Kabul Airport waambulia ndege na magari mabovu

Kuna documentary niliona waingereza wakiharibu vitu wakati wakiondoka. Hadi visu vinakatwa. Nyaya zinakatwa. Bunduki zinasagwa, risasi zinakaangwa nk.
 
Kwanini USA hawakuzichukua hizo ndege zao na Halikopta?

Kwanini waliamua kuziacha Afghanistan hata kama wameziharibu?

Maana mpango wa wao kuondoka ulishatangazwa na Biden tena mpaka tarehe ya kuondoka ilisha julikana mapema.
Pengine,gharama za kuzisafirisha ni kubwa kuliko kuziharibu..Na ikumbukwe nikama walihitaji ya muda zaidi,Taliban waliwakatalia..
..Ni dhahiri kuna vitu waliondoka navyo,na ni kweli kuna vitu wameacha vingine vikiwa vimeharibiwa na vingine vizima kabisa..


Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Una akili sana we jamaa.
 
Zitatengenezwa tu na zitatumika tena usicheze na taliban
Hawa waarab Hawa na binamu zao waajemi,kwanini wasiungane wwnzishe vita ya tatu ya Dunia,Afghanistan,Iran,Saudia,Qatar,Pakistan,Malaysia,Uturuki,Misri,Syria,na washirika wao Urusi,china waungane wachapane na US na binamu yake UK na Ulaya,na Israel,Ili tueshimiane hapa duniani.
 

Kwenye hiyo link uliyoweka kuna sehemu Wenyewe usa wanasema hivyo vitu sio deal wala sio tishio kwa usalama wa usa …"It is not the type of equipment that will be of great strategic use to any force, and does not represent a significant threat to US forces or the militaries of neighbouring countries."

Kwahiyo Iran anaona USA wajinga kwa kuacha hayo magali [emoji23][emoji23]
 
Hapana kuna ndege nyingi zimeachwa na us army
 
Hawahitaji huo uchafu kubazi na mtutu wa kirusi na kanzu + ndevu ni uanaume tosha,kwa lugha nyingine tunaita man to man.
 
Hata katika baadhi ya nchi za afrika zilipopata uhuru,wazungu waliwazibia baadhi ya mijengo na kuzimiwa umeme.
Taliban waziweke makumbusho hizo hedicofta samahani ni helicopter ili watu walipie kwenda kuziona.
Ombi langu kwa Taliban. Tunawaomba Taliban msiweke tozo mpya ya miamala
 
Mimi kitu kimenifurahisha ni kua Mabeberu wamerudi kwao baada ya miaka 20 ya kula kapa...Mabeberu waaenda kwa nchi za wenyewe na kujifanya wajua kila kitu!!!, wametia akili sasa, watafute pahali pengine kwenda kutest vyombo na wanajeshi wake. Mtaliban ni mkavu.......imagine Mrusi pia alioga hapo kandahar!
 

Nilisema Mmarekani ni mnafiki watu wengi hawakunielewa. Leo wamekuja na hoja ya kushirikiana na Taleban ila wanasema hawataitambua kama serikali halali.

Yaani baada ya kujifanya kupigana na Taliban kwa takriban miaka ishirini, uharibifu wote huo, mauaji hayo yote! Marekani anakuja kushirikiana na Taliban? Huu upuuzi unatakiwa kushabikiwa na maduwanzi tu.

Hata kama wameacha magofu bado ukweli uko pale pale, Marekani imeshindwa na kuondoka Afghanistan kwa aibu.

Hakuna taifa litakaloliogopa Marekani tena. Wana PR tu ila nguvu ya vita labda teknlogjia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…