Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Sina hasira bali nakueleza uhalisia.Usiwe na hasira tafadhali mkuu...plz
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sina hasira bali nakueleza uhalisia.Usiwe na hasira tafadhali mkuu...plz
Kuna kufuru mbaya zaidi ya hio?😂 😂 😂
Mitazamo tu mkuu wangu, niwazacho mimi na wewe vinaweza tofautiana lakini wote tukawa na lengo la kufikia sehemu fulani nzuri.Si sahihi kusema hivyo kwa sababu hata wawekezaji wanakopa na mitaji inakufa. Mungu mwenyewe huwapa watu wake. Pia tukiwa wawekezaji wote nani atanunua kwa mwingine?
Hakika umenena Robert!Habari za Jumapili!
Maisha sio Pouwa! Nakubaliana na wale wanaosema Maisha ni majaliwa. Na jitihada hazizidi kudura.
Wapo waliosoma kwa bidii mila hiyo na waliona taa ya matumaini kulingana na matokeo ya darasani waliyokuwa wakiyapata. Waliamini kuwa maisha yao na hatma yao ipo mikononi mwao kumbe sivyo.
Ilifika hatua wakawa wanadharau wale ambao walikuwa wanaonekana hawana mipango na mikakati kutokana na kutoipenda shule.
Wengi walifikiri kuwa kabla ya miaka 30 tayari wangekuwa wamekomesha jeuri na kiburi cha Umaskini katika maisha yao.
Tayari kichwani walikuwa na picha za jumba kubwa la kifahari ambalo walijua ndio watakayoishi. Bongo zao zilishakuwa na miundombinu ya flyover ambapo gari yao ilikuwa ikipita juu yake huku ndani akiwa yeye na Pisikali moja matata ambayo ndio mkewe.
Kwa wasichana, wao nao walikuwa na maisha yao mazuri katika vichwa vyao. Wanaume Handsome, warefu na wenye vipato na Watanashati walikuwa katika fikra zao.
Sasa miaka imekimbia, hawaelewi nini kimetokea. Matumaini yameyoyoma, ngumi ya matumpa upper cut moja matata imepiga kidevu vijana chali.
Hata zile ramani za majengo na magari walizokuwa nazo miaka hiyo zimefutika.
Yule Mwanamke mrembo akilini waliyemfikiria wangekuja kumuoa wanawaona kwenye magazeti, filamu na kwenye riwaya. Hakuna faraja tena, tumaini limeota mbawa. Wamejiunga kwenye chama cha faraja ya mpito cha Kataa Ndoa.
Hawakumbiki tena ndoto ya kuwa na familia bora baada ya kuyapata maisha mazuri yanayotamanika.
Ni Tekniko Knockout.
Hawakujua kuwa maisha yanakupa yale ambayo hujayaomba na yale ambayo huyataki. Tena maisha hukupa yale ambayo hukudhania kwamba ungekuwa nayo. Kwa sababu maisha ni Nasibu, maisha ni bahati tuu.
Sasa mipango imevurugwa na kuvurugika. Kila kitu pangala pangala! Hata kupanga hawataki kupanga tena. Hata wakisema wapange wanaona wanapoteza muda wao. Sasa ni bora liende túu! Wapo tayari kwa lolote na huo ndio mfumo wa maisha unavyotaka.
Mtu ambaye alipanga kabla ya miaka 30 awe na jumba na gari leo hii hata kodi ya chumba cha laki moja hawezi kuhimili. Unaweza kuona pigo alilopigwa ni zito kwa kiwango kipi.
Kijana, unapopanga mipango yako. Muombe Mungu
Suleiman aliwahi kusema;
Mhubiri 9:11 NEN
Nimeona kitu kingine tena chini ya jua: Si wenye mbio washindao mashindano au wenye nguvu washindao vita, wala si wenye hekima wapatao chakula au wenye akili nyingi wapatao mali, wala wenye elimu wapatao upendeleo, lakini fursa huwapata wote.
Acha Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ndio kikubwa uwe njiani tu usijifungie ndani maana mtu wa kukupa mchongo wa kutoka ni mmoja tu. Unakutana nae kwenye harakati zako tu.Life is not predictable.
Kikubwa fanya kazi kwa bidii na nidhamu ya pesa kuwa nayo.
Ukweli ni kwamba mtu anaekuja kukupa deal ni mtu mmoja tu na kupitia hapo unakuwa mtu mwingine tofauti kabisa kiuchumi
.
Hili nimejifunza kwa watu wangu wengi wa karibu walikuja kuinuliwa na watu
Hapa ndipo nilijifunza kwa udhiirisho kwamba mtu huinuliwa na mtu kupitia ukuu wa Mungu.
Hata mtu unae muona leo ana maisha mazuri ukifuatilia utakuta alikuwa kwnye harakati zake ghafla akatokea mtu akamshirikisha ndio ukawa mwanzo wa kutoka.
Kadhalika wahalifu nao hupiga tukio moja tu na kupitia hapo ndio mwanzo wa kutoka.
So pambana lift itakukuta njiani.
Sasa kama msaada wake hautegemei unamuomba au haumuombi, Utasemaje vijana hawafanikiwi kwa sababu ya Mungu?Msaada wake kwako hautegemei unamuomba au humwombi. Unamtambua au haumtambui.
Ukishatimiza alichokuletea imeisha
Isije kuwa wewe ndio mwehu ila unawaona wao wehu...Hii nchi wehu ndo wanatoboa faster
Hizi kauli za '100m ndogo sana' huwa zinanifurahisha sana.Mil 100 ni hela ndogo Sana huwezi kuacha masomo Kama form four au six maana Kwa nchi zetu wengi Elimu ndo umetufanya tuone Mwanga so the guy Was Right.
Neno lako sio sheriaKuna sehemu nime kulazimisha Mungu hayupo?
Au unaleta kimuhemuhe chako hapa?
Nimekwambia hivi, Mungu anaye pangia watu maisha Hayupo.
Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Hapa kwa kikwete kuna cha kujifunza katika angle nyingine.Hapo napingana na wewe Kikwete alitegemea urais na kweli akawa rais
Mambo ya kumuomba we inakuuma niniSasa kama msaada wake hautegemei unamuomba au haumuombi, Utasemaje vijana hawafanikiwi kwa sababu ya Mungu?
Ni mojawapo tu ya kufuru mkuu lkn siyo mbaya zaidi kuliko zote. Wapo wanaokufuru kwa kusema "Mungu hayupo".Kuna kufuru mbaya zaidi ya hio?
[emoji817][emoji817]Kuna kundi kubwa la vijana linasali na kumsifu huyo Mungu lakini bado maisha yao ni pangu pakavu tia mchuzi..
Hakuna mpango wa Mungu kwenye mafanikio ya binadamu.
Sera mbovu, siasa uchwara, mazingira ya rushwa, ujinga, elimu mbovu, serikali za hovyo ndio chanzo cha umaskini na ukosefu wa fursa kwa vijana wengi hasa barani Afrika.
Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Hakuna ndio sio ushamba ata kwangu na kwako hayupo jamaa yupo sahihi.Kwako wewe hakuna Mungu ni sawa
sasa usitake ulazimishe huo ni ushamba
Yesu alikuwa ni tajiri mkubwa tena mno...kufanya miujiza na kuwapa watu elimu ya kuendesha maisha haukuwa utajiri wa kawaida.Yesu Kwa miaka yake 33 duniani hakuwahi mmiliki nyumba Wala gari( punda) Kwa wakati Ule.
Nyumba na gari ni minor issue, muhimu ni tuutafute Ufalme wa Mungu na HAKIKA yake, hayo mengine tutazidishiwa.
Mkuu mbona naelewa sana? Kweli unaniweka kwenye kundi la watu wasiojua changamoto za kulipa kodi? Nilichopinga mimi ni watu kuona kama ndiyo kielelezo cha mafanikio. Yaani nakubali kuwa ni mafanikio lakini siyo kama ndiyo umemaliza kila kitu. Je, utakubaliana na mimi kuwa mtu akiwa na utajiri mkubwa, unaweza kuishi kwenye nyumba za kupanga maisha yako yote na akahesabika ana mafanikio kuliko mtu mwenye nyumba na hana fedha? Kipi ni mafanikio sasa, nyumba au utajiri?Talk is cheap bruh, siku ukipitia chagamoto na mwenye nyumba anatishia kuifukuza familia yako ndio utelewa kwanini watu wana amani kwa kujenga nyumba zao za kuishi tu hata kama nyumba iko Chanika mwisho.
Watu wengi hawaamini Mungu na wana maisha mazuri tu , na kuna wanaoamini nakusali ila wamepigika vibaya sana .Sina hasira bali nakueleza uhalisia.
Ukweli mtupu [emoji48][emoji48]Habari za Jumapili!