Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Tarehe 1 January 2022 dola moja ya Marikani (USD) ilikuwa sawa na Rubles 77 za Russia. Baada ya vita kati ya Russia na Ukraine mwezi Februari 2022, Russia iliwekewa vikwazo (sanctions) lukuki za kiuchumi na dunia inayoongozwa na Amerika na nchi za Ulaya. Lakini leo nchi hizi zilizoweka vikwazo zinalia kwa njaa na mfumuko mkubwa wa bei ambao haujawahi kutokea tangu dunia hii iumbwe. Nchi hizi sasa zinabadili USD 1 kwa Rubles 55 ili kupata chakula na nishati kutoka Russia. Mara nyingi zinalazimika kupata vitu hivi kupitia kwa nchi janja za China na India.
Hii ndiyo maana ya nchi kumiliki rasilimali asili zake. Nchi zetu nyingi zimeshindwa kufanya hivyo. Utakuta nchi kama Nigeria yenye rasilimali kubwa ya mafuta ya petroleum, mafuta yake yote huenda ughaibuni na yenyewe kulazimika kuagiza mafuta yake kutoka Uarabuni kama sisi. Gesi ya LNG inayovunwa Mozambique yote huenda ughaibuni na wao kuambulia kiduchu. Yote haya yanatokea kwa sababu nchi hizi siyo wamiliki wa rasilimali hizi kufuatana na mikataba waliyowekeana na hizo nchi tajiri za ughaibuni.
Sisi mambo yakoje? Jee huo mkataba wa mradi mkubwa wa LNG unasemaje? Jee tumejipangaje kulisha dunia kwani tuna ardhi tele na mito tele ya umwagiliaji? Ardhi yenye rutuba na malighafi tele ya kutengeneza mbolea.