Kabla ya vita USD 1 ilikuwa sawa na Rubles 77, sasa hivi ni sawa na Rubles 55. Tunajifunza nini kutokana na hali hii kama Taifa huru?

Ni aibu na fedhea kwa nchi zetu za kiafrica.. Tuna rasilimali za kutosha ila tunategemea vitu ving kutoka kwa watu wanao beba rasilimali zwtu..

Sisi africa tumekali u dini tu... Kucha kutwa ni kuangaika na dini zilizoletwa na wao wenyeww..

Tanzania tuna chuma ya kutosha huko liganga.. Ila mpka leo hatujaanza kuvuna na chuma imegundulika toka karne ya 17... Sasa inawezekanaje sisi mpka leo tushindwe kuchimba chuma kama walivyochimba karne ya 17
Hicho chuma kwanza ukiona mchanga wake unaweza kukitambua kuwa hicho ni chuma? Kila jambo na wakati wake.

Dunia haiishi leo kama hatuna teknolojia kwa sasa sio lazima tuchimbe, vizazi vijavyo watachimba. Kuliko kuwapa watu bure rasilimali zetu ni heri ziendelee kukaa ardhini. Sidi tuconcetrate na vitu ambavyo tuna comparative advantage huku tukijenga uwezo katika naeneo mengine.

Kwa mazingira haya ya sasa hakuna mkataba hata mmoja tutakaoingia ambao utaweka mbele maslahi ya nchi ila ya watu binafsi.
 
Sasa si uweke na takwimu, yaani unapinga tu kama aliyekimbia umande.
It is a known fact, hakuna haja ya kutumia nguvu kubwa kuweka takwimu yoyote, unless uwe hujui kitu a.k.a kichwamaji. Huyo aliyesema Tanzania ina gesi nyingi kuliko Russia na Ukraine combined ndio alitakiwa kuweka ushahidi hapa na sio kuweka maneno matupu.

Hata hao CCM hawajawahi kujisifia kuwa Tanzania ina gesi nyingi kuliko Russia na Ukraine combined.
 
Wakati MAGUFULI (R.I.P) Anajaribu kufanya mapinduzi makubwa ya viwanda na kuboresha kilimo chetu. Baadhi yetu tulikuwa busy kumchafua, kumtoa akili, kumtukana na kumtweza hadi Mzee wetu akadhoofika (depression) na kufariki. Na harakati zake tumeachana nazo. Tusubiri kuletewa msaada wa chakula hata na Somalia. Maana ndio Raha ya baadhi yetu kuona tunapendwa kwa kupewa vitu vidogo vidogo. Wakati ninakuwa ngano ilikuwa inalimwa BASUTU ARUSHA iliishia wapi?
 
Kadri Ulaya inavyozidi kuporomoka kutokana na Vita ni fursa kwa Marekani kwa kuwa Ulaya inageuka kuwa 'Kitalu cha uvunaji' cha America hasa ukizingatia wamejizuia kufanya biashara na Russia kwa hiyo America itaneemeka sana kwa hii vita na Hungaray wameligundua na wamejaribu sana kupambana kuzuia hali hiyo lakini wameshindwa
America wamebugi sana kwenye hii vita, wangekuwa na akili wala wasingetaka kui-prolong iendelee kupiganwa kwa muda mrefu kwa kuendelea kuwapa silaha Ukraine. Walitegemea kuidhoofisha Russia, lakini mambo yamekuwa kinyume, ruble inazidi kupanda thamani na uchumi wa Russia kuimarika, mfumko wa bei kwenye nchi magharibi ni wa kutisha, yani kila kitu kimeparaganyika kwa sasa. Kwa jinsi wamarekani walivyo wabinafsi watataka hali iendelee hivyo tu kwa sababu ya interests zao.
 
Ni aibu na fedhea kwa nchi zetu za kiafrica.. Tuna rasilimali za kutosha ila tunategemea vitu ving kutoka kwa watu wanao beba rasilimali zwtu..

Sisi africa tumekali u dini tu... Kucha kutwa ni kuangaika na dini zilizoletwa na wao wenyeww..

Tanzania tuna chuma ya kutosha huko liganga.. Ila mpka leo hatujaanza kuvuna na chuma imegundulika toka karne ya 17... Sasa inawezekanaje sisi mpka leo tushindwe kuchimba chuma kama walivyochimba karne ya 17
Cha ajabu hata fikra za kujitawala na kulinda maliasili zetu kujitegemea watu wengi wanategemea fikra hizi watupe wazungu. Mtu akipata elimu kutoka nchi za magharibi tunamuona ndo kasoma. Akitokea mtu wa kutuamsha kiuzalendo, nidhamu kazini, uwajibikaji, kupambana na rushwa, wizi, vyeti feki, mishahara hewa, mtu huyo anaonekana adui.

Tunafurahia kauli za " kuna pesa nyingi sana za wazungu za kuchukua" "ukitaka kula lazima uliwe" Eti wazungu watuambie bwawa la umeme JNHPP litaleta uharibifu uoto wa asili.Wazungu ambao mpaka leo hawajasaini mkataba wa kimataifa wa kupunguza carbon emissions wa Kyoto wala ule wa Paris. Hawa hawa wanauwa watu kule Iraq, Afghanistan, Libya, Syria lkn hatuwezi kuwaita madikteta wala kuwashitaki kwani hawajasaini ile protocol iliyounda ICC.

Juzi tu hapa manjegere chonde chonde wa TANESCO alisimamia uwashwaji wa mitambo Songas ili kuongeza uzalishaji umeme! Tunarudi kulekule! Usishangae kusikia Symbion nayo imewasha mitambo yake baada ya kulipwa bilioni 300! Watu wapige hela huku mwananchi akiendelea kunyonywa mpaka nyama ya ubongo. wakati huku tunaambiwa bwawa la stieglers litaanza kazi 2024 (kama hatujaletewa kisingizio chengine). Tunaburuzwa na sisi Bado tupo usingizini tukijidanganya kwamba Tanzania si kisiwa na kwamba tufanye kazi kwa bidii. Safari Bado ndefu, mengi tutayaona

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
America wamebugi sana kwenye hii vita, wangekuwa na akili wala wasingetaka kui-prolong iendelee kupiganwa kwa muda mrefu kwa kuendelea kuwapa silaha Ukraine. Walitegemea kuidhoofisha Russia, lakini mambo yamekuwa kinyume, ruble inazidi kupanda thamani na uchumi wa Russia kuimarika, mfumko wa bei kwenye nchi magharibi ni wa kutisha, yaani kila kitu kimeparaganyika kwa sasa. Kwa jinsi wamarekani walivyo wabinafsi watataka hali iendelee hivyo tu kwa sababu ya interests zao.
Na waarabu wamegoma amri ya US kuongeza uzalishaji mafuta ili bei ishuke kwani wao faida wanaitaka pia kipindi hiki ambacho bei iko juu. Political Economics...

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
Chuma kilichopo Liganga kinatosha matumizi ya dunia nzima kwa zaidi ya miaka 100. Kiasi cha gesi iliyopo kwenye ardhi na bahari yetu inaizidi ile iliyoko Russia na Ukraine combined. Lakini tunajiona wanyonge kwenye dunia hii na kuendelea kuwa ombaomba wa dunia kama walivyo ndugu zetu na watani zetu Wagogo kwa akina Ndugae! Tuna maelfu kwa maelfu wa tembo wenye nzuri zenye thamani kubwa sana duniani ambazo tungaliweza kuwa tunazivuna bila kuwaua tembo (bali tunawapandikizia za bandia). Thamani ya pembe za tembo 100 kwa mwezi ingalituwezesha kuteremsha bei ya mafuta ya petroli hadi kufikia Sh buku moja au hata jero kwa lita!!!
Wahindi wametupa mradi mkubwa wa maji. Unafikiri wanatupa bure? Pengine ndo wanahitaji udhibiti wa chuma chetu wapate global economic position ya kuuza chuma duniani

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
Tarehe 1 January 2022 dola moja ya Marikani (USD) ilikuwa sawa na Rubles 77 za Russia. Baada ya vita kati ya Russia na Ukraine mwezi Februari 2022, Russia iliwekewa vikwazo (sanctions) lukuki za kiuchumi na dunia inayoongozwa na Amerika na nchi za Ulaya. Lakini leo nchi hizi zilizoweka vikwazo zinalia kwa njaa na mfumuko mkubwa wa bei ambao haujawahi kutokea tangu dunia hii iumbwe. Nchi hizi sasa zinabadili USD 1 kwa Rubles 55 ili kupata chakula na nishati kutoka Russia. Mara nyingi zinalazimika kupata vitu hivi kupitia kwa nchi janja za China na India.

Hii ndiyo maana ya nchi kumiliki rasilimali asili zake. Nchi zetu nyingi zimeshindwa kufanya hivyo. Utakuta nchi kama Nigeria yenye rasilimali kubwa ya mafuta ya petroleum, mafuta yake yote huenda ughaibuni na yenyewe kulazimika kuagiza mafuta yake kutoka Uarabuni kama sisi. Gesi ya LNG inayovunwa Mozambique yote huenda ughaibuni na wao kuambulia kiduchu. Yote haya yanatokea kwa sababu nchi hizi siyo wamiliki wa rasilimali hizi kufuatana na mikataba waliyowekeana na hizo nchi tajiri za ughaibuni.

Sisi mambo yakoje? Jee huo mkataba wa mradi mkubwa wa LNG unasemaje? Jee tumejipangaje kulisha dunia kwani tuna ardhi tele na mito tele ya umwagiliaji? Ardhi yenye rutuba na malighafi tele ya kutengeneza mbolea.
Na fahamu pia kuwa Benki ya Urusi wanaidhibiti sana hiyo Rouble isipande zaidi kwaajili ya athari za export... Kupanda kwake kumewapa faida kubwa kwenye export ya bidhaa za nishati na mbolea. Ila wao wanasema ikipanda zaidi itaathiri ushindani wa export wa bidhaa nyingine kwenye soko la Dunia.. Ina Maana bidhaa za Urusi zitakuwa ghari zaidi kwa sababu ya thamani ya fedha hivyo kushindwa kushindana na bidhaa kutoka nchi shindani. Hivyo wanaidhibiti sana wao wenyewe isipande zaidi. Huo mchezo huwa anaucheza sana China ili bidhaa zake ziwe cheap zaidi kwenye soko la Dunia.
 
Chuma kilichopo Liganga kinatosha matumizi ya dunia nzima kwa zaidi ya miaka 100. Kiasi cha gesi iliyopo kwenye ardhi na bahari yetu inaizidi ile iliyoko Russia na Ukraine combined. Lakini tunajiona wanyonge kwenye dunia hii na kuendelea kuwa ombaomba wa dunia kama walivyo ndugu zetu na watani zetu Wagogo kwa akina Ndugae! Tuna maelfu kwa maelfu wa tembo wenye nzuri zenye thamani kubwa sana duniani ambazo tungaliweza kuwa tunazivuna bila kuwaua tembo (bali tunawapandikizia za bandia). Thamani ya pembe za tembo 100 kwa mwezi ingalituwezesha kuteremsha bei ya mafuta ya petroli hadi kufikia Sh buku moja au hata jero kwa lita!!!
Tembo Tena kuwanyofo pembe zao hpn utapigwa Vita na dunia nnzima
 
Hii vita imenifunza vitu viwili, tuwe makini kuchagua viongozi na umuhimu was kutumia rasilimali zetu
 
Hicho chuma kwanza ukiona mchanga wake unaweza kukitambua kuwa hicho ni chuma? Kila jambo na wakati wake.

Dunia haiishi leo kama hatuna teknolojia kwa sasa sio lazima tuchimbe, vizazi vijavyo watachimba. Kuliko kuwapa watu bure rasilimali zetu ni heri ziendelee kukaa ardhini. Sidi tuconcetrate na vitu ambavyo tuna comparative advantage huku tukijenga uwezo katika naeneo mengine.

Kwa mazingira haya ya sasa hakuna mkataba hata mmoja tutakaoingia ambao utaweka mbele maslahi ya nchi ila ya watu binafsi.
ndicho alichopanga raid wa awamu ya kwanza walipoingia walipoingia viongozi wengine wakaamua kutuuza
 
Tarehe 1 January 2022 dola moja ya Marikani (USD) ilikuwa sawa na Rubles 77 za Russia. Baada ya vita kati ya Russia na Ukraine mwezi Februari 2022, Russia iliwekewa vikwazo (sanctions) lukuki za kiuchumi na dunia inayoongozwa na Amerika na nchi za Ulaya. Lakini leo nchi hizi zilizoweka vikwazo zinalia kwa njaa na mfumuko mkubwa wa bei ambao haujawahi kutokea tangu dunia hii iumbwe. Nchi hizi sasa zinabadili USD 1 kwa Rubles 55 ili kupata chakula na nishati kutoka Russia. Mara nyingi zinalazimika kupata vitu hivi kupitia kwa nchi janja za China na India.

Hii ndiyo maana ya nchi kumiliki rasilimali asili zake. Nchi zetu nyingi zimeshindwa kufanya hivyo. Utakuta nchi kama Nigeria yenye rasilimali kubwa ya mafuta ya petroleum, mafuta yake yote huenda ughaibuni na yenyewe kulazimika kuagiza mafuta yake kutoka Uarabuni kama sisi. Gesi ya LNG inayovunwa Mozambique yote huenda ughaibuni na wao kuambulia kiduchu. Yote haya yanatokea kwa sababu nchi hizi siyo wamiliki wa rasilimali hizi kufuatana na mikataba waliyowekeana na hizo nchi tajiri za ughaibuni.

Sisi mambo yakoje? Jee huo mkataba wa mradi mkubwa wa LNG unasemaje? Jee tumejipangaje kulisha dunia kwani tuna ardhi tele na mito tele ya umwagiliaji? Ardhi yenye rutuba na malighafi tele ya kutengeneza mbolea.
Mkuu,
Usijidanganye. Uchumi wa nchi haupimwi kwa pesa ya nchi kupanda au kushuka peke yake. Kuna factors nyingine nyingi sana.

Kwanza ili kuzuia ruble isianguke Bank kuu ya Russia ilipandisha interest kutoka 9.5% mpaka 20%. Niambie hayo ni maumivu kiasi gani kwa wananchi wenye mikopo? Imagine leo hapo Tanzania interest ipandishwe kwa siku kwa asilimia 10.5.

Pili wameweka masharti magumu kununua pesa za nchi za nje. Unatakiwa kulipia tozo asilimia 30. Yaani ukitaka kuuza rubble laki moja kabla hujaingia mambo ya exchange rate, serikali huchukua elfu 30 kama tozo. Unabakiwa na elfu sabini ndio unabadilisha kwenda pesa ya nje.

Tatu, sasa kuna vikwazo kwahiyo Russia hainunui tena vitu nje. Ina maana mahitaji ya pesa za nje kununulia technologies, parts, kwenda utalii, ndege zao kuwa nje na kutumia pesa za nje hakuna. Kwahiyo nchi imefungiwa na mahitaji ya pesa za nje ni madogo mno.

Nne, Russia wamelazimisha kila mtu anaponunua kitu Russia atumie Rubble, kwahiyo kwa wafanyabiashara wa nje wanahitaji rubble hivyo mahitaji ya rubble ni makubwa kuliko mahitaji ya dola.

Tano, inflation ya Russia mwaka huu inategemewa kuwa asilimia 23. Hayo ni maumivu makubwa mno kwa wananchi. Angalia TZ tunavyopiga kelele kuhusu vitu kupanda.

Vitu vyote hivyo kwa ujumla, ukivipeleka kwa mwananchi wa kawaida wa Russia vina maumivu makubwa maana unemployment imeenda juu. Parts mbalimbali kwenye viwanda hakuna hivyo baadhi ya viwanda vinapunguza wafanyakazi.

Kwahiyo kwa kesi ya Russia usione kupanda kwa rubble ukafikiri uchumi wao unapanda. In fact uchumi kwa mwaka huu umesinyaa kwa asilimia 15
Tarehe 1 January 2022 dola moja ya Marikani (USD) ilikuwa sawa na Rubles 77 za Russia. Baada ya vita kati ya Russia na Ukraine mwezi Februari 2022, Russia iliwekewa vikwazo (sanctions) lukuki za kiuchumi na dunia inayoongozwa na Amerika na nchi za Ulaya. Lakini leo nchi hizi zilizoweka vikwazo zinalia kwa njaa na mfumuko mkubwa wa bei ambao haujawahi kutokea tangu dunia hii iumbwe. Nchi hizi sasa zinabadili USD 1 kwa Rubles 55 ili kupata chakula na nishati kutoka Russia. Mara nyingi zinalazimika kupata vitu hivi kupitia kwa nchi janja za China na India.

Hii ndiyo maana ya nchi kumiliki rasilimali asili zake. Nchi zetu nyingi zimeshindwa kufanya hivyo. Utakuta nchi kama Nigeria yenye rasilimali kubwa ya mafuta ya petroleum, mafuta yake yote huenda ughaibuni na yenyewe kulazimika kuagiza mafuta yake kutoka Uarabuni kama sisi. Gesi ya LNG inayovunwa Mozambique yote huenda ughaibuni na wao kuambulia kiduchu. Yote haya yanatokea kwa sababu nchi hizi siyo wamiliki wa rasilimali hizi kufuatana na mikataba waliyowekeana na hizo nchi tajiri za ughaibuni.

Sisi mambo yakoje? Jee huo mkataba wa mradi mkubwa wa LNG unasemaje? Jee tumejipangaje kulisha dunia kwani tuna ardhi tele na mito tele ya umwagiliaji? Ardhi yenye rutuba na malighafi tele ya kutengeneza mbolea.
 
America wamebugi sana kwenye hii vita, wangekuwa na akili wala wasingetaka kui-prolong iendelee kupiganwa kwa muda mrefu kwa kuendelea kuwapa silaha Ukraine. Walitegemea kuidhoofisha Russia, lakini mambo yamekuwa kinyume, ruble inazidi kupanda thamani na uchumi wa Russia kuimarika, mfumko wa bei kwenye nchi magharibi ni wa kutisha, yaani kila kitu kimeparaganyika kwa sasa. Kwa jinsi wamarekani walivyo wabinafsi watataka hali iendelee hivyo tu kwa sababu ya interests zao.
Ukiwa na akili ndogo utafikiri ni hivyo. Uchumi wa Russdia kwa mwaka huu tu wa 2022 utasinyaa kwa asilimia 15.

Interest rate imepnda kutoka asilimia 9.5 mpaka 20%. Unemployment imepanda juu.

Nchi imefungiwa na watu wake wengi hawatoki. Kwa mtu aliyeko Russia kuna madhara mengi sana ila Russia hawana haki hata ya kupiga kelele. Ni udikteta kule.
 
Biden alikuwa anakenua kuona jinsi ruble ilivyokuwa inaporomoka baada ya sanctions zao. Yule bastard sijui anajisikiaje sasa kuiona ruble imeimarika kuliko ilivyokuwa kabla ya sanctions!
Hata sisi tukitaka leo tunaweza kuipandisha shilingi kwa dola. Ila kwa kufanya hivyo tutaumiza mno wananchi wetu. Tukiweka interest rate asilimia 30 pesa zote zitarudi benki na mahitaji ya kununua pesa za nje yatapungua mno maana tuitakuwa hatuagizi chochote toka nje.

Uzalishaji utashuka na unemployment itaongezeka.

Uchumi sio rahisi hivyo kama mnavyoona eti kisa rubble imepanda. Rubble imepanda kwasababu Putin kachukua hatua kali kali, Kuuza rubble sasa unakatwa tozo asilimia 30.

Hivi leo Tanzania waseme kuuza shilingi pesa za nje unakatwa tozo asilimia 30, kuna mtu atauza tena shilingi?
 
Hii vita imewafaidisha sana Urusi kiuchumi kuliko kuwaathiri hasa kutokana na vikwazo.
Sio kweli ndugu yangu. Uchumi wa nchi haupimwi kwa kupanda au kushuka tu kwa fedha. Unapimwa kwa maisha ya kila mwananchi kwa nchi husika. Russia mwaka 2022 uchumi utasinyaa kwa asilimia 15. Unafikiri nini madhara yake kwa raia?

Russia interest imepanda kutoka asilimia 9.5 mpaka 20%, je nini madhara yake kwa raia wa kawaida?

Viwanda vinakosa parts na kupunguza uzalishaji, nini madhara yake kwa raia?
 
Back
Top Bottom