi"
 
Sasa kama msaada wake hautegemei unamuomba au haumuombi, Utasemaje vijana hawafanikiwi kwa sababu ya Mungu?
Mambo ya kumuomba we inakuuma nini
We siumesema hakuna Mungu sasa unachukizwa nini ukisikia mtu anasema anamuomba Mungu

Watu tumefanikiwa sababu ya Mungu na ushuhuda tunao aya kasirika
 
[emoji817][emoji817]
 
Yesu Kwa miaka yake 33 duniani hakuwahi mmiliki nyumba Wala gari( punda) Kwa wakati Ule.

Nyumba na gari ni minor issue, muhimu ni tuutafute Ufalme wa Mungu na HAKIKA yake, hayo mengine tutazidishiwa.
Yesu alikuwa ni tajiri mkubwa tena mno...kufanya miujiza na kuwapa watu elimu ya kuendesha maisha haukuwa utajiri wa kawaida.

Yesu hakutaka kumiliki hivyo ulivyo orodhesha kwa kuwa ni Materials.

Hapa duniani alikuja kwa kusudi maalumu
 
Talk is cheap bruh, siku ukipitia chagamoto na mwenye nyumba anatishia kuifukuza familia yako ndio utelewa kwanini watu wana amani kwa kujenga nyumba zao za kuishi tu hata kama nyumba iko Chanika mwisho.
Mkuu mbona naelewa sana? Kweli unaniweka kwenye kundi la watu wasiojua changamoto za kulipa kodi? Nilichopinga mimi ni watu kuona kama ndiyo kielelezo cha mafanikio. Yaani nakubali kuwa ni mafanikio lakini siyo kama ndiyo umemaliza kila kitu. Je, utakubaliana na mimi kuwa mtu akiwa na utajiri mkubwa, unaweza kuishi kwenye nyumba za kupanga maisha yako yote na akahesabika ana mafanikio kuliko mtu mwenye nyumba na hana fedha? Kipi ni mafanikio sasa, nyumba au utajiri?
 
Ukweli mtupu [emoji48][emoji48]
kumbe bado tuna wanasalfasa katika nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…